Wakuu habari, maoni yangu:
1. Mleta uzi amenukuu kinachosemekana ni barua ya maombi ya kazi toka kwa 'mhitimu wa Mzumbe.' Hivi nani anaweza kuthibitisha kuwa hiyo ni barua ya huyo mhitimu na sio ya mhitimu wa chuo kingine au ya kutungwa na mleta uzi? Maana hapo hakuna ushahidi wowote unaothibitisha hicho alichosema mleta uzi.(Kwa kuwa mleta uzi ameamua kuvunja maadili ya kazi kwa kutoa siri za kazi angekuwa mkweli angetoa nakala ya hiyo barua watu waone)
2.Yawezekana mleta uzi ni mwanafunzi katika chuo anachokifahamu yeye mwenyewe akiwa na mawazo kuwa akikashfu wahitimu wa vyuo vingine yeye ataonekana bora.
3.Ikiwa mleta uzi ni mfanyakazi basi ni janga kwa mwajili na kwa taifa maana anachukulia kirahisi suala la uvunjifu wa maadili ya kazi hususani utoaji wa siri za ofisi nje.
4. Jamiiforums ni mahali pa mijadala yenye kulisha akili, kupanua uwezo wa kufikiri na kuleta hoja bora kwa maendeleo ya taifa letu. Mjadala kama huu hapa hautimizi malengo ya jamiiforums, pia hausaidii taaluma wala elimu hapa Tanzania. Nawiwa kusema ni uzi wa kitoto ulioletwa na mleta uzi mtoto aliye na nia ovu dhidi ya taifa letu na wahitimu wa vyuo vingine. Nasema hivi kwa kuwa mleta uzi angekuwa na nia njema angejadili kwa mapana tatizo la kiingereza kwa wahitimu mbalimbali, na hapo wachangiaji wangechangia maoni chanya bila kukashifiana.