Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Soda mbaya zaidi ni zile zinazozwa kwenye chupa za plastiki, fursana, azam cola, nk.

Enzi zetu tulikuwa tunakunywa soda za chupa siku za sikukuu na maji ya mtungi, matatizo ya kisukari na pressure yalikuwa machache sana.
 
Urongo mtupu! Tunyweni soda baridi wandugu,, hii ni vita ya kibiashara kati ya pombe na soda!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] unajifanya kichwa ngumu sio
 
Nashangaa wengine ndo tunasikia leo habari hizi! acha kunywa soda utaona utakavyopunguza matumizi ya kuto kwenda hospitali. kiwango kikubwa cha sukari kilichopo ndani ya soda kina leta madhara makubwa sana kiafya. Kinywaji salama ni maji tu! ndani ya mwili wanasema kunatakiwa kusafishwe, kama vyombo unasafisha kwa maji safi, je mwili wako ndo unausafisha kwa soda? kama mmea unaupa maji ili ukue na si soda, kwa nini wawapa wanao soda? tafakari
 
Kila kitu kina madhara mwilini endapo kikizidi,Hata maji yenye PH 7 yana madhara yakizidi,CHa msingi tufanye mazoezi kuweka mwili fiti,kuondoa sumu tunazokula na kunywa.
 
Utashangaa kuona wagonjwa wanapelekewa soda wodini na jamaa zao eti waongeze Damu............!!! kazi kweli kweli.........


Hahahaa Mkuu umenichekesha. Tena unakuta Jamaa/wauguzi wamekomaa kabisa ati "mgonjwa mleteeni na soda apozee dawa". Huwa nachoka sana.

-Kaveli-
 
naona jamaa kaamua kutoa thread hii msimu wa sikukuu

msimu mzuri wa soko la soda na vinywaji balidi
 
Nikiskia mtu kafa kwa kunywa soda basi nitaziacha
 
Naona watu wanajibu kishabiki sana, kiukweli soda ni mbaya mbaya sana kama unaweza kuiepuka acha mara moja.
 
Back
Top Bottom