Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

SI siri kwamba katika kampeni za urais za uchaguzi wa Oktoba 31, nilivutiwa zaidi na mgombea wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa kuliko wa CCM, Jakaya Kikwete.

Sababu ni nyingi lakini moja kubwa ni kwamba Dk. Slaa alikuwa ni alama ya mabadiliko tunayoyahitaji katika nchi yetu wakati ambapo Kikwete alikuwa ni alama ya muendelezo wa mambo yale yale (status quo).

Hata kwenye kampeni zao wawili hao walijipambanua kwa misingi hiyo hiyo – Kikwete alikuwa anamwaga ahadi za kujenga hiki na kile (wakamwita ‘Bwana Miradi) lakini Dk. Slaa yeye aliahidi kuleta mabadiliko ya kisera na kimuundo katika uendeshaji wa serikali.

Mabadiliko aliyoyaahidi Dk. Slaa ni pamoja na Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano na tume mpya huru ya taifa ya uchaguzi. Kwa hakika, Dk. Slaa alikwenda mbali zaidi kwa kuahidi kuwa angeuanza mchakato wa kuipa Tanzania katiba mpya ndani ya miezi sita tu ya kuingia kwake Ikulu.

Ni bahati mbaya kwamba Dk. Slaa hakuweza kuingia Ikulu, kwa sababu ya kuchakachuliwa kwa kura zake, lakini je; Watanzania tukubali kwamba kutoingia kwake Ikulu ndio uwe mwisho wa mabadiliko hayo mawili tunayoyahitaji kwa ustawi wa taifa letu?

Sijui wewe msomaji jibu lako ni lipi kwa swali hilo, lakini langu mimi ni ‘hapana’. Tunapaswa sote kuanzisha kampeni ya kitaifa ya kudai mambo hayo mawili; kwani ni dhahiri sasa CCM na serikali yake, haiwezi kuyaleta bila kushinikizwa.

Nasisitiza kwamba CCM na serikali yake haiwezi kuyaleta kwa hiari, kwa sababu viongozi wake si visionary wa kuweza kuona jinsi ukosefu wa mambo hayo mawili unavyoweza kuvuruga amani na usalama wetu huko mbele ya safari.

Na hapo ndipo ninapomkumbuka Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Enzi zake, Mwalimu aliyaheshimu mno mabadiliko ya nyakati na aliyasoma vyema maandiko ukutani, na kila alipoona kuna jambo linaloweza kutishia amani na umoja wa Watanzania, alichukua hatua kulirekebisha au kulikemea. Hakusubiri wananchi waanze kushinikiza mabadiliko hayo.

Ni kwa muktadha huo Mwalimu aliyaona mabadiliko ya nyakati na kuyasoma maandiko ukutani, na hivyo kupendekeza Tanzania iachane na mfumo wa chama kimoja cha siasa na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi; jambo ambalo, hatimaye, lilitimia mwaka 1992.

Ni kwa muktadha huo vilevile, Mwalimu aliyaona mabadiliko ya nyakati na kusoma maandiko ukutani, na kushauri iundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Iliwachukua watawala wetu karibu miaka 14 kuiona lojiki ya ushauri huo wa Mwalimu, na ndipo walipolitekeleza wazo hilo mwaka huu.

Kwa kumbukumbu hizo chache, nadiriki kusema kwamba kama Mwalimu Nyerere angelikuwepo leo hai, angelikuwa wa kwanza kuishauri CCM na serikali yake kuipa Tanzania Katiba mpya inayoendana na mazingira ya sasa, na pia kuipa tume mpya huru ya taifa ya uchaguzi. Asingelisubiri shinikizo la wananchi au wafadhili kuleta mabadiliko hayo.

Mwalimu angalipendekeza hivyo kwa sababu alikuwa kiongozi visionary anayeona hatari iliyopo mbeleni ya kuendelea kuwanyima Watanzania mabadiliko hayo mawili makubwa ya kimsingi.

Kwa sasa hatuna tena kiongozi visionary wa sampuli ya Nyerere anayeweza kusimamia mchakato wa kuleta mabadiliko hayo bila shinikizo la wananchi au wafadhili (wazungu).

