Maelfu ya Wananchi Wamiminika Katika Mapokezi Mazito ya Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi na CPA Amos Makala Mkoani Simiyu

Maelfu ya Wananchi Wamiminika Katika Mapokezi Mazito ya Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi na CPA Amos Makala Mkoani Simiyu

Na walivyo maskini, mmewachota Kwa Hadi ya nyama na ubwabwa mkutanoni. Napajua Simiyu kuliko neno lenyewe Simiyu
 
Na walivyo maskini, mmewachota Kwa ahadi ya nyama na ubwabwa mkutanoni. Napajua Simiyu kuliko neno lenyewe Simiyu
 
Naona unaumia sana na kuteseka sana moyoni mwako unapoona mafuriko ya watu wakiminika katika mikutano ya CCM
Mafuriko ya CCM au wananchi mkuu!?? Hapo naona watu wamevaa CCM pamoja na wanafunzi waliolazimishwa kwenda kumpokea kiongozi wa CCM
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika CCM ni Baba lao, ni tumaini la watanzania,ni nuru ya wanyonge,ni nyota ya matumaini.Hiki chama ndio kimebeba matumaini ya mamilioni ya watanzania.ndio kimeshikilia furaha ya mioyo ya mamilioni ya watanzania.ndio chama kiletacho tabasamu katika nyuso za watu hata kama ni wagonjwa .

Mapokezi Makubwa yaliyoshuhudia maelfu ya watu wakiminika na kufurika mkoani Simiyu kuwalaki Wajumbe wa Secretarieti wakiongozwa na Katibu Mkuu wetu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi, Mheshimiwa CPA Amos Gabriel Makalla pamoja na Dada yetu Rabia ni mapokezi ya kihistoria.ni mapokezi yenye kuonyesha imani kubwa waliyonayo mamilioni ya watanzania kwa CCM.

Ni mapokezi ambayo unaweza kufikiria labda watu wameisha mitaani kwote mpaka makanisani.ni mapokezi ambayo unaweza kufikiria labda ni mafuriko ya watu wakitoka kuangalia Mpira wa dabi inayowakutanisha Watani wa Jadi Simba na yanga. Ni mafuriko ambayo unaweza kufikiria labda watu wanavutwa kwa sumaku kutoka kila Sehemu waliko.

Kwa hakika CCM haina mbadala wake katika Taifa hili.haina mshindani wala wa kuipa upinzani iwe ni jukwaani au katika sanduku la kura .ni CCM pekee iliyo katika mioyo ya mamilioni ya watanzania.huu ni zaidi ya upendo kwa CCM.haya ni Mahaba ya hali ya juu sana inayoyapata CCM kutoka kwa watanzania.

Halafu utashangaa CHADEMA na kuchanganyikiwa kwao waanza kushangaa pale CCM itakapo zoa na kukomba viti vyote uchaguzi wa serikali za mitaa ,pamoja na kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 90 uchaguzi mkuu hapo mwakani. CCM ni mpango wa Mungu Mwenyewe. Sasa miamba na majabali haya ya siasa za kisayansi yameingia mkoani Simiyu kuvurumisha mikutano mizito huku yakiteketeza vichaka vyote vya wapinzani.

Siasa ni sayansi.siasa ni watu na watu ni imani, na imani huja kwa kugusa maisha ya watu. CCM imegusa maisha ya mamilioni ya watu na ndio maana inaaminika na kupata watu katika mikutano yake.sasa CHADEMA wasio aminika kwa watu waliitisha maandamano matokeo yake wakajikuta wanamuandamanisha Mbowe ,mwanae na mke wake ambaye haikueleweka kama anakwenda ni kazini au anataka kuandamana.

View attachment 3116783

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nikionaga picha kama hizi ndiyo huwa najiuliza hivi hii nchi ina wagonjwa wa akili kiasi gani? Je kwa nini Mungu aliwanyima akili waTanzania?
Wakitoka hapo 9 katika 10 ya hao hawajui kesho wataishije. Lakini kesho wapo na watesaji (sadists) wao, Tundu Lisu anawapa nadharia ya demokrasia lakini hawaelewi!

Vanity! Huwezi kumwokoa asiyejijua. It is striving after wind.

…..,,,,,,, niepushi nisinywe kikombe hiki cha sumu ya CCM
 
Wivu utakuuwa mwaka huu.
 
Mafuriko ya CCM au wananchi mkuu!?? Hapo naona watu wamevaa CCM pamoja na wanafunzi waliolazimishwa kwenda kumpokea kiongozi wa CCM
Kama unaweza kuwalazimisha mamillioni ya watu kuhudhuria.basi nenda na wewe ukaandae mkutano mkubwa wa aina hiyo.
 
Ni ukweli usiopiopingika,wewe uko kwenu huko ya huku huyajui ila huyu mtu hatumpendi,bisha utakavyo lakini huku ataangukia pua labda mchakachue kama kawaida yenu.
 
Ni ukweli usiopiopingika,wewe uko kwenu huko ya huku huyajui ila huyu mtu hatumpendi,bisha utakavyo lakini huku ataangukia pua labda mchakachue kama kawaida yenu.
Screenshot_20240928-224331_1.jpg

Back
Top Bottom