SoC01 Maendeleo binafsi, ni Maendeleo ya Jamii nzima

SoC01 Maendeleo binafsi, ni Maendeleo ya Jamii nzima

Stories of Change - 2021 Competition

Tumain Temu

New Member
Joined
Sep 17, 2021
Posts
0
Reaction score
1
“Maendeleo binafsi, ni Maendeleo ya Jamii nzima”.

Habari zenu, ndugu wana Jamii Forums, haswa jukwaa hili la "stories of change". Ni tumaini langu sote tu wazima wa afya.

Andiko hili litaangazia juu ya ukombozi wa fikra.

Kama ifuatavyo;
Mtaji wa kwanza wa Maendeleo binafsi ni Ukombozi wa Fikra au Mawazo. Maendeleo binafsi uwanza kwa kujiuliza swali hili “kwa nini? Naishi” kisha baada ya kupata majibu unajitabia vyema kuishi ndani ya kusudi kwa kutokupapasa papasa mambo kama ilivyo ada ya watu wengi siku hizi, mara mfanyabiashara asubui, dalali mchana na mwanasiasa jioni. Utambuzi binafsi wa Mwl Julius Kambarage Nyerere ni mfano mojawapo wa kauli hii ya “Maendeleo binafsi, ni Maendeleo ya Jamii nzima” kwani, Tanzania tunajivunia utambuzi na jitihada zake za Mapinduzi kutoka mikononi mwa wakoloni.

Kwanini naishi?; Hili ni swali ambalo kila mtu atakaye mafanikio ni lazima kujiuliza swali hili. Kwani, kujua sababu ya kuishi kwa kila mtu ndani ya jamii, ni msingi mkubwa wa maendeleo katika Nyanja mbalimbali ndani na nje ya jamii hiyo.

Mfano: Mtu akijua sababu ya yeye kuishi tangu ang'ari kijana, kuwa yeye kapewa kipawa cha kuongoza. Hii ni nzuri sana kijana kutambua mapema maana itamfanya mtu huyo aweze kujiandaa mapema kuwa kiongozi bora nasi bora kiongozi, kwa kujitabia vyema ilikufikia kusudi la yeye kuishi pia kujifunza zaidi maswala yote yanayo gusa jamii na uongozi kupitia Nakala na Vitabu mbalimbali vyenye mandhari ya uongozi.

Hivyo jamii itanufaika vyema na kiongozi huyo ufikapo wakati wake wa kuongoza, kwa maana huo ni wito wake kwa hapa Duniani (Tatizo la uongozi haliko kwenye chama, tatizo liko kwa viongozi au mtu wenyewe). Kama ilivyo ada ya sasa “Watu waona bora kuwa viongozi ili waweze kujichumia fedha na mali za umma kwa urahisi” Pia kuna baadhi ya viongozi wanaojifunza uongozi wakati wa kufanya uongozi, hili nalo ni tatizo maana urudisha nyuma kasi ya maendeleo ya jamii au nchi usika, hivyo utaona kutokujitambua mapema kumesababisha kuzorota kwa kasi ya maendeleo ndani ya jamii au nchi.

Athari za kuishi humu Duniani pasipo kujua sababu ya wewe kuishi: Watu wengi hatujui kwa nini tunaishi, hili ni tatizo kubwa linalo ikumba jamii yetu pasipo kujua au kutambua kwa maana watu tunaishi ili mradi mkono umeingia kinywani na siku kupita tu. Matokeo yake ni kuishi mtazamo wa “Popote Kambi” au kwa lugha nyingine unaweza sema "Maisha ya majaribio" .

Mungu haku-muumba mwanadamu kwa bahati mbaya, wenda wewe umeumbwa ufanye kazi ya udaktari kwa nafasi ya Udaktari bingwa wa Moyo basi pasipokujua kwanini unaishi au pasipo kujua kusudi la wewe kuumbwa unaishia kujihusisha au kijichanganya na siasa hivyo kuwa mwanasiasa wa kusifia sifia wakubwa (wenye vyeo) hata pale panapo hitaji kukosolewa ili mradi tu kupata teuzi. Tatizo si popote kambi, tatizo ni kujua mahala sahihi pa wewe kuweka kambi.

Mama mmoja siku za uzee wake alimwita mwanaye, akasema kiwanja hiki nitamwezesha mkuu wa shirika la Watoto yatima lakini wewe nitakuachia Pete hii, niliyoachiwa na Babu yako mzaa Babu yako Kijana akachukia sana nafsi mwake japo alionyesha uso wa furaha mbele za mama yake lakini Mama alitambua hilo kama usemi usemao “Jicho la Mtu mzima, la ona mbali” au “Amjuaye mwana, mzazi”.

