Madiwani Tanzania nzima hawazitaki mashine za kamari za kichina ila Serikali kuu chini ya Mwigulu inaziruhusu

Aisee ni janga la taifa hii kitu, CCM kazi yao ni kutumia linear equations za kuongeza umaskini, ufukara, ujinga, upumbavu, magonjwa ili waendelee kufanya yao
Alafu wanamwita rais wa wanyonge anaona sifa kumbe unyonge wenyewe umeletwa na unyanyaji na ufisadi wa serikali ya CCM.
 
Hii nchi nayo tunazidi kuwalaumu serikali ๐Ÿคฃ
Wew mtoto wako unamtuma kazi, anaenda cheza dubu, usimlaumu Mwigulu, jilaumu wew kwa kufeli malezi, tunahitaji kujenga kizazi chenye nidhamu, ambacho hata kikiona madubu mia kinajua kamari sio nzima,

Tujenge kizazi ambacho hata kione bia za bure kret 70 kijue bia nakunywa mwisho 2 nyingine naacha, ila sasa wazazi tunaacha watoto ovyo kisha tunalaumu serikali
 
Mwigulu lazima alaumiwe acha ufala. Kwa nini vifaa vingine ambavyo vinamadhara kwa taifa vinazuiwa kuingia nchini. Lakini madubu anayafagilia.
 
Ukizungumza haya watu wanakuonea huna akili , kwamba uwepo wake inakuhusu nini au unakuathiri wapi

Wanashindwa kujua watu wanafikiria jamii yote sio wewe tu , jamii iliathirika na wewe unaathirika


Mtaa ukiwa na vibaka na wezi lazima na wewe utaathirika na janga hilo ima kuibiwa au wanao kujiunga kuwa wadokozi na hatimae vibaka.

Mtu anafoka we inakuuma nini, wewe inakuathiri nini. Hizi mashine zinafanya watu wawe na ubongo ulio lemaa , uwezo unashuka , mtu hafikirii beyond ya hapo kupata kipato anaona ndio njia rahisi na ya haraka kupata hela
 
Sio kwamba kuna ushirikina?
Ni utaalamu tu wa zile taa zake na rangi rangi zile zikichanganyika na sauti tofauti tofauti zinazosikika katika kila unapoizungusha mashine ndio zinazokwenda kuuteka ubongo wa mchezaji na kumfanya anakuwa Teja wa hizo mashine !!
Hatari sana ! Duniani kote zilipo hizi mashine watu wanalia !!
 
Kabisa kabisa ๐Ÿ‘๐Ÿ’ฏ๐Ÿ™
 
Huna hoja
 
Hizo Mashine wewe binafsi zinakuathiri vipi na uwepo wake?
Wewe jaribu kufikiria tutakuwa na kizazi Cha aina gani huko mbeleni...!

Badala ya vijana kutumia akili zao kubuni njia bora za kuzalisha kipato wanajenga uraibu wa michezo ya kubahatisha!
 
๐ŸŽถ๐ŸŽถNi Kweli pesa sina nacheza michezo ya Bahati Nasibu๐ŸŽถ
๐ŸŽถNa mi nakomaa Aah aah Nizishike Pesa kama kina Nasibu๐ŸŽถ
MADUBU YA WACHINA ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
Yanamaliza vichenchi kila nikijaribu..
Hivi leo ntakula Kweli?
namuuza mwanangu Ibrahimu Ajibu...๐ŸŽถ๐ŸŽถ

KONTAWA ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