Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 53
- 539
Nikiambiwa nim-rate huyu mkuu wa idara aliyeandaa hili dodoso kwa wafanyakaze wake basi nitampa 0/5. Huyu hata taratibu na sheria za utumishi wa umma hazijui na kama anazijua basi ameamua makusudi kuihujumu taasisi yake.
Kiwango cha ufanisi wa mfanyakazi hupimwa kwa OPRAS na sio kwa madodoso ya koridoni na ya kimbea kama haya. Madodoso ya kutajana hayajawahi kuiacha ofisi ama taasisi husika salama, sababu baada ya hapo aliyetajwa kuwa ndiye bora atavimba kichwa na aliyetajwa kama kihiyo atavunjika moyo na utendaji wake utashuka zaidi, na wengine waliobakia wataanza kufanya kazi kwa unafiki wa kumridhisha mkubwa bila kujali ubora wa kazi.
Kinachosikitisha zaidi dodoso kama hili kufanywa na taasisi kubwa kama Muhimbili National Hospital, ambayo ndio tunasema imebeba sura ya huduma za afya nchini, ndiyo role model wa sekta nzima ya afya na ndiyo kioo cha huduma za afya nje ya nchi yetu. Hivi wakija watu kutoka nje kuja kubadilishana ujuzi hapo hospitalini na wakakutana na madodoso ya kijima namna hii si wataona wamepotea njia na kurudi walipotoka?
Nashauri watu wa utumishi wawe wanafanya semina za mara kwa mara kwa watumishi wake maana hiki kinachofanyika inaonekana ni kutojua tarratibu za kiutumishi na kutokujua namna bora ya kuongoza watumishi.