Maelezo ya Polisi kuhusu Panya Road hayaeleweki. Kwanini wanaua na siyo kukamata? Je, ni yale yale ya akina Zombe yanajirudia?

Narudia Tena humu Kuna comments za panya roads na wazazi wanaonufaika na huu uporaji. Watawatetea tuu.
Inatia mashaka kuamini kama Hawa wanaouliwa ni panya lodi au wavuta madawa ni ngumu kuwatofautisha tusije tukachekelea kuwa mambo sasa shwari baada ya muda matukio yakaendelea polisi wafanye kazi kwa weledi
 
Hii inaitwa impunity

Hawa ndio polisi wetu!.

Naunga mkono hoja

True

Ila pia hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa polisi wauaji hawa!. Karma haitawaacha salama, ubaya wa karma inawatandika kuanzia aliyewatuma hadi anayepaswa kuchukua hatua lakini hakuchukua!.

Mfano zile pyu pyu za Lissu, si zimepangwa na kutekelezwa na watu wasiojulikana, lakini karma yake ni usipime!. Tumewashuhudia...
naomba nisimalizie...
P
Some braza nakuelewa sana
 
Ni mara nyingi sana inatokea kuona polisi wetu wakisimama kwenye podium kuzungumza na waandishi wa habari, wanachozungumza mara nyingi ni "watuhumiwa walipigwa risasi na wakafa wakikimbizwa hospitali" Wakati huo huo hakuna ushahidi wa polisi kushambuliana na hao wanaowaita wahalifu, wananchi hawaoni na kuhakikisha kuwa kulikuwa na milio ya risasi.

Miaka ya nyuma, Zombe na wenzake walileta hadithi inayofanana na haya yanayoendelea....Kirahisi rahisi wafanyabiashara wakauawa, huku wakisingiziwa ni majambazi, hadi tume ilivyoundwa ikathibitisha kuwa wale ni wafanyabiashara waliopelekwa Mabwe pande na kuuliwa huko.

Sasa haya leo yameshamiri, polisi wanatatua matatizo yao kwa kuua, kwa nini wasiwashike? Kweli kuna asiye na akili akataka kupigana na panga na polisi walio na silaha kali? Katika kipindi cha wiki 3, watu/wananchi 19 wameshapoteza maisha mikononi mwa polisi. Maelezo yao polisi wetu hayaeleweki. Yaani ya kuunga unga tu!

Nani leo hii atawaamini polisi wanaoua watu wasio na makosa? Kwanini wasiwakamate washukiwa wa ujambazi ili waweze kuwataja wauaji wengine? Na mbona hawaonyeshi sehemu kulipokuwepo hayo mapambano? Wanaonyesha mapanga yenye damu (Polisi wanajua ukweli kuwa wanadanganya)

Polisi wetu hamna credibility, mnaua, mnatesa na kuumiza wananchi wasio na hatia. Hakuna anayewaamini kwa matendo yenu.
-%20KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Zombe alikwapua hawa wa sasa hivi hawakwapui , hiyo ni moja ya tofauti , pili wazombe hawakuwa watuhumiwa wa uhalifu au kukutwa kwenye kutenda uhalifu , hawa panya wanakutwa sehemu
 
Sijui Serikali inatoa ujumbe gani kwa watani zangu vijana wa Kisukuma wanaoua wazee wao kwa kuwakuta tu macho mekundu.
Au kwa sababu gongo haramu lakini konyagi ni halali kwa kuwa inabandikwa ETS.
Basi na gongo iruhusiwe kubandikwa Electronic Tax Stamps ili nayo iwe halali.
 
Back
Top Bottom