Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Bwana Pascal Mayalla ameandika:

"...., kitu cha ajabu ni kuna madudu fulani ya kiajabu ajabu sana ya kisheria, yamefanyika kwenye sheria zetu!, kwa kutungwa kwa sheria batili zinazokwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977!. Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatoa uamuzi kuwa hayo ni "madudu" ( neno madudu ni langu sio la mahakama), na madudu hayo yakachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!."

Tuseme huyu bwana hajui mahali sahihi pa kuyapeleka haya anayodhani kuwa ni mapungufu ili kupatikana ufumbuzi?

Au kama hao anaowatuhumu naye amekaa kimaslahi binafsi zaidi tu?

Kwa msingi huu bwana huyu anasema au hasemi nini kuhusu lolote fyongo ambalo liko kama lilivyo leo?

"Bwana Pascal Mayalla hausomeki. Kutokusomeka kwako kunafanya wajumbe kujiridhisha kwanza kwa kila PDF kuona kulikoni, hujakumbukwa tu?"
 
Wanasheria wenyewe ndio hao kama akina chenge ambao walituingiza ktk mikataba mibovu na utakatishaji fedha uliokubu kwa maslahi yao binafsi! watu kama hawa walikuwa wanatakiwa wasiwe tena ktk uso wa dunia!
Badala ya kujadili hoja wewe unafanya character assassination-YALEYALE
 
Bwana Pascal Mayalla ameandika:

"...., kitu cha ajabu ni kuna madudu fulani ya kiajabu ajabu sana ya kisheria, yamefanyika kwenye sheria zetu!, kwa kutungwa kwa sheria batili zinazokwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977!. Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatoa uamuzi kuwa hayo ni "madudu" ( neno madudu ni langu sio la mahakama), na madudu hayo yakachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!."

Tuseme huyu bwana hajui mahali sahihi pa kuyapeleka haya anayodhani kuwa ni mapungufu ili kupatikana ufumbuzi?

Au kama hao anaowatuhumu naye amekaa kimaslahi binafsi zaidi tu?

Kwa msingi huu bwana huyu anasema au hasemi nini kuhusu lolote fyongo ambalo liko kama lilivyo leo?

"Bwana Pascal Mayalla hausomeki. Kutokusomeka kwako kunafanya wajumbe kujiridhisha kwanza kwa kila PDF kuona kulikoni, hujakumbukwa tu?"
Bwana Paskal Mayala naye ni kati ya watu wanapaswa kujibu walikuwa wapi wakati haya yanafanyika
 
Niruhusu kuchangia yafuatayo
1. Tanzania haikukosea kuanza elimu ya chuo kikuu kwa kuanza na taaluma ya sheria kwani ndiyo taaluma iliyotolewa kwenye chuo kinachoaamika kuwa chuo kikuu cha kwanza -Bologna mwaka 1088.
2. Pamoja na taaluma ya sheria kuwa ya kwanza kufundishwa chuo kikuu lakini kwenye maisha ni taaluma ya mwisho kuhitajika
3. Kosa kubwa lililotokea ni wanasheria kujiweka kimbelembele kuweka utaratibu wa watu kuendesha maisha yao wakati uwezo huo hawana. Nitoe mfano wanasheria wanakuja mwisho baada ya Bwana A kukubali kumuuzia Bwana B gari, anachotakiwa kufanya mwanasheria ni kuweka katika maandishi A na B walivyokubaliana kuuziana gari. Iliyo sasa wanasheria wamejigeuza wao ndio wenye gari na kuwawekea maneno mdomoni mnunuzi na muuza gari tena katika lugha na maneno mengi ambayo ili A na B wayaelewe wanahitaji mtu mwingine kuwasaidia kuelewa.. Hakuna jambo linaanzishwa, kuwakilishwa na kuendeshwa na wanasheria linanyooka - ni kona kona. Kwa ujumla wanasheria ni wasanii wa kutupwa.
 
Katika vitu vinavyokushusha chini Pascal Mayalla !

Ni pamoja ba unafiki wako,kwa kumaanisha kwamba sio muwazi unaeweza kutoka na kusema unachokisimamia na kukiamini.

Machapisho yako yanakunyima nafasi,sababu kila upande huwa unashindwa kuelewa kama uko nao au la!

Mfano mdogo hapa!

Wewe ni mwanasheria na pia mwandishi nguli.
Umeshindwa nini kwenye Makala yako,kwenda direct kwenye kuzitaja hizo sheria zenye mapungufu na ambazo ni batili.

Umetumia muda mwingi na ukurasa mzima kurudia rudia jbo lile lile kwa sababu zako uzijuazo ninafsi.

Na hapo ndio panapofanya usiaminike......

Wewe na Zitto mnaelejea kuwa na unasaba fulani katika mtindo wenu kimaisha,kupitia taaluma zenu.
Mbona amekuwa zaidi ya wazi
1. Kasema hatuna wanasheria tuna watu waliosoma sheria na wanademka tu huku mitaani;
2. Kasema sheria mbovu sana zimeweza kutungwa na kutumiwa mbele ya macho yao.
3. Kaonyesha kwamba wanasheria wote hawajui namna ya kutotoa hapo walipotufikisha
 
Kwa Maslahi ya Taifa Nipashe ya Jumapili ya 15 January 2023 ni swali
"hivi kweli sisi Tanzania tuna wanasheria wa ukweli au tuna wasomi tuu wa sheria, waliosomea sheria na kuhitimu?. Kama ni kweli tuna wanasheria, jee wanasheria waliopo ni wapo kweli au ni wapo wapo tuu?!. Kama kweli Tanzania tuna wanasheria, wa ukweli na sio tuu wasomi wa sheria, na ni kweli wapo kiukweli, ilikuwaje kuwaje, madudu makubwa hivi ya ajabu ya kisheria, yakafanyika ndani ya nchi yetu kuanzia kwenye serikali yetu, kwenye Bunge letu na kwenye Mahakama yetu?, yaliwezaje kufanyika wakati tuna wanasheria wa ukweli?!, tena wengine ni manguli na wabobezi na wabobevu?!, huo unguli wao ubobezi na ubobevu ni kwenye nini?!
Hili ni swali nililoliuliza mwezi January 2023, bado liko valid mpaka leo kwa hiki kinachoendelea sasa kwenye vikao vya Bunge vinaendelea jijini Dodoma kupitishwa miswada 3 ya sheria, ikiwemo sheria mpya ya uchaguzi inayokwenda kupitishwa na madudu haya haya niliyoyazungumza hapa!.
Najiuliza mambo haya ya ajabu hivi yanaweza kufanyika vipi wakati tuna wanasheria manguli wabobezi na wabobevu wa sheria!, huo unguli, ubobezi na ubobevu wa sheria ni kwenye nini?.
P
 
Back
Top Bottom