'Madogo' wa miaka ya 2000 kila kitu wanajua wao

'Madogo' wa miaka ya 2000 kila kitu wanajua wao

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
WanaJamiiForums, habarini!

Vilio vya ugumu wa maisha vimezidi kushika kasi siku baada ya siku. Zaidi vilio hivi vinatoka kwenye kundi hili la hawa vijana wa 2000 kuja juu. Ukizingatia ndilo kundi ambalo limemaliza vyuo vikuu na kwa ukubwa lipo mtaani.

Wadogo zetu hawa siwasemi na wala siwalaumu. Naeleza mshangao nilionao kwenye tabia zao mbovu(kwa wengi niliowaona) zinazopelekea 'mabroo' wengi wavunjike moyo wa kuwashika mikono pindi wanapomaliza vyuo.

1. Kila kitu wao wanajua, huna cha kuwaambia.

Wadogo zetu hawa, wao wanajua YOTE na huna cha kuwaambia. Wanakuja kukuomba ushauri ilhali majibu tayari wanayo. Hawashauriki wala hawapangiwi. Jeuri, dharau, kiburi, na kupenda starehe hapa ndipo mahali pake.

2. Makundi ya kipuuzi na 'usela'.

Wadogo zetu hawa wanawalaumu bure tu 'mabroo'. Makundi ya kuvuta bangi na shisha ambayo yamejaa kwenye groups zao za WhatsApp ndiyo mchawi wao.

Kujiliza liza hovyo kwa visichana na kutojitambua kwa wakati. Halafu wakishauriwa wanakuwa wakali. Wao wanajua kila kitu.

'Shobo' za kijinga kwa waliofanikiwa, tamaa na kutoridhika, kutaka maisha ya bata na hawana hela. Haya yanakiharibu sana kizazi hiki cha 2000.

'Madogo' wakiendelea hivi, hasa hili la kutokubali kujishusha na kushaurika, walai vichwa vyao vitakatwa, maana tayari vimeshaelekea kibra.
 
Na ni kizazi ambacho hakichagui hakibagui....yeyote ni halali yao.
Na huviambii kitu...havijui maana ya mkubwa au kumweshimu mkubwa wote mko sawa.
Hakika wazazi wapo na kazi kubwa sana ya kuumia mioyo mpaka kaburini.
 
Kisa gugo ndo mana wanafeli....wangejua kilicholeta neno mbio za marathon wasingesumbua
 
Mtoa mada uloongea yote ni ya kweli 100%
 
Back
Top Bottom