Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Mdada uber sio biashara ni parttime job ya kawaida, ni kama mtu unatoka kigamboni unaenda mlimani city kuliko uende long way bila faida unaweka uber on upate abiria u save hela ya mafuta, Lakini Tz ajira hazitoshi tunaona bora tutumie uber kama kazi goodluck mkuu in fact by uber u can make up to $200/mth hapa Tz lakini majuu madereva wa uber wanapata hadi $2000-3000/mth pia usisahau kutoa 20% yao
Ni 25% mkuu au wameshusha???
 
Habari !! nina wazo lakusaijili gari yangu iwe uber!! kwa wale wanaojua, je kazi hiii ina faida? changamoto zake ni zipi?
 
Kama unawazo la kufanya biashara ya uber pia ni vyema ukapitia hapa ujue changamoto na mukihitaji naweza ongelea upande wa pili Advantages ili uweze kujua kabla ya kuamua.

Unaambiwa utamu wa ngoma ingia uone!
Nimekuwa nikisumbuliwa na madereva wangu wa uber kwa kutofikisha hesabu 30,000/=kwa siku na mafuta ni yangu nimemwekea nusu tank siku ya kuanza.

Sikuchukua uamuzi mgumu ikabidi nimsimamishe mmoja ambaye kila siku aishi sababu bahati nzuri nikapata likizo nikaamua nijaribu kujifunza mazingira ya hii biashara kwa madereva. Nimeona yafuatayo

1, Uber calculator inacount pale tu unapofikia mteja so unapotoka kumfata haihesabu ili iingize kwenye nauli na unaweza ukawa upo kinondoni ukapata request ya magomeni sasa piga hesabu utoke kinondoni to magomeni bure alafu mpeleke mtu kutoka magomeni hospital to mwembechai kwa elfu tatu tu.

2, Uber calculator inasitisha kuhesabu malipo pale tu unapomfikisha mteja so kurudi gharam za mafuta ni juu yako na kuna maeneo ukimpeleka mtu hupati wa kurudi naye unaweza ukasubiri hata two hours

3, Foleni za dar; kuna foleni kiasi kwamba japo wanadai nauli is equal to time and lenth spent but tofauti ni ndogo san yani unaweza kutoka posta unaenda Tabata unatumia masaa mawili nauli ni only ten thousands.

4, Nauli wanazotoza; uber wanatoza less than 50% ya tax na wanachoangalia wao eti ni mda tu na umbali bila kukumbuka TRA tunalipa 318,000 kwa mwaka 70,000 Halmashauri, tunafanya service ndogo ndogo kama oil na kubwa kama kubadilisha tyre nk wao hawaoni hili.

5, Asilimia wanazochukua kwa sisi wamiliki wa hivyo vyombo is not fair wao wanakata 25% ya kila safari bila kujua hiyohiyo 75% tunanunua petrol, kufanya service,kulipa fine za barabarani na hapo hapo dereva apate posho yake.

6,Gari kuwa nyingi katika eneo moja kwa mfano utakuta kila dereva anang'ang'ania maeneo kama posta, upanga, masaki na osterbay hivyo kufanya trip kuwa za kubangaiza sana dereva anaweza kaa lisaa hajapata trip hivyo ni ngumu kufikisha hesabu.

7, Gharama za ziada yani unakuta kunagharama ambazo sio calculated kwenye biashara ila lazima dereva akumbane nazo kama kuwa na smartphone yenye uwezo sio kila smartphone inaweza, kuwa na internet bundles all the time na kuwa na charge wakati wowote kwani tangu nianze kutumia play store apps sijaona app inakula charge kama ya uber driver yani mpaka simu inapata moto but hizi gharama hawazioni wao wanang'ang'ana na 25%.


8, Usumbufu wa matatizo ya kimtandao yani siku kukiwa na tatizo la mawasiliano ya simu au internet huwez fanya biashara na kwetu Tz matatizo hayo ni kawaida sana.

Nimeamua yakuwa kama itafika january 2019 Uber watashindwa kutatua kero zetu wamiliki tulizozipeleka natoa gari zangu zote na kuziuza nifanye biashara nyingine na si mimi tu bali hili ni tamko la baadhi wamiliki tuliloliamua.
 
