Maduka ya Kifahari yafungwa Milan, Italia baada ya waandamanaji kuingia mtaani kuipinga Serikali

Maduka ya Kifahari yafungwa Milan, Italia baada ya waandamanaji kuingia mtaani kuipinga Serikali

uchumi wa Ulaya unategemea rasilimali za kupora Africa na uarabuni. Nje ya hapo tutarajie chumi zao kuyumba
Fanyeni kazi muache visingizio vya kijinga jinga. Watu mumekalia ufisadi kila kona kila mtu aliye kwenye kanafasi anataka tu aibe kisha mnasingizia Ulaya.

Kina Abdul kabla mama yake hajawa rais hakuna aliyekuwa anamjua lakini leo ni bilionea kivipi? Ni ufisadi mtupu.

Waafrika lazima tukubali tuna tatizo na tutabaki hivihivi mpaka mwisho wa dahari. Bure kabisa.
 
Maduka mengi katika mtaa wa kifahari wa nguo na bidhaa za bei mbaya wa Via Montenapoleone ambapo kuna chapa maarufu kama Chanel, Tiffany na Dior yaliondoa bidhaa zao kwenye madirisha ya maonyesho ili kuchukua tahadhari.

Maandamano hayo kupanda kwa gharama za maisha, huduma mbovu za jamii na kero zingine zinazofanana na hizo yaligeuka kuwa ya vurugu nchini Italia na Ubelgiji mnamo tarehe 17–18 Oktoba 2026, yakishabihiana na ghasia kubwa zilizotokea katika nchi jirani ya Ufaransa.

Waandamanaji kadhaa waliovaa kofia za kufunika sura (wengi wakiaminika kuwa ni watoto wadogo) walichoma moto mapipa ya taka na kupora maduka katikati mwa mji mwishoni mwa wiki. Hii ilitokea baada ya maandamano ya amani ya siku ya Jumamosi yaliyokuwa yakilalamikia huduma mbaya za jamii na gharama za maisha kupanda.

Miongoni mwa maduka yaliyovamiwa na kuporwa ni maduka ya vifaa vya michezo ya Decathlon na Arc’teryx, pamoja na duka la kampuni ya simu ya Vodafone, kama picha za TV zilivyovyoonyesha. Maduka ya nguo ya Levi’s, Under Armour na Decathlon yalifunika madirisha yao kwa mbao na maboksi.

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka ujao, alilaani ghasia hizo na kuongoza mkutano na mawaziri pamoja na wakuu wa usalama siku ya Jumatatu ili kujadili hali hiyo ambapo pia walizungumzia maandamano dhidi ya serikali na kupanda kwa gharama za maisha huko Milan na miji mingine mikubwa nchini Italia.

"Serikali itajibu kwa ukali mashambulizi haya dhidi ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuweka sheria za kuzuia vurugu zinazofanywa na watoto wadogo," aliandika Waziri wa Mambo ya Nje Antonio Tajani kwenye mtandao wa X (ambaye pia ni naibu waziri mkuu kama Salvini).

Kama sehemu ya mpango huo wa kukabiliana na vurugu, gazeti la Corriere della Sera lilisema Meloni anafikiria kuongeza muda wa kuwashikilia watoto wadogo kabla ya hukumu, na kupambana na makundi ya vijana wahuni, huku akiharakisha baadhi ya sheria za usalama ambazo kwa sasa zinajadiliwa bungeni.

Polisi wa Italia walisema walikuwa wamewakamata na kuwashikilia vijana 271 wakati wa vurugu za Milan siku ya Jumapili. Kati ya hao waliofikishwa kituo cha polisi, watu 32 walitiwa mbaroni kabisa (akiwemo watoto wadogo 23 na raia wa kigeni 13). Watu wengine 28 waliripotiwa kwenye vyombo vya sheria.

Vurugu hizo zilifuatia mapambano yaliyotokea siku ya Jumamosi katika miji mingine ya kaskazini mwa Italia kama Bologna, Brescia, Bergamo na Turin, ambapo waandamanaji 28 walikamatwa, kulingana na taarifa ya polisi ya siku ya Jumapili.

Vurugu hizi zilifanana na zilizotokea nchini Ufaransa, ambapo mamia kwa maelfu ya watu waliofanya maandamano kulalamikia gharama kubwa za maisha na huduma mbaya za jamii walimwagika mitaani siku ya Jumamosi, katika maandamano yaliyokuwa na vurugu kubwa zaidi kuwahi kuonekana nchini humo kwa miaka mingi.

View attachment 3694074
Wake wakodishe FFU au Polisi na Majeshi ya Afrika waone hap Gen Z watakavyochakzwa mpaka wachakae waache ujinga
 
Kwahiyo wewe kwako unatawala kidikteta? Kuwa mwanafamilia yeyote akichelewa kutekeleza jukumu alilopewa hapewi nafasi ya kuelezea kwanini?
Au maana ya Demokrasia ndiyo inakupiga chenga.
Ni bora ,kwani udikteta unataka nn zaidi ?
 
Fanyeni kazi muache visingizio vya kijinga jinga. Watu mumekalia ufisadi kila kona kila mtu aliye kwenye kanafasi anataka tu aibe kisha mnasingizia Ulaya.

Kina Abdul kabla mama yake hajawa rais hakuna aliyekuwa anamjua lakini leo ni bilionea kivipi? Ni ufisadi mtupu.

Waafrika lazima tukubali tuna tatizo na tutabaki hivihivi mpaka mwisho wa dahari. Bure kabisa.
Ni nature ya mtu mweusi kuwanyoshea wengine vidole kwa matatizo yake mwenyewe.
 
africa ambao tuna hizo rasilimali tupo wapi kiuchumi?
Kama isingekua kufadhili viongozi mafisadi tusingeendelea!? Burkinafaso ni mfano hai. Ufaransa alikua akifadhili uasi nchi isitulie yeye anabeba Uranium na madini mengine muhimu. DR Congo nako Belgium,Marekani na Israel wanafanya kama Ufaransa alivyofanya Burkinabe.
 
Sawa umetolea mifano burkinafaso na congo je nchi nyingine zilizobaki?
Nikurahishie tu shida ya africa ni viongozi wabinafsi na waroho wa madara na mafisadi.
 
Hizo ni porojo tu. Waafrika siku zote ni kupenda tu visingizio sasa je Tanzania mnasingizia nini? Ebu sema tukusikie basi.
 
Sawa umetolea mifano burkinafaso na congo je nchi nyingine zilizobaki?
Nikurahishie tu shida ya africa ni viongozi wabinafsi na waroho wa madara na mafisadi.
Hiyo ni shida moja wapo sio shida pekee. Pia hao viongozi walafi embu fuatilia nani anawapa kiburi na sapoti kama sio wao!?
 
Kwanini maandamano kama hayo hayatokei china ?
Hii ndiyo tofauti kati ya Demokrasia na Ujamaa uliochangamana na demokrasia kidogo sanaa.
 
Back
Top Bottom