Madudu mengine TFF na Bodi ya Ligi

Madudu mengine TFF na Bodi ya Ligi

Makendaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
271
Reaction score
141
Leo Bodi ya Ligi wametangaza Maendeleo ya Ligi kuu Tanzania VPL pamoja Na Kutoa Adhabu kwa Vilabu/Wachezaji waliokiuka Sheria na kanuni Za Mpira Hapa Tanzania.

Katika Kutoa Adhabu Hizo Nimezipitia Kwa makini na Kugundua Madudu yaliyo fanyika wakati wa Utoaji Adhabu Hizo na Kudhihirisha kuwa Adhabu hizo zilitolewa Na Watu ambao pengine wana Mahaba Na Timu Fulani....

Naomba mpitie hapa..

NB: Nimeifupisha na Kuchukua Yale ambayo nimekuja Kuya zungumzia Hapa.

Aidha klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi namba 134 dhidi ya timu ya Mbeya City, pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo huo.

Mchezo namba 117 uliozikutanisha Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu ya Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kukataa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Wakuu hapa pana kautata kidogo nimezi fuatilia hiz adhabu nikagundua kitu na nimeliona Hili...

Kanuni No 14(9) imetumika kuiadhibu timu ya Stand United kwa kosa la kutokuingia vyumba vya kubadilishia nguo na Faini wakapigwa 500,000 Na kanuni hiyohiyo imetumika Kuiadhibu Timu ya Simba kwenye mechi yao na Yanga Na kwa kosa Hilo La kutokuingia vyumba vya kubadilishia nguo lakini wao Wamepigwa Fain 300,000!

Hiz Faini zinapigwa kwa Upendeleo au wanaangalia Na Timu?

Nawasilisha.
 
Hii ndio Tz. Wanabadilisha kanuni katikati ya msimu wa ligi na timu moja inaanza kutumia kanuni mpya huku timu nyingine zote zikiwa hazina taarifa ya mabadiliko hayo.
Uongozi wa Malinzi umegawa nafasi za kamati kwa kulipa fadhila waliomsaidia kuingia madarakani na matokeo ndio haya sasa.
 
Uongozi wa Malinzi umekamatwa sana na mtu mmoja pale tff Geofrey Nyange Kaburu,
Yeye ndo kila kitu pale tifu tifu malinzi amebaki kama kivuli tu, anaelekea kokote kule anakotaka kaburu.......
 
Uongozi wa Malinzi umekamatwa sana na mtu mmoja pale tff Geofrey Nyange Kaburu,
Yeye ndo kila kitu pale tifu tifu malinzi amebaki kama kivuli tu, anaelekea kokote kule anakotaka kaburu.......

Huu mpira sijui unaelekea wapi kwa mtindo huu na wanafanya vituko Hadi wanajisahau kama kuna watu wanaona.
 
Hii ndio Tz. Wanabadilisha kanuni katikati ya msimu wa ligi na timu moja inaanza kutumia kanuni mpya huku timu nyingine zote zikiwa hazina taarifa ya mabadiliko hayo.
Uongozi wa Malinzi umegawa nafasi za kamati kwa kulipa fadhila waliomsaidia kuingia madarakani na matokeo ndio haya sasa.

Na kama kutumika ingetakiwa itumike msimu ujao
 
Back
Top Bottom