Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

Familia yake majanga afanye mambo yake tu aachane nao.
 
Wacha awachane live ili wajulikane vizuri wapunguze kuzunguka kumtangazia ubaya mwenzao, ujue kuna mtu anakufanyia visa halafu yeye wa kwanza kutangaza wewe mbaya mtu ukimweleza sio kweli anayosema anaona kama mzaha mwishoe huyo uliyemweleza anashuhudia kwa kufanyiwa yeye na huyo mbaya anakuwa kashaumbuka kumbe kweli ndivyo alivyo
 
Mwanzo nilimshangaa dada mmoja alipokataa kuolewa na mtu mwenye nazo leo nimepata picha maana kila mtu anakutizama hata anayeamka kwenda kunywa mataputapu anataka umpe pesa, anayeshindwa shule ndio wa kwako umtafutie shule. Umasikini raha Afrika
 
Waafrika tumeshindwa....tumeshindikana
 
Naungana na familia yake, Ade ni mtelekezaji wa familia. Mngesikiliza upande wa pili wa mama yake na dada yake mpaka wanafikia hatua ya kupangisha hiyo nyumba kutokana na kukosa hela ya matumizi msingewalaumu.

Anadai alimfungulia biashara mama yake, lakini ujue biashara ni kitu cha asili, asiye na asili ya biashara hawezi, lazima afilisike, halafu mama yake ilitakiwa amtunze yeye mwenyewe, mbona akina Oliech wa Kenya wanatunza familia vizuri tu?

Huyo kaka dereva wa malori Ujerumani ndo amekuwa anatuma dola 5000 kila mwezi kulisha familia yao iliyoko Ghana.

Ade hana pa kutokea kwenye lawama hizi, kuna ushahidi kwamba kawatelekeza mno wakati pale Togo kuna vitoto vinacheza ligi ndogo za ufaransa na familia zao zimekuwa boosted kiuchumi kwa namna moja au nyingine.
 
hahaha! eti tumeshindwa...tumeshindikana Patrickn hii kiboko

Mkuu si unacheki mwenyewe mara tubaguane kule SA,mara tuue maalbino,mara tumalize tembo, mara tuuane kwa itikadi za kidini... mbaya zaidi watu tunaodhani ni wasomi ndio wanaturudisha nyuma, eti rais anajiuzia mgodi... tumefeli mkuu
 
Hicho kisa kisomeni vizuri na ku-reason kila paragraph mtagundua Emmanuel Adebayor ana matatizo makubwa ya kifamilia, na source ya matatizo hayo itakuwa ni yeye tu.

Ni maoni yangu tu.
 
bowlibo;

1.soma na kirudie ulichoandika boss
2.pitia changamoto za miaka yote ambazo ndugu wa Emma walikuwa wana angaika katika media
3.pitia media zilivyoripot juu ya saga hili hasa katika kipindi hiki cha miezi mitatu nyuma-asa media za Ghana
4.mwisho njoo katika only one post ya Emma juu ya saga lililodumu kwa kipindi kisichopungua miaka 12 to date
5.naamini utakuwa umejiridhisha,otherwise mhmhmh sina neno la ziada.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo Ujamaa umezidi hapa Afrika. Ndio maana bara ma nchi za Afrika haziendelei. Watu wako tayari kumsomesha mmoja na baadae wanampelekea mizigo yao yote kisa walimsomesha. Hii inarudisha maendeleo nyuma maana unakuta mtu mmoja anahudumia watu karibia 20 pamoja na familia zao
 

Mkuu ninavyojua ni hivyo nilivyoandika, labda najua kidogo sana katika hili saga, nitafuata maelekezo yako kuchimba zaidi.
 
Duh eti awajengee nyumba kila mtu na kuwalipa wage kila mtu kila mwezi??? This is too much
 
Mama yake mchawi, ndiye anasababisha hata maendeleo ya ade ya kisoka kuwa matatani. Halafu huyu mama kawajaza chuki ndugu zake ili wamchukie. Wachawi wanakera sana.
 
Eti awajengee nyumba na kuwalipa mishahara kila mwezi? au sijaelewa hapo?

Ilo mbona linawezekana... Mshahara Million 300/=Tsh. tena kwa wiki.

Atashindwa vipi kulipa mil 1 kwa ndugu 20 tu. Yaani tena kwa mwezi.
 
Mwanzo nilimshangaa dada mmoja alipokataa kuolewa na mtu mwenye nazo leo nimepata picha maana kila mtu anakutizama hata anayeamka kwenda kunywa mataputapu anataka umpe pesa, anayeshindwa shule ndio wa kwako umtafutie shule. Umasikini raha Afrika

mie najuta ila namshukuru Mungu kanipa akili na nguvu za kujitafutia mwenyewe.
 
He has a year left in a 100,000 pounds a week contract, He is very far away from being poor. He earns in a year what most will never earn in a lifetime even here in UK.
Vipi kuhusu matumizi bro
 
Mama yake mchawi, ndiye anasababisha hata maendeleo ya ade ya kisoka kuwa matatani. Halafu huyu mama kawajaza chuki ndugu zake ili wamchukie. Wachawi wanakera sana.

Familia nzima ni wachawi, hata Ade ni mchawi unajua chanzo cha ugomvi na kolo Toure pale Man City ni chuki za kichawi?
 
Pole zake Adebayor hii kwa Africa ni kawaida sana. kaka yangu kawasaidia ndugu zetu km sita hivi secondary na vyuo lkn leo wanamsemaje? yaani we acha tuu NDUGU LAWAMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…