Mama akamwagiza mwanaye kwenda kwa wanunua vyuma chakavu kuulizia wangeweza kununua hiyo pete kwa bei gani? Aliambiwa sh.500/= akarudi na kumweleza mama yake bei hiyo aliyo ambiwa, mama akamwagiza tena kwenda kwa wanunuaji wa mikufu na pete za zamani, kwa hapo akaambiwa sh.50,000/= akaagiziwa tena kwa wafua dhahabu na madini ya chuma hapo akaambiwa sh.5,000,000/= kwa awamu hii kijana alirudi nyumbani na tabasamu kubwa mno alipofika nyumbani na kumweleza mama yake Habari za mambo yote hayo akifikiri amekwisha yafikia mafanikio Lakini mama akamwagiza tena kwenda kwenye nyumba za makumbusho kuulizia wao wangeweza kununua kwa bei gani pete hiyo alipo fika aliambiwa watanunua kwa Sh. Milioni mia moja kwani ni kitu pekee cha thamani na cha garama kilicho tafutwa si chini ya miaka 25 iliyo pita, ndipo kijana huyo akarejea nyumbani na kumweleza kama alivyo ambiwa.

Mama akamwambia “Mwanangu takaujue na utambue mahala sahihi pa wewe kujizatiti kimaisha kwani ukiwa sehemu sahihi utathaminiwa, utafanikiwa na utaheshimika sana nasi vinginevyo kama ulivyo ona mahala sahihi pa hiyo pete kuwekwa jinsi kulivyo thaminiwa sana kuliko mahala pengine uliko pita awali”.

Namna ya kujua sababu ya wewe kuishi: Mosi, mwombe MUNGU akuongoze katika kila hatuazako za kutaka kujua sababu ya wewe kuishi. Pili, mwombe MUNGU akujuze kusudi la kuzaliwa kwako hapa duniani kwani kila binadamu anakitu chatofauti au chakipekee zaidi alicho umbwa nacho na mwenye kujua hilo ni MUNGU Pamoja na wewe mwenye, mwenye kubalikiwa kipawa hicho pale tu ufanyapo tathimini ya Maisha yako.

Tatu, tenga muda wa kutosha kisha tathimini kwa kina ni vitu gani unapenda sana kufanya kwa kujari na kwaumakini mkubwa zaidi hata bila malipo wewe uko tayari kufanya kitu hicho au kushiriki kwa asilimia zote, au ni kitu gani? Ukiambiwa kufanya, kusikiliza au kuona wakati unakazi nyingine za msingi za kufanya uko radhi kuachana nazo kwa mda ilikufanaya jambo hilo kwa u weledi mkubwa.

Pia unaweza uliza wazazi wako, mlezi au Rafiki yako wa karibu sana, swali hili “Hivi mimi na stahili kuwa nani?” sikiliza majibu yao na uyafanyie tathimini kwa kulinganisha hayo majibu uliyo pokea kutoka kwa jamaa zako wa karibu na majibu ulio pata baada ya kupitia namna ya kwanza, ya pili na ya tatu kama nilivyo eleza.

Faida za kujua kwanini unaishi: Mosi, ni kumjengea muhusika ujasiri binafsi wa kujieleza na kujipambanua kimawazo na kimtazamo mbele ya jamii hususani katiak kusudi lake. Pili, kumsaidia muhusika kutambua na kujua changamoto zinazo ikabili jamii au nchi yake au eneo lake anamo-ishi. Tatu, kumjengea muhusika nidhamu ya muda, tabia na pesa. Pia, kumsaidia muhusika kuchagua nini afanye, nini asikilize na nini atazame kwa maana “You are what you read” “or listen or Doing frequently”. Pia kumsaidia muhusika kuchagua watu au marafiki sahihi wa kuambatana nao. Mwisho, kuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo kwa jamii au nchi ulioko ni lazima kila mtu kulitambua kusudi kisha kufanya bidii ya kuliishi kusudi hilo.

Note: Baadhi ya watu wakiisha tambua kwa nini wanaishi, uanza kufikilia ni kwa jinsi gani watafikia kusudi lao, ndugu yangu usitake kujua njia gani utapitia au kutumia hadi kufikia kusudi kwa maana hutoweza kupitia hizo njia uzifikiriazo, cha msingi wewe ni kujitabia vyema katika kusudi kwani Tabia njema ni mtaji tosha.

Unaweza soma Habari za Yusufu mwana wa Yakobo (soma Biblia: Mwanzo sura ya 37,38,39,40 hadi 41) inaeleza namna Yusufu alivyo tambua mapema sababu ya yeye kuishi akiwa na umri wa miaka 17, hakujua namna ya kufikia au kukamilisha kusudi lake lakini mwisho wake ulikuwa mzuri kwani aliweza kufikia kusudi aliloumbiwa kwa kujitabia vyema katika sababu ya yeye kuishi na kuipa kipaumbele sababu hiyo pasipo kujali ugumu aliokumbana nao katika safari yake ya kufikia sababu hiyo ya yeye kuishi hapa Duniani kwani ulipofika wakati wake jamii yake na jamii za watu wengine walinufaika sana na uongozi wake. Asante.

“Maendeleo binafsi, ni Maendeleo ya Jamii nzima”.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom