Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Mkakati unafanywa kijanja sana, makonda alikuwa Mbeya kutekeleza hilo. Mkuu dunia haina siri
Kuna uwezekano kuna siri kubwa sana ambayo hawa wanao hama wanaoneshwa ukweli, mfano labda kuna usaliti mkubwa sana kwa nchi unaendelea nyuma ya pazia na jamaa wakioneshwa ushahidi usio kuwa na shaka wanaona afadhali waende CCM kuliko kuuza nchi.

Hizi ni hisia tu, huenda sipo sahihi.
Haiingii akilini kufikiria viongozi wengi namna hii wa upinzani hasa CDM wanaenda CCM kwa kuongwa pesa.
tena wanatoka kila kona ya nchi , hadi jimboni kwa Mwenyekiti wa CDM.
 
sasa pia watawanunua Wananchi wenye uchu wa mageuzi nchi nzima?Inaweza kuwa furaha ya muda tu kwao Ya Mungu mengi
 
Acheni kutu pumbaza Tunataka kujua issiue ya Kugola. Ni lini mnamfikisha mahakamani? Maana hizi zuga ni za kuwafanya Watanzania wasahau ya Kugola and company.

Hivi CCM chama chenye miaka mingi kwenye siasa kuliko vyama vyote Africa mmefikia mahali pa kusherehekea kupokea wapinzani?

Mna tia aibu. Ni kwamba mmekosa kabsa mbinu mbadala wa kufanya siasa? Nawainea huruma. Maana sasa huku mna bebwa na dola, huku tume ya uchaguzi, kule kununua wapinzani hadi raha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kugola Ni yule mkatika viuno? Amefanyaje tena?
 
Naona "Fidofido" wa kike anatumia nguvu za ajabu na kishenzi kupata jimbo la mbeya ili amtoe "kifimbo cheza" kitini kule mjengoni
 
Hii taarifa bado haijawa kamili.Hata hivyo kwa Mbeya wao sio wa Kwanza kutoka kuna baadhi walishatangulia.Lakin bado wasidhani watapita udiwani wakiwa ccm.Labda Nyadhifa zingine za kuteuliwa kama ukurugenzi n.k Lakin kwa madiwani wa ccm Mbeya huwezi kupita labda kwa mtutu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni upuuzi uliopitiliza kwa masomo kucheza mchezo wa kioga wakijinga wa kitoto yaani, UNAKATAZA WASIFANYE SIASA, WASIENDE KUONGEA NA WANACHAMA, WANANCHI KWA KUTUMIA DOLA HALAFU MWENYEWE UNAJIFANYIA SIASA NA VYOTE ,UNAONGEA UNALOPENDA BILA SHIDA HALAFU BAADAYE UNATANGAZA UMEWASHINDA, MUNGU AWALAANI NA KUWAANGAMIZA NYIE MLIOPEWA DHAMANA OVYO
 
Basi kama ni kweli madiwani wote hao 11 wanahama nivyema Mkiti F.Mbowe ajiulize au yawezekana huko CDM hakuna room for discussion. Mtaji wa wanasiasa sio kupuuzia wanaohama!!!!
 
I told you!
Kuna tatizo kubwa guys.

Wale wenye macho wanaona, wanye fikra za kuona mbali wanaona, wenye masikio wanasikia.
Wenye kukubali ushauri na ukosoaji wataanza kutuelewa tunaopiga kelele kuna tatizo sehemu ndani ya upinzani.

Siamini kama watu wote hawa wana nunuliwa.
Erythrocyte nilisikia Mbeya watu wenye msimamo hawanunuliki sasa hiki sijui ndio nini?!!!
'NASHINDWA KUSHANGAAA'.
Kuna unachokijua lakini unaficha , ongea yote halafu na mimi nitatoa mchango wangu
 
Back
Top Bottom