Uber na Taxify hazimfaidishi Dereva wala owner Wa gari , labda uniambie inampa Dereva uhakika Wa kula na sio kupeleka hesabu
 
Uber inawabidi waongeze bei kwakweli. Hata ukiwa abiria sometime unaona aibu na kutoa tip. Haya yakiendelea uber itakufa nchini na hasara itakuwa kwetu sote.

Nadhani tatizo kubwa ni kuwa wameuhamishia mfumo wa marekanj hapa. Kule, madereva wanatumia magari yao binafsi hivyo concept ya hesabu haipo. Kwahiyo bei kuwa ndogo na 25% hazina madhara sana

Kuna rep wao humu, waliangalie hili. dricks
 
Uber inawabidi waongeze bei kwakweli. Hata ukiwa abiria sometime unaona aibu na kutoa tip. Haya yakiendelea uber itakufa nchini na hasara itakuwa kwetu sote.

Nadhani tatizo kubwa ni kuwa wameuhamishia mfumo wa marekanj hapa. Kule, madereva wanatumia magari yao binafsi hivyo concept ya hesabu haipo. Kwahiyo bei kuwa ndogo na 25% hazina madhara sana

Kuna rep wao humu, waliangalie hili. dricks
Umeona mkuu
 
Unatumia gari aina gani mheshimiwa?
Kama ni I.S.T tuwasiliane ukihitaji kuziuza.
 
Inabidi waende na uhalisia. Kumplease mteja tu haitoshi. Dereva nae anatakiwa aridhike. Waelewe kuwa hapa nchini watu wanafanya hii kazi kama njia yao kuu ya kuingiza kipato na sio side gig kama business model yao inavyodhani.
Umeongea point mkuu
 
Unajua sisi watu wa mikoani hizi kelele za UBER tumeanza kuzisikia muda sana kwanza since ziko huko ughaibuni mpaka sasa bongo niwe muwazi kongole kwa mtoa mada katika pita pita zangu za kufuatilia nini uber wanafanya, changamoto na mafanikio tangu kipindi kile mnataka kugoma this is the best thread I have read compared to all of them! Mleta uzi umechanganua vizuri sana kiasi ambacho mtu yeyote anaetaka kuingia kwenye biashara hii anapata elimu ya kutosha nini ni nini? Na nini si nini?
 
Hiyo biashara imeshakuwa kichaa sasa...simshauri mtu anunue gari aingize huko ataishia kulia kila cku...mm nlitamani sn hii biashara mwaka huu mwanzoni nikamuuliza jamaa yangu mmoja ambae alikuwa anafanya akaniambia hali ngumu sn gari zimekuwa nyingi halaf nauli kiduchu mara hao uber wanatoa tu discount kwa wateja bila kushauriana na watoa huduma.

Poleni sana ndugu zangu
 
uber ilikuwa mwanzoni kipindi ndio imeingia tz... watu walipiga pesa nyingiiii sana

ila sasa tangu taxfy aje uber kaharibiwa soko then magari yaliyojisajiri uber yakawa mengiiii

siku hizi ni hasara tu
 
Ila nadhani kwa sababu ya kuwa ni biashara huria kwani si unajitoa kwenye hiyo Uber ukiona biashara hailipi.nadhani kuliko kuanza kulialia hapa ni bora kifanya maumuzi ya haraka.unavyozidi kuchelewa gari zako zinazidi kushuka thamani.baadaye utauza kwa bei ya hasara.si unajua magari kama hayo madogo yanauzwa kwa namba yaan A,B,C,au D.
 
Unajua sisi watu wa mikoani hizi kelele za UBER tumeanza kuzisikia muda sana kwanza since ziko huko ughaibuni mpaka sasa bongo niwe muwazi kongole kwa mtoa mada katika pita pita zangu za kufuatilia nini uber wanafanya, changamoto na mafanikio tangu kipindi kile mnataka kugoma this is the best thread I have read compared to all of them! Mleta uzi umechanganua vizuri sana kiasi ambacho mtu yeyote anaetaka kuingia kwenye biashara hii anapata elimu ya kutosha nini ni nini? Na nini si nini?
Thanks kwa kuelewa
 
Back
Top Bottom