Madikteta na wafalme huwa na sera nzuri sana za kiuchumi.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Madikteta au wafalme huwa wana akili moja inayowafanya wawe wazuri sana kwenye uchumi. Wao wakiona kitu fulani kinawaingizia pesa za kutosha, au sehemu fulani inaingiza pesa za kutosha basi akili na nguvu zao zote wanaelekeza huko. Mfano kama sehemu kunatoa dhahabu zinazowapa utajiri basi barabara, reli, na miundombinu mingine mingi itaelekea huko. Lengo si kuboresha hayo maeneo au kuyalipa fadhila kwa mali yanazotoa. Lengo ni kufanya yatoe mali nyingi zaidi kwa mtindo huo.

Ikitokea mali nyingi ipo kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda nk, basi madikteta hupeleka nguvu huko huko. Matokeo yake hujikuta bila kutarajia wamekuwa na sera nzuri za kiuchumi.

Kiongozi wa kidemokrasia yeye akili yake inaangalia wapi kuna kura au publicity nzuri. Atatumia mabilioni kujenga barabara za lami mitaa ya Dar au daraja la kukatiza baharini lakini barabara kwenda machimboni au kwenye mbuga za wanyama kunakomuingizia mabilioni ya pesa zikiwa na mashimo.

Nimewahi pita sehemu wanachimba dhahabu. Uchimbaji mkubwa unafanyika, wageni, wachina wanachimba sana lakini ukiangalia miundombinu ni hovyo. Hospitali, huduma za maji na barabara za huko hazishawishi mtu kuishi.
 
Mbona hakuna hizo sera nzuri kwa Museveni na Samia ?
 
Utafiti wa IMF wa mwaka 2023 uliochunguza mabadiliko ya uchumi na mifumo ya kisiasa katika nchi mbalimbali uliona kuwa ukuaji wa uchumi una uwezekano mkubwa wa kudumu chini ya demokrasia, huku mdororo mkubwa ukiwa na uwezekano wa kudumu zaidi chini ya utawala wa kiimla. Hii haimaanishi kila demokrasia ni bora kuliko kila udikteta, bali inapingana na dhana kwamba udikteta una faida ya jumla katika uchumi. 

Tatizo la hoja yako ni kudhani kwamba kwa sababu dikteta anaweza kufanya maamuzi haraka, basi maamuzi yake yatakuwa sahihi.
 
Madikteta au wafalme huwa wana akili moja inayowafanya wawe wazuri sana kwenye uchumi. Wao wakiona kitu fulani kinawaingizia pesa za kutosha, au sehemu fulani inaingiza pesa za kutosha basi akili na nguvu zao zote wanaelekeza huko. Mfano kama sehemu kunatoa dhahabu zinazowapa utajiri basi barabara, reli, na miundombinu mingine mingi itaelekea huko. Lengo si kuboresha hayo maeneo au kuyalipa fadhila kwa mali yanazotoa. Lengo ni kufanya yatoe mali nyingi zaidi kwa mtindo huo.

Ikitokea mali nyingi ipo kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda nk, basi madikteta hupeleka nguvu huko huko. Matokeo yake hujikuta bila kutarajia wamekuwa na sera nzuri za kiuchumi.

Kiongozi wa kidemokrasia yeye akili yake inaangalia wapi kuna kura au publicity nzuri. Atatumia mabilioni kujenga barabara za lami mitaa ya Dar au daraja la kukatiza baharini lakini barabara kwenda machimboni au kwenye mbuga za wanyama kunakomuingizia mabilioni ya pesa zikiwa na mashimo.

Nimewahi pita sehemu wanachimba dhahabu. Uchimbaji mkubwa unafanyika, wageni, wachina wanachimba sana lakini ukiangalia miundombinu ni hovyo. Hospitali, huduma za maji na barabara za huko hazishawishi mtu kuishi.
Mbona wengine ni waovu na Sera zao ovuuu?
 
Back
Top Bottom