Hata chaguzi za caf na fifa zipo hivi hivi na hapa ndio utajua kwanini watu wanataka kuuana kwenye uraisi wa FA pote duniani, maraisi wa fa huwa wanakula rushwa ya mabilioni linapokuja swala la kupiga kura caf, fifa, uefa.
kwa wale wafuatiliaji wa michezo kiundani wanafahamu kwanini south Africa alikosa nafasi ya kuandaa world cup 2006, Russia haikuwa na sifa ya kuandaa world cup 2018 kutokana na ubaguzi wa kutisha lakini waliongoza kwa kura na kuwa host, Qatar na joto lote zaidi ya 40 degrees Celsius mwezi wa 6 ambapo ndio ratiba ya kuanza wc walipata Kura nyingi na kuwa host nation 2022 wakawa wanajiuliza imekuwaje, matokeo yake wamefoji wc kuchezwa December kwasababu huwezi kucheza kwa joto lile. Baada ya kura hizi zilifumuka kesi nyingi na kuonesha wapiga kura walivyoingiziwa mabilioni kwenye account zao
Athari mfumo huu ni kwamba hawa wajumbe wa mikoa, nchi huwa wanashindwa wamuunge mkono nani kwa kuogopa kutokupewa kipaumbele iwapo wasiyemchagua atashida. Rejea nchi za afrika zilimuunga mla rushwa mwezao blatter chaguzi zote, alipotoka walimuunga mkono hayatou, ulaya walimuunga infantino.. unategemea nini hapo