SoC02 Madhara yatokanayo na matumizi holela ya dawa za kuongeza nguvu za kiume

SoC02 Madhara yatokanayo na matumizi holela ya dawa za kuongeza nguvu za kiume

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 26, 2022
Posts
6
Reaction score
3
MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI HOLELA YA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME

UTANGULIZI
Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya sehemu za siri za mwanaume kuwa na uwezo mdogo au kutokuwa na uwezo kabisa wa kuhimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Tatizo hili limekuwa kubwa katika jamii na kwa kufuata mkumbo kumeibuka matumizi mabaya ya dawa za aina mbalimbali zikihamasishwa kurudisha nguvu hizo.

Mifano ya dawa hizo ambazo zimejulikana sana hapa nchini zikitumiwa na rika zote ni kama vile MKONGO, VIAGRA, CIALIS, VARDENAFIL na AVANAFIL. Na kati ya dawah zo nne, tatu zimesajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa nchini (TMDA) na zina majina tofauti kama vile Sindenafil, Evoke, Erecto, Zwagra, Silment, Njoi, Viagra na Levitra.

Dawa hizi hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu ndani ya mishipa ya sehemu za siri au uume kwa kuongeza kiwango cha damu hivo kufanya uume uwe na damu ya kutosha na kuuwezesha kufanya kazi vizuri. Kwa kawaida kitabibu hizi dawa zinatumika kutibu wanaume wenye uwezo mdogo au wasiokuw na uwezo kabisa wa kuhimili tendo la ndoa kwa mda mrefu. hata hivo hatari ni kwamba wanaume wengi hutumia dawa hizo bila ushauri wa daktarin huku kukiwa na madhara makubwa kwa watumiaji. kwa sababu wananunua dukani na kutumia bila kufata hata dozi

Sambamba na hilo wazee wengi hutumia dawa hizo kwasabu kadri umri unavyosonga mwanaume huwa anapoteza nguvu au uwezo wa kushiriki tendo la ndoa hii inatokana na kupungua kwa mzunguko wa damu na pia mishipa inanza kuchoka lakini ulishaji wa mbegu unabaki palepale hali hiyo hufanya wanaume ambao umri umeenda kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha wanafanya tendo hilo kama walivokuwa vijana hasa pale wanaposhiriki na mabinti wadogo na tatizo linakuwa kubwa kwa kuwa wengi hawajui madhara yake.

Kwa tathimini za TMDA, utumiaj wa dawa hizo kwa wanaume umekuwa ukiongezeka siku hadi siku hali inayoonesha kuwa wanaume wengi wameathirika na tatizo la upungufu wa kiume.

Swali la kujiuliza ni kwamba je hizo dawa zinafanya kazi unapozitumia?
Kwa mujibu wa tafiti dawa hizi hazitafanya kazi moja kwa moja au vizuri endapo tatizo hilo la kupungua kwa nguvu za kiume limetokana na kuathirika kisaikolojia.mfano kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, kutokujiamini, woga au kuwa na hofu ya kimapenzi na mwenza wako .tafiti zimeonesha kuwa dawa hizi hazitibu kabisa hayo na haziongezi hamu au shauku ya kufanya mapenzi.

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI HOLELA
Dawa hizo husababisha kusimama kwa sehemu za siri za mwanaume kwa muda mrefu hali inayoweza kusababisha maumivu ya sehemu hizo kwa muda mrefu ambapo lisipodhibitiwa kwa haraka linapelekea kuharibu mishipa laini iliyoko ndani ya sehemu hizo kitaalamu huitwa corpus cavernosum smooth muscle ambayo inasababisha uume uweze kusimama baada ya kupumzika ili kuruhusu damu ikusanyike kwenye cavernosum space ambapo baada ya kujikusanya kwa wingi huepelekea uume kusimama na kumwezesha mwanaume kuweza kushiriki tendo la ndoa kiufasaha zaidi. Kwasababu hiyo endapo hii mishipa ikaharibiwa na hizo dawa itashindwa kufanya kazi na kupelekea uume kushindwa kusimama kabisa hata kama mhusika atatumia dawa hizo tena.

Madhara mengine yanayosababishwa na hizo dawa ni pale ambapo zikatumika sambamba na dawa zinazotibu maumivu ya moyo, ambapo husababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa shinikizo la damu, kupata kizunguzungu, kuzimia, mshtuko wa moyo, kiharusi, matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, maumivu ya kichwa, matatizo ya macho na mwishowe kupoteza uhai.

Kwa ufafanuzi zaidi juu ya madhara ya dawa pendwa zinazotumiwa na watanzania kwa lengo la kuongeza nguvu za kiume au matumizi mengine nje ya hayo kwa wale wasio na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ambazoni ni Viagra zinavopelekea madhara makubwa

Viagra (sildenafil)
Kwa mara ya kwanza dawa hii ilikuwa inatumika kutibu tatizo la pressure lakini ilionesha maajabu sana pale ilipoleta natokeo ya kuwafanya wagonjwa wa kiume kua na nguvu nyingi sana za kusimamisha maumbile yao ya uzazi baada yah apo zikazuiliwa kutumika mahospitalini lakini baadae zikafanyiwa uchunguzi na zikarudishwa rasmi kwaajili ya watu wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ambapo walikuwa wanapewa chini ya uangalizi wa madaktari waliokuwa wanawapa ushauri ili kuwafanya wajiamin kuwa wanauwezo wa kufanya vizuri katika tendo hilo

Lakini kwa sasa watu hutumia hata kama hana tatizo la mfumo wauzaziambapo inapelekea kupata madhara makubwa ambapo kwa watu wanaotumia Viagra bila ushauri na huku akiwa na matatizo mengione ya kiafya yuko hatarini kupoteza uhai wake

Kwa sababu kadri mtu anavotumia Viagra ndivyo tatizo linazidi kua baya zaidi ambapo inampelekea asimamishe kwa mda mfupi hivyo akitaka kufanya mapenzi siku nyingine lazima azimeze tena hali hiyo ya kumfanya azimeze kila wakati inamfanya kuwa tegemezi hali ya kumfanya azidi kuongeza dozi yake ili apate nguvu zinazomtosheleza kila wakati mwisho wa siku dawa hizi hutengeneza sumu mwilini na kuua kabisa nguvu za kiume

Mtu anayetumia Viagra yuko hatarini kupata ukiziwi, kupoteza uwezo wa kuona (kutokana na kwamba dawa hizi huua baadhi ya vichecheo vinavyofanya kazi yakusafisha mwanga na picha kuelekea katika mfumo wa fahamu kuharibiwa na dawa hizi

HITIMISHO

Dawa za kuongeza nguvu za kiume hutumiwa kiholela sana hapa nchini ambapo hupelekea madhara makubwa sana kwa sababu watu wengi hawana elimu juu ya madhara yatokanayo na dawa hizo hivyo ushauri wangu ningeiomba serikali iliangalia suala hili na ianzishe kampeni mbalimbali juu ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusiana na matumizi sahihi ya dawa hizo na madhara yatokanayo ya matumizi holela.kwa sababu asilimia kubwa ya wanaume nchini hutumia dawa hizo kiasi kinachopelekea upotevu wa nguvu kazi ya taifa kutokana na mdhara yanayowapata.

Pia serikali inatakiwa ipige marufuku uuzaji holela wa dawa hizo kwenye pharmacy ambapo watatakiwa wauze kwa vibali maalumu na kwa mgonjwa tu na siyo vinginevyo,
 

Attachments

Upvote 1
Back
Top Bottom