Binafsi, niliisikiliza hotuba ya Rais Kikwete ya Alhamisi iliyopita ya kuzindua Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano nikiwa na matarajio kwamba angelizungumzia changamoto hizo kubwa za kidemokrasia zinazoikabili nchi yetu kwa sasa na kuahidi kwamba atazishughulikia. Kwa mshangao mkubwa, Kikwete hakuzungumzia kabisa suala la Katiba mpya wala Tume huru ya taifa ya uchaguzi; japo anajua Watanzania wengi wanalilia mambo hayo mawili pamoja na kufutwa kwa sheria zile 40 kandamizi.

Ni dhahiri rais wetu haioni hatari iliyoko mbele yetu endapo tutaingia katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 tukiwa na katiba hii hii na tukiwa na tume hii hii ya uchaguzi.

Nilieleza wiki iliyopita kwamba yaliyotokea katika uchaguzi wa Oktoba 31 ni maandiko tosha ukutani yanayoashiria mambo mabaya zaidi kwenye chaguzi zijazo kama mabadiliko hayatafanyika ya kuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Kauli tata iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi (JWTZ), Luteni Jenerali Shimbo, siku chache kabla ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, madai kwamba Usalama wa Taifa ulishirikishwa kwenye uchakachuaji wa kura na madai kwamba huko Kagera polisi waliwapiga wananchi mabomu ya kutoa machozi ili kujenga mazingira ya kuchakachua kura, si viashiria vyema kwa taifa lililopania kulinda amani na usalama wake.

Tungekuwa na viongozi visionary, wangeliona kwamba wananchi wameshaanza kupoteza imani na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tuliyonayo sasa. Wangeliona pia kwamba wananchi hawaridhiki na Katiba yetu ya tangu Uhuru na wanataka mpya.

Nisisitize tena kwamba tungelikuwa na viongozi visionary, wasingeendelea kutahadharisha tu kuhusu kupotea kwa amani na usalama; ilhali wanajua kwamba kuendelea kuwanyima Watanzania mabadiliko hayo (ya Katiba na Tume mpya ya uchaguzi), ni kupanda mbegu za kutowesha amani na utulivu huo ambao wameapa kuvilinda.

Nihitimishe kwa kusema kwamba kwa kuwa watawala wetu hawaioni hatari iliyoko mbeleni ya kuendelea kuwanyima Watanzania mabadiliko hayo, umma uchukue jukumu la kuwashinikiza (kwa njia za amani) kuleta mabadiliko hayo ili kuiepusha nchi yetu na vurugu zozote zinazoweza kusababisha umwagaji damu.

Ni rai yangu, hivyo basi, kwa Watanzania wote, wabunge, wanasiasa, waandishi wote wa habari, asasi zote sisizo za kiserikali zinazopigania haki za binadamu n.k, na kwa kushirikiana na wahisani wetu wa kigeni tuunganishe nguvu kuyadai mabadiliko haya muhimu ya kidemokrasia kutoka kwa watawala wetu.

Ni jambo la kutia moyo kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania, Jaji Kiongozi Mstaafu, Amiri Manento, aliwasha moto wa aina hiyo wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa haki za binadamu na Utawala Bora, Jaji Manento alisema hivi: “Ni vyema Watanzania wote sasa tukaamka na kusema tunataka Katiba mpya.”

Mimi nakubalina kabisa na Jaji Manento kwamba wakati umefika Watanzania tuamke na kudai mabadiliko hayo muhimu ya kidemokrasia, na ndiyo maana napendekeza mwaka ujao wa 2011 wimbo uwe mmoja tu: Katiba mpya, Tume mpya!
 
Tanzania ikifa, maiti yake itanuka vibaya sana (na nisingependa hilo litokee)!

Ndugu zanguni wanaJF na watanzania wenzangu popote pale mlipo; ingawa nimejawa na hofu kubwa, bado kisima changu cha matumaini hakijaanza kukauka. Bado nimejawa na matumaini kuwa-tukiiunganisha nguvu zetu, kwa pamoja tunaweza kabisa tukaepusha "inevitable death" ya nchi yetu.

Vinginevyo, huko tuendako ndugu zanguni, si kwema kabisa.

And so, badala ya kupiga porojo hapa jukwaani na kupeana matumaini ya uongo kuwa ipo siku CCM (kwa hiari yake yenyewe), itashika adabu na kuanza kujiheshimu hata kutupatia Katiba Mpya, sasa ni wakati muafaka wa kuanza rasmi mchakato wa kudai Katiba Mpya!

