Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
 
Wakitoka hapo wanaandaa uchaguzi na kupita bila kupingwa, wasomi wetu maDR hamna kitu kichwani, halafu eti anahoji umuhi kwa Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya kwamba hazina umuhimu mwaka huu waa uchaguzi. Hivi ana akili huyu mnayemuita Msomi???
 
Acheni kutu pumbaza Tunataka kujua issiue ya Lugola. Ni lini mnamfikisha mahakamani? Maana hizi zuga ni za kuwafanya Watanzania wasahau ya Lugola and company.

Hivi CCM chama chenye miaka mingi kwenye siasa kuliko vyama vyote Africa mmefikia mahali pa kusherehekea kupokea wapinzani?

Mna tia aibu. Ni kwamba mmekosa kabsa mbinu mbadala wa kufanya siasa? Nawainea huruma. Maana sasa huku mna bebwa na dola, huku tume ya uchaguzi, kule kununua wapinzani hadi raha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom