Maelezo kuhusu kodi ya ardhi na jengo

Maelezo kuhusu kodi ya ardhi na jengo

Nimefurahi kufahamu....kwa sababu kuna mtu namfahamu anaplan ya kuuza nyumba kwa sababu ya taarifa za uongo kuhusu hii issue ya kodi
Huyo atakuwa ajajenga nyumba. Amerithi nyumba ushindwe kulipa Tshs15,000 au Tshs 45,000 kwa mwaka. Na akiuza anarudi katika Umasikini wa kufa mtuuu
 
Ndugu what if unaghorofa,hakuna ongezeko lolote la kodi (meaning ni nyumba ya kuishi lakini ni ghorofa)...naomba ufafanuzi
Bado ni nyumba ya makazi unless kama unaifanyia biashara kama zile za Masaki wanazolipa kwa dola' wanachoangalia mkuu kwa kuwa kinachoangaliwa ni matumizi ya jengo, yaani ni kiwango kidogo kama kuchangia serikali
 
Kodi ya nyumba uwa ni 0.15% ya thamani ya nyumba na ndio maana nyumba nyingi za zamani unakuta wanalipa Tshs15,000.
Wanachukulia thamani ya mwisho ya nyumba kwa apa mjini ni Tshs 10,000,000.
Mfano mzuri
Thamani ya nyumba ni
Tshs 10,000,000*0.15%= Tshs15,000.
hiyo uliyotoa ndio fomula ya kodi ya jengo ila kwa ubabe ama kwa kuwaona watu wajinga TRA na halmashauri za majiji wamekuwa wakijikadiria bila kufata taratibu zinazotakiwa
Mwaka 2013 halmashauri zote za jiji la Dar es salaam waliteua makampuni ili kufanya tathimini za nyumba kwa ajili ya ukadiriaji kodi lakini cha ajabu mwaka uliopita wamepandisha kodi kinyemela hapa nazungumzia kodi ya jengo.Kawaida nyumba ikijengwa thamani yake inapungua ila thamani ya ardhi inaongezeka lakini wao sijui wametumia vigezo gani kuongeza thamani za nyumba
 
Hapana haiwezi kuwa hivyo, haiwezi kuzidi 0.3% ya thamani ya jengo. Maeneo mengi inatozwa kati ya 0.005% hadi 0.1% ya thamani ya jengo.
Kodi ya jengo ni 0.1% ya thamani ya jengo.........
 
Back
Top Bottom