Sasa ni wakati wa kufikiria na kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kujaribiwa au kufanyika nchini mwetu. Mambo kama vile-kuishinikiza Serikali dhalimu ya CCM iruhusu na ikubali madai yetu ya Katiba Mpya.

Nashauri kwanza tuanze na njia ambayo ni rahisi kushinda njia zote.

Njia ya Petition.

Hilo likishindikana, then tutaruka kwenda hatua nyingine-hatua kali zaidi kuliko hii ya petition (naomba nisiizungumze hapa kwasasa-maana najua makachero wa-CCM watairukia na kuanza kuifanyia kazi/kubuni mbinu za kutukabili).

Katiba ya sasa ina mapungufu mengi mno, na yafuatayo ni mambo ambayo ningependa kuona yanafanyiwa mabadiliko:

(1). Mawaziri na manaibu waziri wateuliwe toka nje ya Bunge
(2). Wakuu wa mikoa wapigiwe kura moja kwa moja na wananchi wa mikoa yao
(3). Serikali iruhusu wagombea binafsi (Independent candidates)
(4). Madaraka ya Rais yapunguzwe (kuna mjadala mrefu hapa)
(5). Katiba iruhusu matokeo ya Rais kupingwa mahakamani
(6). Kila mkoa uwe na mwanasheria mkuu wake
(7). Mkuu wa Tume ya Uchaguzi (NEC) asiteuliwe na Rais
(8). Cheo cha mkuu wa wilaya kifutwe (badala yake Mkungenzi wa maendeleo, apewe madaraka hayo)

P.S. Unaweza ukaongezea mambo mengine ambayo ungependa kuona yanafanyiwa mabadiliko kwenye hii Katiba Mpya tunayodai (ukisha sign petition, weka comment ya jambo unalotaka kuona linafanyiwa marekebisho).

Ushirikiano wenu nyote unahitajika. Saini petition hapa: TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition

- Mkuu heshima yako sana, la msingi sana hapo ni NEC ambayo ndio kwanza imeletea tafrani recently, sasa naomba kukuuliza hivi unataka kwenye katiba yako mpya NEC ichaguliwe na nani ndio itakua FAIR, kwako na kwa wana-CCM?

William.
 
Ni kwa kelele na sauti ENDELEVU tu, ndipo kilio hiki kitasikilizwa na kukubalika, na hatimaye mijadala huru ya uelimishaji kwa kila raia kuruhusiwa. Uzoefu unaonyesha kuwa walio madarakani wana kawaida ya kupinga sana mabadiliko, maana hawajui aftermath yake, hivyo tusitegemee kabisa huruma yoyote toka kwenye ruling class.
 
Tanzania ikifa, maiti yake itanuka vibaya sana (na nisingependa hilo litokee)!

Ndugu zanguni wanaJF na watanzania wenzangu popote pale mlipo; ingawa nimejawa na hofu kubwa, bado kisima changu cha matumaini hakijaanza kukauka. Bado nimejawa na matumaini kuwa-tukiiunganisha nguvu zetu, kwa pamoja tunaweza kabisa tukaepusha "inevitable death" ya nchi yetu.

Vinginevyo, huko tuendako ndugu zanguni, si kwema kabisa.

And so, badala ya kupiga porojo hapa jukwaani na kupeana matumaini ya uongo kuwa ipo siku CCM (kwa hiari yake yenyewe), itashika adabu na kuanza kujiheshimu hata kutupatia Katiba Mpya, sasa ni wakati muafaka wa kuanza rasmi mchakato wa kudai Katiba Mpya!

Sasa ni wakati wa kufikiria na kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kujaribiwa au kufanyika nchini mwetu. Mambo kama vile-kuishinikiza Serikali dhalimu ya CCM iruhusu na ikubali madai yetu ya Katiba Mpya.

Nashauri kwanza tuanze na njia ambayo ni rahisi kushinda njia zote.

Njia ya Petition.

Hilo likishindikana, then tutaruka kwenda hatua nyingine-hatua kali zaidi kuliko hii ya petition (naomba nisiizungumze hapa kwasasa-maana najua makachero wa-CCM watairukia na kuanza kuifanyia kazi/kubuni mbinu za kutukabili).

