'Madogo' wa miaka ya 2000 kila kitu wanajua wao

'Madogo' wa miaka ya 2000 kila kitu wanajua wao

Na ni kizazi ambacho hakichagui hakibagui....yeyote ni halali yao.
Na huviambii kitu...havijui maana ya mkubwa au kumweshimu mkubwa wote mko sawa.
Hakika wazazi wapo na kazi kubwa sana ya kuumia mioyo mpaka kaburini.
Wewe mwenyewe ulivyokua 20's ulikua hivyohivyo..!
 
Ninacho wapenda wanakonfidensi sana hata kama ni yakijinga. Lakini wakipigwa msasa vizuri watasaidia sana kuutoa utawala wa shetani sisiemu..
 
Ni wakati wao. Nakumbuka wakati nina miaka 20 mambo niliyokua nayafanya ni tofauti na sasa. Muda wao ukipita lazima watabadilika.
 
Wengi wao ulimbukeni tu..
Hakuna kitu wanajua zaidi ya ujinga uwezi kuta mtoto wa 2000 smart anafanya ujinga ujinga aiseeee....

Au ndgu yangu Vishu Mtata unasemaje maana wewe unapenda sana vitoto vya 2k
Videmu vya buku mbili ni maji mara moja kama maharage ya mbeya, kikubwa uwe na muda tu.
 
WanaJamiiForums, habarini!

Vilio vya ugumu wa maisha vimezidi kushika kasi siku baada ya siku. Zaidi vilio hivi vinatoka kwenye kundi hili la hawa vijana wa 2000 kuja juu. Ukizingatia ndilo kundi ambalo limemaliza vyuo vikuu na kwa ukubwa lipo mtaani.

Wadogo zetu hawa siwasemi na wala siwalaumu. Naeleza mshangao nilionao kwenye tabia zao mbovu(kwa wengi niliowaona) zinazopelekea 'mabroo' wengi wavunjike moyo wa kuwashika mikono pindi wanapomaliza vyuo.

1. Kila kitu wao wanajua, huna cha kuwaambia.

Wadogo zetu hawa, wao wanajua YOTE na huna cha kuwaambia. Wanakuja kukuomba ushauri ilhali majibu tayari wanayo. Hawashauriki wala hawapangiwi. Jeuri, dharau, kiburi, na kupenda starehe hapa ndipo mahali pake.

2. Makundi ya kipuuzi na 'usela'.

Wadogo zetu hawa wanawalaumu bure tu 'mabroo'. Makundi ya kuvuta bangi na shisha ambayo yamejaa kwenye groups zao za WhatsApp ndiyo mchawi wao.

Kujiliza liza hovyo kwa visichana na kutojitambua kwa wakati. Halafu wakishauriwa wanakuwa wakali. Wao wanajua kila kitu.

'Shobo' za kijinga kwa waliofanikiwa, tamaa na kutoridhika, kutaka maisha ya bata na hawana hela. Haya yanakiharibu sana kizazi hiki cha 2000.

'Madogo' wakiendelea hivi, hasa hili la kutokubali kujishusha na kushaurika, walai vichwa vyao vitakatwa, maana tayari vimeshaelekea kibra.
Mmmh kazi ipo
 
Back
Top Bottom