Maendeleo huletwa na wananchi wenyewe kwa kulipa kodi

Maendeleo huletwa na wananchi wenyewe kwa kulipa kodi

songo mwene

Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
91
Reaction score
101
Maendeleo huletwa na wananchi wenyewe kwa kulipa kodi, ni jukumula Serikali kuhakikisha inatengeneza sera na namna bora ya kuhakikisha kila Mwananchi analipa kodi,

Serikali ya awamu ya Sita iliona ni bora kuziingiza kodi kwenye miamala ya simu ili kila unapofanya muamala ikatwe kodi moja kwa moja.

Jambo Hilo ni zuri pengine linaweza kuwa na changamoto zake pengine kuhusu ukubwa wa makato lkn nia ni njema.

Siku za hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii tuliona wachina wakitaka kuumiliki uwanja wa ndege wa nchi ya Uganda baada ya kushindwa kulipa deni lao hii inatupa funzo kuwa kila Mwananchi aendelee kulipa kodi ili kuepuka mikopo kutoka mataifa makubwa kwani mikopo hiyo huwa na riba kubwa kwahiyo Serikali iendelee kubuni vyanzo vya mapato bila kumuumiza Mwananchi wa kawaida.
 
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato unafaida gani?
 
Na hakuna maendeleo baada ya kodi kulipwa, ikatumika kununulia mavieete kwa viongozi, na matumzi yasiyo na tija ya moja kwa moja na walipa kodi.
 
Lipa Kodi il watu wapate kuiba zaidi

Wasinipakazie ufisadi ulikuwepo awamu ya 5 siyo awamu hii ya 6

Oooh nimesahau hivi bodi ya bandari inavyofanya madudu (kutafuna pesa za serikali kiulaini) niliichagua lini?
 
Tulipe Kodi lakini siyo kulipa Tozo
 
tulipe kodi kwa maendeleo yetu na vizazi vyetu.

ktk ulimwengu huu wa sasa hakuna vya bure.
 
Wewe unalipa?
Utatumiwa na mikoa ya Kagera, Geita na kigoma kama ilivyo KIA unatumika na mikoa ya kilimanjaro, Arusha na Manyara na kwa watalii wanaokuja Serengeti sababu Mara na Manyara hakuna uwanja wa kutua ndege kubwa hivyo hivyo kwa Geita mjini, mkoa wa Kagera na kigoma hakuna viwanja vya kutua ndege kubwa kama airbus.
 
Maendeleo huletwa na wananchi wenyewe kwa kulipa kodi, ni jukumula Serikali kuhakikisha inatengeneza sera na namna bora ya kuhakikisha kila Mwananchi analipa kodi,

Serikali ya awamu ya Sita iliona ni bora kuziingiza kodi kwenye miamala ya simu ili kila unapofanya muamala ikatwe kodi moja kwa moja.

Jambo Hilo ni zuri pengine linaweza kuwa na changamoto zake pengine kuhusu ukubwa wa makato lkn nia ni njema.

Siku za hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii tuliona wachina wakitaka kuumiliki uwanja wa ndege wa nchi ya Uganda baada ya kushindwa kulipa deni lao hii inatupa funzo kuwa kila Mwananchi aendelee kulipa kodi ili kuepuka mikopo kutoka mataifa makubwa kwani mikopo hiyo huwa na riba kubwa kwahiyo Serikali iendelee kubuni vyanzo vya mapato bila kumuumiza Mwananchi wa kawaida.
Nyie wajinga sikilizeni. Hakuna asiyejua umuhimu wa kulipa kodi. Watu wanahoji matumizi ya anasa ya viongozi wa serikali na CCM kwa kutumia kodi zetu. Magari ya anasa kwa mfano. Kusafiri kwa madaraja ya juu kwenye ndege kwa mfano. Kulala hotel za gharama kwa mfano. Safari zisizo na maana kwa mfano. Maisha ya anasa wanayoishi kwa mfano. n.k.
 
Back
Top Bottom