Katiba ya sasa ina mapungufu mengi mno, na yafuatayo ni mambo ambayo ningependa kuona yanafanyiwa mabadiliko:

(1). Mawaziri na manaibu waziri wateuliwe toka nje ya Bunge
(2). Wakuu wa mikoa wapigiwe kura moja kwa moja na wananchi wa mikoa yao
(3). Serikali iruhusu wagombea binafsi (Independent candidates)
(4). Madaraka ya Rais yapunguzwe (kuna mjadala mrefu hapa)
(5). Katiba iruhusu matokeo ya Rais kupingwa mahakamani
(6). Kila mkoa uwe na mwanasheria mkuu wake
(7). Mkuu wa Tume ya Uchaguzi (NEC) asiteuliwe na Rais
(8). Cheo cha mkuu wa wilaya kifutwe (badala yake Mkungenzi wa maendeleo, apewe madaraka hayo)

P.S. Unaweza ukaongezea mambo mengine ambayo ungependa kuona yanafanyiwa mabadiliko kwenye hii Katiba Mpya tunayodai (ukisha sign petition, weka comment ya jambo unalotaka kuona linafanyiwa marekebisho).

Ushirikiano wenu nyote unahitajika. Saini petition hapa: TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
na kuongezea ...kila mtanzania awe na kitambulisho cha uraia...( ID CARD)
 
Napendekeza kuwa katika katiba hiyo mpya tunayodai, iwepo Mahakama ya katiba ambayo itaamua pamoja na mambo mengine, kuhusu uhalali wa ushindi wa Raisi. Pia ndiyo itaamua kuhusu mambo makuu yanayohusu katiba, ikiwa ni pamoja na kufanywa mabadiliko ya msingi
 
mkuu point zako nzuri sana,ila naomba nipingane na wewe kwenye suala la kupinga matokeo ya urais mahakamani maana kma unavyotujua sisi watanzania hatuna utamaduni kukubali kusema tumeshindwa hata kma kila kitu kinaonesha tumeshindwa kihalali.

Mfn mzuri ni hizi timu zetu za mpira utakuta wamezidiwa kila kitu na wamefungwa ukiwauliza watakupa sababu za kitoto kbs,hii ni hv hv mpk kwa wanasiasa,kwaiyo me naona kama tukiweka suala la kupinga majibu mahakamani NCHI HAITA TAWALIKA,me nazan kuna na NEC huru inatosha kbs. Hayo ndo mawazo yako.m
Well, natambua concens zako mkuu. Ila kama uchaguzi wa wabunge unaruhusiwa kuwa challanged mahakamani, nadhani hata uchaguzi wa urais unaweza pia kupingwa mahakamani na mambo yakaenda sawa. Kwamba, hukumu yeyote itakayotolewa na mahakama kuu, basi itasimama. Ila hapa inabidi mahakama kuu pekee yake ndo' ipewe nafasi ya kusikiliza kesi. Plus, mchakato wa kuwapata majaji wa wamahakama kuu unapaswa kujadiliwa upya ili kuipa mahakama crediility na kuwafanya watu wawe na imani na maamuzi yeyote yale yatakayotolewa na mahakama hiyo.

Lakini pia naomba niongeze kitu ktk iyo list yako, naomba pia tushinikize kua wanasiasa walipe kodi pia. Maana hawa watu (rais,makamu wa rais,waziri mkuu, mawaziri na wabunge)hawalipi kodi kabisa,me naona hili ni ttz maana kma mtu ulipi kodi huwez kuwashinikiza wawekezaji walipe kodi maana wewe u don't feel tha pitch. Nazan wakilazinishwa kulipa kodi watawashika mashati na hao wawekezaji pia
Pendekezo lako ni zuri sana! Thank you!
 
Thanks again bro this is what i was fighting for........ Vipi kuhusu ile issue ya kuwa na hard copy as well.

You know majority ya watu hawapo online... and Once Dr. Slaa nilivyomuuliza kuhusu hii issue alisema tukipata kama 5million people wanaweza wakawa enough sasa that number kuipata online peke yake itakuwa tabu.

So I was suggesting kama una hard copy ili watu waziprint na kuzitoa copies na kuwapata watu mitaani na vijijini ili wazisaini all is needed ni address ya kuzipost pindi baada ya kuzijaza. Thanks again. Together we shall overcome
Bro, naandaa hard copy [Portable Document Format (PDF)] ambayo nitaipost hapa JF na kwenye blogs zingine (facebook included) ili watu waweza kudownload/print/toa copy na kuwapatia watu mitaani, mashuleni, makanisani, misikitini, (na... mechi za ligi kuu, maofisini, n.k) wasaini.

Nitazungumza na Dr. Slaa pia this weekend--kujadili jinsi ya kuwatumia wabunge wa Chadema katia mchakato huu wa kudai Katiba Mpya.

P.S. Nitakupatieni maelezo ya kutosha kuhusu jinsi ya kuzituma hizo form baada ya kuwa zimesainiwa. Ninahakika tukishirikiana, hizo sahihi millioni 5 zitapatikana within a year.
 
Yes huu ni wakati muafaka ni lazima tuingie uchaguzi 2015 na katiba mpya kwa manufaa ya Tanzania yetu. Kama watawala wako kwa ajili yetu wasingoje mpaka Tanzania iingie kwenye machafuko ndipo waanze kuitisha kura ya maoni kwa gharama ya damu ya wana wa nchi.

TANZANIA NCHI YANGU NITAKUPIGANIA KWA JASHO NA DAMU NA SITA ISHI KITUMWA BILA HOJA ZENYE MASHIKO NA HAKI NDANI YA NCHI YANGU.
 
- Mkuu heshima yako sana, la msingi sana hapo ni NEC ambayo ndio kwanza imeletea tafrani recently, sasa naomba kukuuliza hivi unataka kwenye katiba yako mpya NEC ichaguliwe na nani ndio itakua FAIR, kwako na kwa wana-CCM?

William.
Mkuu William, heshima kwako pia. Swali lako ni zuri sana. Well, katika Katiba Mpya tunayodai, suala la Tume ya Uchaguzi ya Taifa [National Electoral Commision (NEC)], ningependa tuige mfumo wa kimarekani ambapo Tume yao inaundwa na wajumbe sita (ambapo kisheria wajumbe kutoka chama kimoja hawaruhusiwi kuvuka watatu). In other words, kama wajumbe watatu watatoka CCM;then wawili watoke Chadema, na mmoja atoke CUF. Kadhalika, kwa mfumo wa kimarekani, ingawa wajumbe (nasisitiza, wajumbe na sio mkuu/mwenyekiti wa Tume); huteuliwa na Rais, chombo kinachoidhinisha wajumbe hao ni Senate (kwa Tanzania itakuwa Bunge la Jamhuri). On top of that, zinahitajika kura zaidi ya 4 kupitisha pendekezo/azimio lolote ambalo Tume hiyo itaamua. Na Uenyekiti wa Tume unazunguka kati ya wajumbe kila mwaka. Let's say mwaka huu mwenyekiti anatoka CCM, basi mwakani mwenyekiti atatoka CUF, na mwaka unafuata mwenyekiti atatoka Chadema. Miaka sita ikiisha then Rais anaweza akapendekeza majina mpya, yakapelekwa bungeni, yakapigiwa kura na wabunge wote; ama anaweza akaamua kupendekeza majina yale yale (cha msingi hapa ni kuhakikisha kuwa hakuna mjumbe anarudia Uenyekiti zaidi ya mara moja ndani ya kipindi cha miaka 6). Do you see my point here, mkuu? Mwenyekiti hateuliwi na Rais kabisa, hence inapunguza mzigo wa kutaka kumridhisha Rais kama ilivyo hivi sasa kwa 'kuchakachua kura' (Gee, I hate that euphemism, I prefer zaidi maneno 'kuiba kura').

P.S. Kwa mtizamo wangu, kambi ya Upinzani Bungeni iachiwe kazi ya kumpatia Rais majina ya watu watatu ambao wataingia kwenye hiyo tume ili Rais ayapeleke majina hayo pamoja na majina mengine matatu atakayopendekeza (Rais, akishirikiana na chama chake) ili yakapigiwe kura Bungeni. Who knows? Leo CCM iko madarakani. 2025 inaweza ikawa Chadema ama chama kingine tusichokijua. So, nadhani huu utakuwa mfumo mzuri, na wa haki. Na pia utaondoa lawama zisizo za lazima toka vyama vya mageuzi.

