MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Ifahamike Ukraine na Urusi ni watu wamoja, na lugha inayotumika sana Ukraine ni Kirusi, maelfu ya Warusi hawaungi mkono huu uvamizi dhidi ya ndugu zao, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii wengi wanatukana sana maana hawaelewi nini sababu za mauaji yanayoendelea au tija yake kwa Urusi, pia kuna taarifa baadhi ya wanajeshi wa Urusi wamenza kujisalimisha Ukraine na kugoma kuendelea kuua ndugu zao bila kuelewa nini sababu kuu.
Putin kwenye hili kachemsha, ingekua vita dhidi ya watu wa tabaka tofauti, Warusi wengi wangemuelewa, lakini hapa ni mauaji kwa ndugu zao kabisa wanaochangia vinasaba, na hakutumia muda wake vizuri kuwaelewesha ulazima au umuhimu wa mauaji haya, kakurupuka tu na kutuma majeshi yaanze uvamizi.
Huu uvamizi umesababisha Warusi wengi walio ugenini waishi kwa aibu ya kutojitambulisha popote utaifa wao.
https://www.news10.com/news/ukraini...sian-platoon-surrendered-to-ukrainian-forces/