Zama zinabadilika kila uchao...
Zamani wazee wetu walikuwa wanakula mtama umechanganywa na ulezi, hio ikapita.
Wakaja wakoloni wakaleta muhogo toka Amerika ya Kusini, mtama na ulezi vikapunguza umaarufu, wazee wetu waliwashangaa sana watu wa kizazi chao kwa kukumbatia muhogo na kuacha mtama na ulezi wakasahau kuwa hata wao waliacha kula mizizi na matunda wakakumbatia mtama na ulezi.
Baadaye yakaingia mahindi kutokea huko huko kwa mkoloni, watu wakaacha muhogo wakachangamkia mahindi, wazee wa wakati huo wakawashangaa sana kwa nini kuacha muhogo kukumbatia mahindi "vyakula vya watu weupe visivyo na faida mwilini"??.
Baadaye ukaingia mchele, wazee wanaokula mahindi wanawashangaa sana wanaoukumbatia mchele kwa kuwa ni "chakula cha kuja".
Sasa ulaji wa chipsi unaingia kwa kasi kama vile ambavyo vingine viliingia kwa kasi na watu wakashangaa pia kwa nini watu kukumbatia "mavyakula ya wazungu".
Ni zama tu zinabadilika mkuu, baadaye tutaingia kwenye ngano na mavyakula ya makopo na watu watapuzia chipsi pia.
Madaktari wamejikita kueleza madhara ya chipsi badala ya kutueleza na faida zake pia, haya ni madhaifu makubwa sana katika kuleta judgement ya kitu, huwezi kusikia one sided story peke yake.
Zama mpya zinakuja, za zamani zinapotea, lakini all in al hakuja jipya chini ya jua.
Vijana kuleni kiepe yai, kwa kuwa hizi ni zama zenu.