P.S. # 2: Mkuu, usisahau kusaini petition hapa:
http://www.gopetition.com/petitions/tunahihitaji-katiba-mpya.html
 
Kila mwananchi mwenye ufahamu wa maendeleo, sauti zenu zinahitajika katika kudai katiba mpya.
 
Madai ya kutaka Katiba mpya yamezidi kupamba moto nchini kufuatia wadau kadhaa kusema kwamba uchumi wa Tanzania hauwezi kukua endapo hakutafanyika juhudi za makusudi katika kuhakikisha katiba iliyopo inabadilishwa.
Maoni hayo yalitolewa jana jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, baada ya ufunguzi wa mkakati wa pili wa Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta II).
Zitto alisema uchumi wa nchi hauwezi kukua wakati katika Katiba iliyopo ina baadhi ya vipengele ambavyo haviungi mkono jitihada za kukuza uchumi huo.
“Uchumi wa Tanzania hauwezi kukua endapo hakuna Katiba imara, maana katika tathmini za uchumi, sheria ikiwa mbovu lazima na mfumo mzima wa uchumi uwe mbovu,” alisema.
Aidha, Zitto alimpongeza Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, kwa kukubali kuliingiza suala la mabadiliko ya Katiba katika mjadala ambapo alisema hiyo ni dalili nzuri ambayo ameionyesha kwa Watanzania.
“Ninampongeza sana Kombani kwa kukubali kuliingiza katika majadiliano suala la mabadiliko ya Katiba, ameonyesha dalili nzuri kwa Watanzania,” alisema na kuongeza: “Endapo atalifanikisha hili, atakuwa amejenga historia ya taifa na ya jinsia pia yeye kama mwanamke.”
Aidha, Zitto alitoa rai kwa serikali kusikia kilio cha Watanzania ambao wanataka mabadiliko ya Katiba hiyo kukubali kufanya marekebisho.
“Mabadiliko ya Katiba ni lazima yafanyike kwa kuwa bila hivyo ni vigumu kuondoa umaskini na pia lazima serikali ikubali kuzungumzia suala hilo,” alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Aliongeza kuwa wakati Tanzania inatarajia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake hapo mwakani, Serikali inapaswa kutathmini namna ambavyo imeongoza, namna ambavyo haki za watu zimelindwa pamoja na namna ambayo raslimali za taifa zilivyotumika.
Naye Mwenyekiti wa Asasi za Kiraia (Policy Forum), Moses Kulaba, alisema kuna umuhimu wa kuandikwa kwa Katiba mpya hususani katika kuangalia uwezekano wa kuwezesha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) pamoja na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwa nguzo huru ili zitekeleze majukumu yake kwa ufanisi zaidi.
Alisema japo kuwa vyombo hivyo vinafanya kazi, lakini bado uhuru wake ni mdogo sana jambo ambalo linavifanya kuonekana kwamba havifanyi kazi kwa ufanisi.
“Uwajibikaji katika vyombo hivi unaonekana kuwa si wa kiufanisi zaidi kutokana na kwamba vinabanwa…yaani ni kama mtu mwenye meno, lakini hawezi kung’ata,” alisema na kuendelea: “Endapo Katiba itabadilishwa kutakuwa na uhuru wa kuwajibika vizuri.”
Kulaba alisema wakati Tanzania inaingia katika mpito wa mabadiliko ya uchumi kutoka ujamaa kwenda soko huria, suala la Katiba halikujadiliwa na ndio maana hakuna mafanikio ya uchumi.
Wakati huo huo, Serikali imesema awamu ya kwanza ya Mkukuta imeshindwa kufanikiwa katika mpango wake wa kupunguza umaskini wa kipato na kuongeza kuwa suala hilo bado linahitaji jitihada binafsi.
Akizindua Mkukuta II, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema sababu zilizochangia kutofikiwa kwa malengo ya mkakati huo ni pamoja na viwango vya elimu visivyo na tija ya kutosha inayowezesha kupata ajira.
Alisema sababu nyingine ni tija ndogo katika uzalishaji inayosababishwa na uwekezaji mdogo na matumizi ya teknolojia duni, mapungufu katika kuibua vipaumbele vichache na usimamizi katika utekelezaji mdogo wa sera na mikakati ya kitaifa na kisekta.
Nyingine ni uwezo mdogo katika kushirikisha sekta binafsi na asasi za kijamii katika utekelezaji huo.
Alizitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na ukuaji mdogo wa mapato ya serikali ukilinganisha na mahitaji yake, uhaba wa viwanda vya kusindika mazao ya kilimo pamoja na sekta binafsi kushindwa kuhimili ushindani wa kimataifa na ongezeko la idadi kubwa ya watu.
Hata hivyo, Mkulo aliyataja mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya Mkukuta kuwa ni pamoja na utekelezaji wa jitihada za elimu na afya ambapo Tanzania ilifanikiwa kutoka nafasi ya 163 mwaka 2000 hadi kufikia nafasi ya 151 mwaka 2009 na kufanikiwa kutoka katika kundi la nchi za chini na kuingia katika nchi za kati.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema), ameitaka Serikali kubadilisha Katiba kwani bila kufanya hivyo mambo mengi hayawezi kutekelezwa kwa ufanisi.
Ndesamburo alitoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo ya ufundi katika kituo cha Women Education and Economic Centre (WEECE) kilichopo katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema nchi inapita katika matatizo makubwa kutokana na kuwapo kwa viongozi wengi ambao ni ving’ang’anizi wa madaraka, jambo linaloweza kuhatarisha amani ya taifa hili.
“Umefika wakati wa serikali kufanya mageuzi ya kweli ya Katiba ili amani na utulivu wa nchi iendelee kudumishwa na kulindwa kwa gharama yoyote ... hatutaki viongozi mafisadi,” alisema Ndesamburo.
 
