MAENDELEO BILA UMOJA NI UMASKINI
Tanzania kama taifa tuliongoza harakati nyingi sana za kiukombozi hasa katika nchi nyingi zilizoko kusini mwa frika. Umaarufu wetu ulitokana na umoja wetu katika kuhakikisha kwamba, wale wote tuliowatangulia kupata uhuru nao wanakuwa huru angarau hata kwa uhuru wa bendera. Kama wasemavyo waswahili, kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Baada ya kupata uhuru mwaka 1961 kazi iliyokuwa imebaki ni kuijenga nchi.Ujenzi huu si wa siku moja na hautakuwa na kikomo kwasababu matatizo yapo siku zote na hayatakoma.
Huko nyuma baada ya uhuru tulionekana kama tuwamoja kuliko tulivyo sasa, kosa kubwa ambalo tutalifanya ni kutokukubali kwamba sasa umoja wetu kama taifa umetikisika.Tukiendelea kudhani na kukubali kwamba tu wamoja wakati kuna kila dalili za kuonyesha kwamba tumeparaganyika tutakuwa tunajaribu kutatua tatizo kwa dawa isiyokuwa tiba. Tumekuwa na mivutano pamoja na mabishano sana nchini, si jambo baya kuvutana ama kubishana, maana inaonyesha uhai wa watu katika kufikiri kwa kupatia ama kwa kukosea.
Lakini mabishano yenye maana yanategemewa kuwa na mwisho mzuri wenye kutufanya tuwe wamoja zaidi kuliko kutugawanya. Maendeleo hayatawezekana kama umoja wetu utakuwa na mashaka.Tunaweza kuwa kwenye safari moja lakini kila mmoja akiwa na malengo yake litakuwa jambo gumu sana kufikia mwisho wa safari yenyewe ambao kwanza ndo imeanza.
Tumekuwa ni taifa la majibizano badala ya mazungumzo, hakuna wa kumlaumu, hakuna atakaye twambia tunakosea bali utashi wetu unaweza kupima matendo yetu na kugundua kwamba tunaendelea kukosea. Tunapokuwa na lugha gongana katika taifa tunakuwa kama wajenzi wa mnara wa baberi, ambao walishindwa kuendelea na ujenzi baada ya kutoelewana lugha. Kama tunahitaji kujiletea maendeleo ya kweli, kwanza tuna jukumu kama taifa kuhakikisha tunarekebisha tofauti zetu. Jambo hili litawezekana tu ikiwa tutajiona tuna haki sawa ya kushiriki kuijenga nchi hii na kwamba hakuna kundi linalodhani kazi yake ni kuliletea kundi lingine maendeleo, hayo yalifanywa na wakoloni.
Tumekuwa na utamaduni wa kupendana, kusaidiana, kuoleana, kuheshimiana kama ndugu toka zamani, sifa hii ndiyo iliyotutofautisha sisi na wao. Lakini naanza kuona kama tunazidisha juhudi za kufanana na wale tuliokuwa washauri wao kwa vyovyote vile watapenda tufanane na nyakati zao, ili tusiwe na usemi tena mbele yao tuna kila sababu ya kukataa kwa vitendo siyo maneno tu. Njia pekee itakayofanya tuweze kuwa wamoja ni majadiliano na hili si katika eneo la siasa tu ambalo linaonekana kwa urahisi kama tatizo mojawapo lenye kutufanya tusiwe wamoja, bali hata katika mambo mengine ambayo yanaleta mawazo mchanganyiko. Kuna wakati tunaweza kuwalaumu wale tunao tofautiana nao mawazo bila kufahamu kwamba inawezekana tatizo liko kwetu.
Tunaweza kutofautiana katika baadhi ya mambo, lakini yasitufanye tuvunje umoja wetu. Hofu, hisia na mazoea vinaweza kuwa sababu mojawapo katika kuvuruga umoja wa watu. Mipango ya maendeleo haitawezekana kama tunahofiana, tunachukiana, tunawindana, tunatuhumiana, tunadhulumiana, tunashitakiana nakadhalika.
Tunaweza tusiogope macho ya watu lakini kama tunakwenda makanisani misikitini angarau tushitakiwe na nafsi zetu kwa Mungu, kwasababu tuna maisha mafupi sana duniani kuliko muda tunaoishi makaburini na huko hatuendi na vyeo, pesa au chochote sisi sote ni nyama ya udongo.Tuhubiri upendo zaidi kuliko chuki, hivi huwa tunajisikiaje tunapokuwa peke yetu baada ya kusema uongo hadharani.
Umoja tuliokuwa nao kama taifa ulijengwa juu ya misingi ya haki, usawa na utu, tunapoanza kuteleza katika misingi hiyo hatuwezi kutegemea matokeo tofauti na kutengana, ili tuendeleze umoja huo ni muhimu kuheshimu misingi hiyo.Tanzania kutokuwa na matatizo ya ukabila wala udini si kwa bahati mbaya ni kazi ilifanyika kuhakikisha kwamba mambo haya hayatugawi na hayatatugawa tutaendelea na dini zetu au makabila yetu tukiwa wamoja.
Kadhalika mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao upo kwa mujibu wa Sheria usiwe sababu ya kutugawa, tunaweza kuwa na mfumo huu bila kugawanyika, tatizo moja naliona ni juu ya hofu ya kupata na kupoteza madaraka, lakini lazima tutambuwe kwamba madaraka si jambo la kudumu ingalikuwa ni hivyo basi mpaka leo tungalikuwa tunatawaliwa na wakoloni. Tukubaliane kwamba kama nchi kuna wakati tunaweza kuwa tunapitia katika kipindi kigumu, lakini ni busara zaidi kutazama changamoto mbalimbali zinazotufanya tusiwe wamoja, tukizibaini tukae tuzungumze kwaajili ya kuzipatia ufumbuzi badala ya kushitakiana.
Hakuna mahala popote duniani mashitaka yamewahi kuleta amani na umoja badala ya uhasama, kinachofanya mahabusu na magereza zetu zinajaa watu si kwasababu ya watu wanaotenda uharifu bali ni kwasababu ya kupenda sana mashitaka badala ya mazungumzo nje ya mahakama na bahati mbaya sana dunia ya leo imekuwa kama kijiji tofauti na hapo zamani, ambapo jambo lolote lilifanyika bila dunia kuwa na habari.
Mwisho naweza kusema, kuna haja ya kuimarisha umoja na mshikamano wetu kama taifa, tunaweza tusiseme lakini dhamiri zetu zina kili juu hali halisi tulionayo katika nchi, umoja wetu ndiyo maendeleo yetu, utengano wetu ndiyo umaskini wetu, tunaweza kuchagua kuwa na maendeleo ama kuwa na migogoro isiyoisha na matokeo yake tukashindwa kupiga hatua za kimaendeleo tuzungumze, tujadiliane, tukubaliane tusonge mbele.

Upvote
1