The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wananchi na madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wamekataa kuendelea na mkandarasi anayejenga Soko Kuu la Mwanga na Soko la Samaki katika Mwalo wa Katonga, wakidai ameshindwa kutekeleza mradi kwa wakati na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara waliokosa maeneo ya kufanyia biashara zao.
Mvutano huo umeibuka wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo uliofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo madiwani na wananchi walimkataa mkandarasi mshauri, wakisema ameshindwa kusimamia kazi ipasavyo.
Soma pia: Special Thread: Matukio ya Rafu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Soko la Mwanga lilivunjwa takribani miaka mitatu iliyopita kwa lengo la kulijenga upya kwa viwango vya kisasa, lakini mpaka sasa ujenzi wake unasuasua, hali iliyoongeza malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara.
Kutokana na hali hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Baraka Lupori, ametoa tamko rasmi la kutaka mkataba wa mkandarasi huyo usitishwe mara moja ili taratibu za kumpata mkandarasi mwingine zianze. Pia, ameishauri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ichunguzwe, akidai kuwa wakandarasi wanaopatikana kupitia ofisi hiyo mara nyingi wamekuwa wakisababisha ucheleweshaji wa miradi mkoani humo.