waziri wa sheria...iwapo tume haitakuwa chini ya serikali itaripwa na nani? Alihoji.na amesema walishajaribu kufanya hivyo watu wakawa wanakimbia na masanduku ya kura na hamna wa kuwachukulia hatua za kisheria kwa sababu hawako chini ya serikali

when did they try? THAT'S THE DUMBEST EXCUSE EVEeeeR FOR A MINISTER...it's a typical NO-BRAINER, too stupid!?
 
Whew intelligent idea!

mie nimefoward hii link through my email : TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition

nimewaomba wasaini na waendelee kuizungusha! naomba na nyie mfanye vivyo hivyo. very soon will get filled!

nimeamini humu ndani mna vichwa!
 
Mkuu William, heshima kwako pia. Swali lako ni zuri sana. Well, katika Katiba Mpya tunayodai, suala la Tume ya Uchaguzi ya Taifa [National Electoral Commision (NEC)], ningependa tuige mfumo wa kimarekani ambapo Tume yao inaundwa na wajumbe sita (ambapo kisheria wajumbe kutoka chama kimoja hawaruhusiwi kuvuka watatu). In other words, kama wajumbe watatu watatoka CCM;then wawili watoke Chadema, na mmoja atoke CUF. Kadhalika, kwa mfumo wa kimarekani, ingawa wajumbe (nasisitiza, wajumbe na sio mkuu/mwenyekiti wa Tume); huteuliwa na Rais, chombo kinachoidhinisha wajumbe hao ni Senate (kwa Tanzania itakuwa Bunge la Jamhuri). On top of that, zinahitajika kura zaidi ya 4 kupitisha pendekezo/azimio lolote ambalo Tume hiyo itaamua. Na Uenyekiti wa Tume unazunguka kati ya wajumbe kila mwaka. Let's say mwaka huu mwenyekiti anatoka CCM, basi mwakani mwenyekiti atatoka CUF, na mwaka unafuata mwenyekiti atatoka Chadema. Miaka sita ikiisha then Rais anaweza akapendekeza majina mpya, yakapelekwa bungeni, yakapigiwa kura na wabunge wote; ama anaweza akaamua kupendekeza majina yale yale (cha msingi hapa ni kuhakikisha kuwa hakuna mjumbe anarudia Uenyekiti zaidi ya mara moja ndani ya kipindi cha miaka 6). Do you see my point here, mkuu? Mwenyekiti hateuliwi na Rais kabisa, hence inapunguza mzigo wa kutaka kumridhisha Rais kama ilivyo hivi sasa kwa 'kuchakachua kura' (Gee, I hate that euphemism, I prefer zaidi maneno 'kuiba kura').

