Maendeleo gani mapya mmepata kijijini/mtaani kwenu kati ya 2015 hadi leo 2020?

Barabara Zina mahandaki ya kufa mtu ,Shule Kila siku tunaitwa tukatoe michango Mara ya uji ,chakula ,mlinzi,maji, hospital hakuna dawa, watumishi wa umma hawana adabu kabisa.
 
kwangu hakuna kilichofanyika hata nukta yaani alivyoviacha Kikwete ndo hivyo hivyo
 
Hivi mmewahi kujiuliza kwa nini viongozi wakuu wanapokwenda kwenye shughuli za khtaifa pale uwanja wa taifa hutumia barabara ya Kilwa ?Ukweli ni kwamba barabara inayounganisha uwanja wa taifa kupitia maghorofa ya Keko,Keko fanicha,VETA hadi mataa ya Nyerere rd ina mahandaki kibao.Kiukweli wilaya hii ya Temeke barabara zake nyingi ni za hovyo.Mathalani barabara inayoanzia Davis kona Tandika kupita maghorofa ya Tandika kuelekea mwembe yanga hadi mahakama ya mwanzo Temeke nayo majanga.Hata ile toka Majaribio hadi Temeke Sudani ni aibu.Mbunge wa huku angekuwa ni toka chama pinzani mbona angejuta.Hivyo tunapopiga chapuo kuna haya pia na hizi kero ni za miaka mingi tu hazija anza juzi.
 
Faida ya awamu hii ni kuwa. 1 wanapima na kugawa vipimo vya UKIMWI bure.
Hasara
1. Bunge lipo gizani
2 Kondomu bei kubwa na hadimu
3 Chumvi imepitaka bei ya Sukari
 
Vipi huko mtaani/kijijini kwako nini kipya kimeongezeka kama ishara ya maendeleo kuanzia 2015 hadi 2020?
3: Kupimiwa viwanja mtaa mzima na kupewa mawe (mchakato endelevu).
9: ongezeko la route ya dadadala ambapo zamani tulikuwa tunatumia hadi 1200 kwenda kusaka fwedha jijini sasa ni 600 tu.

Ni hayo mawili huku mtaani kwetu, na tunashukuru kwa kweli kodi tuliyoitoa imefanya hayo, ila pia hela imekuwa ngumu kuipata
 
Hapa kwetu Area D dodoma matukio ya kutisha kutekwa na kupotea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…