Madudu ya wahitimu vyuo vikuu.

 

Ukichesha!!!!!!!!
 

Asante mchango wako ni mzuri.
 
Reactions: mka
Watanzania tunachekesha, tunategemea miujiza mpaka kwenye elimu? Huyo dogo aliyeandika barua hiyo hana kosa kabisa. Kosa ni mwalimu, na kama wanaopata div four za mwisho ndiyo wanaenda ualimu tutegemee nini? Wazee wetu zamani hata walioshia darasa la nne wako fit kishenzi, mnadhani siri ni nini? Zamani ualimu ilikuwa kazi ya maana ili uwe mwalimu ulitakiwa ufaulu vizuri. Tunatengeneza taifa la vilaza, miaka 50 ijayo ni disaster wandugu, oh!!!!!
 
bongo hamna chuo bwana kuna ssampuli ya vyuo bana
 
Barua ya mhitimu Mzumbe University imeibua vicheko visivyo na mwisho kwenye idara ya utumishi hapa ofisini.

...........nawaibia kidogo tu!





"....... I has a bachelar in accounts and finance...."

Yeye Kakosea english,
Wewe huna maadili,
Unatoa siri za Ofisi!
Hivyo ndivyo ulivyofundishwa, kuwa kila unaloliona unalitoa?
Kwa kuwa huna maadili toa na zile siri za madudu yenu mengine ya idara ya Utumishi hapo ofisini!

Hata Hivyo:

Tutaamini vipi kama ni kweli ni mwanafunzi wa Mzumbe, au pengine una agenda ya siri ya Kuharibu sifa ya wahitimu wa chuo hicho na chuo kwa ujumla!

Nasema hivi kwa sababu katika hali ya kawaida si kosa hilo tu linaweza kuwa limeonekana kwa Milioni ya applicants waliojitosa kinyang'anyiro hicho.
 
Barua ya mhitimu Mzumbe University imeibua vicheko visivyo na mwisho kwenye idara ya utumishi hapa ofisini.

...........nawaibia kidogo tu!


"....... I has a bachelar in accounts and finance...."

Lakini mbona tatizo la kutojua kuandika barua ya maombi ya kazi ni tatizo la wahitimu wengi tu wa vyuo tofauti hapa bongo! Na si tatizo la wahitimu wa mzumbe pekee!!! Binafsi nimebahatika kuwasaidia wahitimu wa vyuo tofauti na mzumbe kudraft barua za kuomba kazi.
 
kiingereza ni lugha tu kama kiswahili, kimatengo, kihehe, kizaramo na nyinginezo nyingi! sio lazima ujue kiingereza kuonyesha taaluma yako, kuna watu wana shule ndefu tu duniani na hawajui kiingereza mfano wachina, wajapani, waarabu, wafaransa, tembelea scandinavian countries, huko kote kuna maprofesa wa ukweli na hawajui kiingereza na wanagundua mavitu kibao na wanafanya mambo makubwa yanayotusaidia wote kitechnologia. so ni lugha, its not a big deal!
 
Si afadhali ya huyo kaandika toka kichwani kwake. Yupi mbaya kati ya anayecopy na kupesti na anayekosea?
 

Nawe pia laguage ndo nini au nayo ni 10th language kwako?
 
Tatizo si Mzumbe bali ni la sisteam maana hakuna mhadhiri wa chuo kikuu atakufundisha kutofautisha has na have, itakuwa sawa na kumwelekeza mama mwenye mtoto tayari jinsi ya kulala na mwanaume. Hilo ni kosa la wengi hata iwe mlimani, SUA, Udom na kwingineko ingeweza tokea au ipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…