Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Jamani nisaidieni jinsi ya kujiunga, navyojua mimi uber ni gari za watu binafsi sasa kwenye kurejista wananidai car sticker ni ipi hyo? pili wanataka commercial vehicle registration wakati ni gari binafsi je yanipasa kwenda kuchukua upya card ya gari ile ya biashara na plate no nyeupe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani nisaidieni jinsi ya kujiunga, navyojua mimi uber ni gari za watu binafsi sasa kwenye kurejista wananidai car sticker ni ipi hyo? pili wanataka commercial vehicle registration wakati ni gari binafsi je yanipasa kwenda kuchukua upya card ya gari ile ya biashara na plate no nyeupe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya mafunzo elekezi yanayotolewa office za uber viva tower posta uhuru streat kuna program wanaita kuunganishwa ambayo ili uunganishwe ni lazima uwe na card ya gari iliyosajiliwa kibiashara pili lazima uambatanishe na licence yako ya udereva wa gari ndogo za abiria C1 na mwisho badala ya sticker za Halmashauri zinazotumiwa na tax za kawaida uber zao wanakupa wenyewe mtakatana mbele kwa mbele.
Mwisho kwakuwa gari inakuwa imesajiliwa kibiashara ni lazima ulipe kodi seriikalini hivyo unapaswa uende TRA na kiwango ni 318, 000 ambacho unaweza kukilipa kwa awamu nne ndani ya mwaka mmoja .
Hakuna biashara halali isiyo na usajili wa kibiashara usisikilize ya watu mitaani sikiliza wanayokuambia au ninayoongea mimi na ndio mana nimesema biashara ya uber ina changamoto nyingi mno bila shaka umeanza kuziona mkuu
 
Hili swali najua ni common: Uber inalipa hailipi?

Jibu lake: Inalipa kidogo sana.

Kwa nini?

Moja, Inategemea, kama unatumia gari lako mwenyewe ama unatumia la mtu mwishowe upeleke hesabu. Kama gari lako utapata kidogo, kama unapeleka hesabu njaa ni kali sana asikwambie mtu

Mbili, Unatumia mafuta ama unatumia gesi. Kama unatumia mafuta hakuna rangi utaacha kuona, kama unatumia gesi utaona hela.
 
Abiria wengi wa Uber wanajua magari ni ya Uber, kwamba madereva wameajiriwa na Uber na wakapewa magari. So wanafanya kazi ya Uber.

Ukweli: Uber hawana magari wala madereva. Yale magari ni ya watu binafsi sio ya Uber na wale madereva wapo kimpango wao sio waajiriwa wa Uber. Anaweza kukushusha muda wowote akitaka bila kuulizwa chochote maadam ameona inafaa akushushe (mfano unamkera au unamtishia usalama wake).
 
Unashauri aina gani za magari zinafaa kutumika? Na kwanini?
Gari zenye injini ndogo isiyozidi cc 1300, na iwe safi yaani mtu awe comfortable akipanda na dereva akiendesha.

Kwa nini? Kwa sababu nauli za Uber ni ndogo sana, bodaboda ni ghali zaidi ya Uber. Ukiwa na injini kubwa lazima utanilia sana.

Pia, abiria wengi wa Uber kama 95% ni wanawake hivyo lazima gari iwe safi kama wanawake walivyo wasafi na warembo
 
Dereva na Uber wanagawana asilimia ngapi kwa safari?
Wanagawana na nani? Na uber ama na nani? Kama ni Uber wao Uber wanakata 25% ya kile anacholipwa dereva, lakini kuna kitu kinaitwa 'boost' ama 'surge' hizi husaidia kujaza gap la kukatwa 25% hivyo mwisho wa wiki dereva huwekewa pesa benki na Uber na kujikuta kama hajakatwa chochote badala yake Uber wamemuongezea hela na abiria amelipiwa na Uber kitu kama hicho
 
Wanagawana na nani? Na uber ama na nani? Kama ni Uber wao Uber wanakata 25% ya kile anacholipwa dereva, lakini kuna kitu kinaitwa 'boost' ama 'surge' hizi husaidia kujaza gap la kukatwa 25% hivyo mwisho wa wiki dereva huwekea pesa benki na Uber na kujikuta kama hajakatwa chochote badala yake Uber wamemuongezea hela na abiria amelipiwa na Uber kitu kama hicho
Kama mnajazwa mwisho wa wiki inamaana kumbe njaa ya muda tu!?..
 
Vipi kuhusu usalama wa dereva anaye endesha uber?hawezi kuitwa na majambazi wkamteka au kuchukua gari
 
Vipi kuhusu usalama wa dereva anaye endesha uber?hawezi kuitwa na majambazi wkamteka au kuchukua gari
Very possible. Lkn dereva ana mamlaka yote ya kukataa safari hata kama kaipokea hapo mwanzo, akiona mazingira sio rafiki anagoma kwenda. Jukumu la usalama wa gari na dereva ni la dereva mwenyewe.

Pia, abiria anajisajili kwa namba yeyote anayoona yeye na kwa jina lolote analoona yeye na Uber hawahangaiki naye, hvyo hana details concrete za kumfuatilia sana, Lkn details za dereva ni nyingi sana
 
Hivi nikiwa abiria namlipa dereva kutokana na umbali (km) au masaa tutayotembea barabani.?
 
Vipi kuhusu tabia ya baadhi ya madereva kuchezea GPS na kuongeza gharama ya safari ? Mfano unaweza kutembea umbali wa 4 km lakini mwisho wa safari itaonekana 12km

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom