Madudu ya wahitimu vyuo vikuu.

bora huyo aliyekosea grammer kuliko wewe unayetoa mambo ya ofisi nje! hivi maadili ya kazi siku hizi mbona ni hovyo sana? hauna tofauti na yule anayetoa siri za ndani (unasema mambo ya mpz wako hadharani)
kweli wewe ulipewa nafasi kwa bahati mbaya

hahahaha kaka kweli umenkumbusha,moja ya ethics za mtumishi ni confidentiality...jamaa hana kabisa huyu.
 
siyo huyo tu,,,,sasa naanza kuamini product za mzumbe nazo feki,,,kuna mfanyakazi mwenzangu mmoja,asubuhi na mapema unamkuta kavaa sunglasses,anaenda ofisini,hamna hata jua.alafu mchana mida ya lunch namkuta amezivua...Mzumbe vijimambo 2pu

we unavyoonekana ni mbeya na n kilaza mkubwa hapo ofisin kwako.mbona unachunguza ya watu sana hebu fanya mambo ya maana tujenge nchi yetu bwana.
 
Huyu jamaa ni bonge la kilaza,alikuwa kula jukwaa la siasa akitokwa povu eti anachoma kadi ya chadema,anafoc umaarufu JF,so st*pid.#a¿§¥
 
Mzumbe ni chuo cha tarafa.Bado hujaona ya kile chuo cha kata DODOMA ambacho ukiingia getini tu unakutana na mnara wa CCM.Unategemea wahitimu wake watakua na tofauti na ccm??.Hili ni janga tunahitaji kulijadili kwa upana wake

tun mpango wa kubomoa ule mnara kujenga wa chadema.
 

"anyways its" gramatically uncorrect ndugu, kweli lugha yako ya tatu. Wale wale
 
Kwani kuna chuo kikuu gani kinachofundisha kuandika na kuongea Kiingereza?
Mwisho wa siku kama ulitoka na msingi mbovu toka shule ya msingi na sekondari, sidhani kama kuna chuo kitaweza kubadili uwezo wako.
 
Chezea kompyuta za ofisini wala si mafaili yake. Moja kwa moja hiyo ofisi wanajua wewe ndio ulietoa siri na kama wapo smart lazima upigwe chini.
 
Siwezi kushangaa ya mzumbe!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ingekuwa chuo kingine ningeshangaa hata mimi lakini kwa kuwa ni Mzumbe sina haja ya kushangaa labda mniambie maana ya Mzumbe isije ikawa ni mizimu ya jina inawafuata
 
kuna tatizo la lugha kwa watu wengi. sababu mojawapo ni uvivu wa kujisomea na kupenda kusoma vi summary kwa ajili ya mitihani tu.
 

angalia hapo laguage
 
HAMJAMBO WANAFUNZI!!!!! Hivi mpo semester ya ngapi? Vipi boom mmepata pia?
 

Usitetee maovu wewe. Kwani alipitapitaje hadi kufika hapo? Huko mavyuoni hamfundishwi Communication skills? Acha Hoja Zembe!!
 
Barua ya mhitimu Mzumbe University imeibua vicheko visivyo na mwisho kwenye idara ya utumishi hapa ofisini.

...........nawaibia kidogo tu!



"....... I has a bachelar in accounts and finance...."

Hiyo red tu ndo ninayoikubali kuwa ni kosa, ila 7bu kaeleweka yote sawa maana lugha si yake( ilitakiwa aandike ....I Have....). Hiyo blue ni kosa la kawaida sana, kapitiwa bahati mbaya sana, pia kaeleweka (ilitakiwa iwe ... bachelor...).

Tukiongea kiswahili tu tunachapia sembuse kuandika kingereza lugha ya kuja?
  • Wewe muanzisha thread akili yako ni finyu sana, najushauri jiongeze. Tofautisha kati ya mzumbe kama chuo na mtu kama zao la mzumbe.
  • Wewe mtoa mada hujui maana ya confidentiality when it comes to work ethics, nakushauri omba likizo ukajifunze
  • Wewe mtoa mada ndio usiyejua kuliko unayemtuhumu maana hata kurekebisha/kusahihisha umeshindwa, kwenda zako kapurwa wewe.....
 
Wakuu habari, maoni yangu:
1. Mleta uzi amenukuu kinachosemekana ni barua ya maombi ya kazi toka kwa 'mhitimu wa Mzumbe.' Hivi nani anaweza kuthibitisha kuwa hiyo ni barua ya huyo mhitimu na sio ya mhitimu wa chuo kingine au ya kutungwa na mleta uzi? Maana hapo hakuna ushahidi wowote unaothibitisha hicho alichosema mleta uzi.(Kwa kuwa mleta uzi ameamua kuvunja maadili ya kazi kwa kutoa siri za kazi angekuwa mkweli angetoa nakala ya hiyo barua watu waone)

2.Yawezekana mleta uzi ni mwanafunzi katika chuo anachokifahamu yeye mwenyewe akiwa na mawazo kuwa akikashfu wahitimu wa vyuo vingine yeye ataonekana bora.

3.Ikiwa mleta uzi ni mfanyakazi basi ni janga kwa mwajili na kwa taifa maana anachukulia kirahisi suala la uvunjifu wa maadili ya kazi hususani utoaji wa siri za ofisi nje.

4. Jamiiforums ni mahali pa mijadala yenye kulisha akili, kupanua uwezo wa kufikiri na kuleta hoja bora kwa maendeleo ya taifa letu. Mjadala kama huu hapa hautimizi malengo ya jamiiforums, pia hausaidii taaluma wala elimu hapa Tanzania. Nawiwa kusema ni uzi wa kitoto ulioletwa na mleta uzi mtoto aliye na nia ovu dhidi ya taifa letu na wahitimu wa vyuo vingine. Nasema hivi kwa kuwa mleta uzi angekuwa na nia njema angejadili kwa mapana tatizo la kiingereza kwa wahitimu mbalimbali, na hapo wachangiaji wangechangia maoni chanya bila kukashifiana.
 
Sasa kijana kaboronga sisi tunafurahia badala ya kuhuzunika! Kweli kizazi hiki kimelaaniwa. Hata asomee nini lugha anayotumia lazima aijue sawasawa. Haiwezi angeandika kwa Kiswahili. Kuandikiwa na mtu mwing sio sahihi yeye angeomba mtu amsahihishe alichoandika ndio apeleke!
 
Hata mimi nimeshangaa sana hicho kichwa cha somo. Sasa anamkosoa nini huyo mhitimu wa Mzumbe?
 
Mzumbe ni chuo cha tarafa.Bado hujaona ya kile chuo cha kata DODOMA ambacho ukiingia getini tu unakutana na mnara wa CCM.Unategemea wahitimu wake watakua na tofauti na ccm??.Hili ni janga tunahitaji kulijadili kwa upana wake

Hivi suala hapa ni Mzumbe University au ni huyo mhitimu? na hivi unadhani msingi wa mtu kujua lugha kama English ni kazi ya chuo kumfundisha au ni kutokana na msingi wa elimu yake tangu awali? Ukisema hivi nadhani hoja yako haina mashiko yoyote,suala la kiingereza ni tatizo la kitaifa na hii ni kutokana na msingi mbovu tokea awali.Usitegemee kujifunza English ukiwa chuoni ndugu yangu.Kama english yake ni mbovu ni kutokana na msingi wake kuwa mbovu.Analyze kabla hujazungumza!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…