Madhumuni ya Rais yalikuwa kuifanya bandari ya DSM kuwa ya Mwendo kasi ya kisasa kama SGR. Watekelezaji wamechemsha kwa kuanza na International Treaty

Umeandika kitaalamu Sana I wish wangepitia hili bandiko


Alfu Ni vzr hili bandiko ulipeleke kule kwenye story of change utaibuka mshindi moja ya makala mazuri Sana kuisoma mwaka huu

Tena mm naomba unitumie soft copy ili itoke ktk gazeti la mwananchi jtatu

Naomba mkuu
 
Bora umgesoma tu alichokileta huyu bwana Ni kitu kikubwa mno
 
Soma Hadi mwisho kilicho andikwa na msomi huyu
 
Sasa bwana fuma.....

Alichokiandika mleta hoja umeisoma Hadi mwisho au umekurupuka tu

Soma jamaa kaandika vitu vya msingi Sana
Soma acha uvivu
 
Mnapofeli ndio hapo.. Kwanini haujataka kusoma hili andiko lote... Kuna aina tofautitofauti za uandishi, mimi nakuomba rudia tena kulisoma andiko lote. Mama katetewa kwani nia ya aondoke mwenyewe bila kufukuzwa.
Uko sahih Sana mijitu haisomi kitu ndio Mana Hawa Hawa ndio wanasigin vitu Bila kusoma

Hapa hata hajasoma alfu anakuja kumlaumu mleta mada as if mleta mada anamtetea Samia which is incorrect and inconvenience kbsa ,mleta mada ameleta hoja nzuri na makini na pia ameonesha wapi tumekozea na nn ilipazwa kufanyika haraka
 
Siku kama taifa tukiacha ukasuku tutakuwa katika hatua muhimu na hadhimu sana ya kuambiana ukweli kama ulivyo (objective truth) na sio ukweli kama unavyo jitokeza (relative Truth).

Uwazi ni kwamba Honorable causa ndio mhandisi mkuu wa suala hili la bandari wengine wanapakwa mafuta tu kwamba ndo wahusika jambo ambalo sio kweli
 


Usirudie siku mingine kuchosha watanganyika na hili andiko lako pelekea Steve’ake chongolo n.k

Cha ajabu wasomi ndo wanaupinga huu mkataba ila wanao utetea ni waliosoma ni mwijaku tu ndo kamaliza chuo wengine wote nanga tupu
 
Kwa kuongezea, na huyo profesa sijui haukosoma au yeye alitia tu sahihi bila kujua contents… ni maajabu ya Musa, au ni yale maneno aliyosema Lissu” professorial rubbish “ yatimie…? unaambiwa sign , unaanguka tu bila kujua implications za mbeleni. Hivi huyu Mbarawa alimshauri nini S100? Na Tuone sasa ushauri wake wa maandishi Kwa Raisi.
 

Mbarawa kawaaibisha wakufunzi wake bora sa100 ye kapewa udocta sio taaluma yake ila nae hivyo tu
 
Watekelezaji ndio walioweka saini ya rais kwenye IGA?
 
tatizo ni kubeza wataalamu , na kujikita kwenye chama , yaani Jambo la kitaalam unalipeleka kisiasa , unawashirikisha wale wa mlengo wako , kwann kwenye Mambo makubwa usiweke pembeni uchama !!?? kwani kulikuwa Kuna shida gani ukawaita wabobezi wa sheria wakaja kutoa ushauri wao , then wewe ndo uamua Sasa unawasikikiza au unawapuuza.
mambo ya kuamua mambo ya kitaifa kwa hisia za kichama ndo yanayoturudisha nyuma nchi hii.
 
Bora umgesoma tu alichokileta huyu bwana Ni kitu kikubwa mno

Hata akisoma hadi mwisho, shida iko pale mwanzo aliposema Rais alikuwa na nia nzuri na angeacha legacy kwenye uongozi wake, sasa iweje Jambo kama hilo akubali kuharibiwa na watu ambao ana mamlaka ya kuwawajibisha au kuwapiga chini wasimharibie?

Toka sakata la bandari limeibuka huyo rais aliwahi lini hata kutenga siku kulielezea au kuwaondoa hofu watanganyika zaidi ya kusema Kenya wenzetu nyenyenye na mchukue wenye maoni mazuri!

Lisu na Butiku walishauri ni bora sasa hivi lishughulikiwe hilo jambo kabla hajaja huyo DP kuliko aje na aanze shughuli, hajawasikiliza zaidi ya ccm kuenda kuelimisha ujinga na kubadili vifungu vya katiba ili viendane na mwekezaji

Hili swala kumtenganisha rais na huu mkataba ni ngumu sana!
 
Kwanza jifunze kuandika kwa ufupi. Pili mama ana mpango gani na Zanzibar, kwanini ameacha wasinufaike?
 

[emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…