elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
BAADA ya serikali kukazia msimamo wake wa kila mfanyabiashara wa madini, kufanya biashara ndani ya soko la madini, vinginevyo atachukuliwa hatua ikiwemo kutaifi shwa madini na kushitakiwa kwa uhujumu uchumi, katika muda wa siku 18 Soko la Madini mkoani Arusha limeuza madini mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.6.
Ofisa Mfawidhi Mkuu wa Madini Mkoa wa Arusha, Hamis Kamando alisema hayo alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake. Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na mauzo ya madini yenye uzito wa tani 48, kilo 459, gramu 760 na karati 14,549.42 yakiwa na thamani ya shilingi ya kiasi hicho cha fedha.
Kamando alisema katika mauzo hayo ya madini katika soko hilo, Serikali imepata mrahaba wa zaidi ya Sh milioni 188.6 na ada ya ukaguzi wa madini ya Sh milioni 5.5. Alisema kiasi cha Sh bilioni 5.6 kilichokusanywa katika mauzo ya madini ya siku 18 hadi Novemba 30, mwaka huu ni sawa na ongezeko la mara nne na nusu na mapato ya awali.
Ofisa Madini huyo alisema kabla ya Waziri wa Madini, Doto Biteko kuzungumza na wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha, Novemba 12, mwaka huu, soko hilo lilikuwa na wafanyabiashara 10 kati ya wafanyabiashara 107 mkoani Arusha ambao walipaswa kufanya biashara ndani ya solo hilo.
Alisema awali madini yenye uzito wa kilo 1,107, gramu 9,050.38 na karati 2,652.55 yenye thamani ya Sh bilioni 1.2 yaliuzwa na serikali ilipata mrahaba wa Sh milioni 45.6 na ada ya ukaguzi wa madini Sh milioni 12.7 ilikusanywa. Kamando aliwataka wafanyabiashara mkoani Arusha, kuuza madini ndani ya soko hilo na sio eneo lingine kwani serikali haitamvumilia mfanyabiashara mwenye kuvunja sheria na utaratibu wa kuuza madini nje ya soko hilo.
Alisema ofisi yake iko wazi muda wote wa kazi na itatatua changamoto zote za wafanyabiashara wa madini zilizo ndani ya uwezo wake kwa maslahi ya pande zote. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema mapato ya madini yanayopatikana katika soko hilo, yatafanya shughuli nyingi za maendeleo, hivyo aliwaasa wafanyabiashara wa madini kuhakikisha wanauza madini katika soko hilo kwa maslahi ya nchi.
Gambo alisema mfanyabiashara atakayekiuka utaratibu ikiwamo kuuza madini nje ya soko, ameiagiza Polisi kuchukua sheria stahiki kwani huo ni uhujumu uchumi wa nchi ambao haupaswi kuvumiliwa kamwe.
Alisema biashara ya madini inayofanyika mkoani Arusha ni kubwa, hivyo kila mmoja anapaswa kujivunia na kutaka biashara hiyo kunufaisha mkoa na serikali kwa ujumla wake na sio vinginevyo. P“Hili ni jiji la kimataifa linajulikana kwa biashara ya madini na utalii hivyo sote kwa umoja wetu tunapaswa kuichangia serikali kwa kufuata taratibu zilizowekwa katika kufanya biashara na sio vinginevyo,” alisema Gambo.