P.S. Kwa mtizamo wangu, kambi ya Upinzani Bungeni iachiwe kazi ya kumpatia Rais majina ya watu watatu ambao wataingia kwenye hiyo tume ili Rais ayapeleke majina hayo pamoja na majina mengine matatu atakayopendekeza (Rais, akishirikiana na chama chake) ili yakapigiwe kura Bungeni. Who knows? Leo CCM iko madarakani. 2025 inaweza ikawa Chadema ama chama kingine tusichokijua. So, nadhani huu utakuwa mfumo mzuri, na wa haki. Na pia utaondoa lawama zisizo za lazima toka vyama vya mageuzi.

P.S. # 2: Mkuu, usisahau kusaini petition hapa:
TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition

- I mean heshima mkuu, angalau wewe unasema hoja ingawa bado hapa kutakwua na upungufu wa uwakilishwaji wa Wapizani katika kamati kwa sababu wapinzani wapo wengi kuliko ulivyowataja, lakini sio haba mkuu angalau umetoa an idea ambayo kwangu ina some sense kidogo, sawa sawa!

William.
 
Whew intelligent idea!

mie nimefoward hii link through my email : TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition

nimewaomba wasaini na waendelee kuizungusha! naomba na nyie mfanye vivyo hivyo. very soon will get filled!

nimeamini humu ndani mna vichwa!
That's so nice of you my friend! You did the right thing kuforward hiyo link through your email. Naamini kila mtu akifanya hivyo, basi lengo letu la kukusanya sahihi million 5 (kama Dr. Slaa alivyopendekeza), litafikiwa mapema sana. Plus, ninaandaa hard copy [PDF], ambayo watu watadownload, print, make some copies alafu wasambaze huko vijijini nako ili tuwafikie watanzania wote. Katiba Mpya tunayodai, inawagusa na itawaathiri (kwa namna moja ama nyingine) watanzania wote. Hivyo tungependa kuona wote wanapewa nafasi ya kushiriki/toa mawazo yao katika mchakato huu.

Please endeleeni kusaini petition hapa:
TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
 
- I mean heshima mkuu, angalau wewe unasema hoja ingawa bado hapa kutakwua na upungufu wa uwakilishwaji wa Wapizani katika kamati kwa sababu wapinzani wapo wengi kuliko ulivyowataja, lakini sio haba mkuu angalau umetoa an idea ambayo kwangu ina some sense kidogo, sawa sawa!

William.
Mkuu, unachosema ni kweli kabisa (wapinzani ni wengi kuliko nilvyowataja kwenye reply yangu). Lakini hilo ni jambo ambalo linaweza kupatiwa ufumbuzi mzuri kadiri hii debate inavyoendelea kuchanganyia. Binafsi, nadhani simple solution ni kutumia kigezo kinachotumika kutoa ruzuku ili kuwapata hao wawakilishi watatu toka kambi ya upinzani. Say, kwa mfano, Chadema mwaka huu kimepata 28% ya kura zote, then allocation ya wawakilishi kwenye tume tunayoizungumzia, izingatie hiyo perfomance pia. Kadhalika na kwa CUF and other political parties like TLP, DP, NCCR, UPDP, e.t.c. Anyway, hili ni suala ambalo pengine wataalamu wa sheria watahitajika kutupatia ushauri wa kisheria zaidi.
 
Hiyo ndio demokrasia, idadi ya wanaopigiwa kura doesn't matter. wenzetu waliondelea wanapigia kura hata majaji, mayors n.k
 
Mkuu, Edward Teller: unaruhusiwa pia kutoa mapendekezo yako kuhusu ni nini ungependa kiwemo kwenye Katiba Mpya tunayodai. Ukisha sign petition, kuna sehemu inakuruhusu kuweka comment, please put your comment there. Hizo comment zitapitiwa na watu wenye utaalamu kwenye mambo ya sheria, then comment zote zilizokaa vizuri, zitaingizwa kwenye hard copy ya petition. Naona Dr. Wilbroad Slaa ameitikia wito na kusaini petition. Naomba akina Zitto, Lissu,na Mbowe pia waige mfano wa mzee wetu, wasaini petition. Hope nimejibu swali lako.

Truly So Mr. BOngoTz, comment zetu ni muhimu sana. Katika hiyo sehemu ya comment unaweza kuandika kama outline ya mambo makuu ambayo unataka yabadilishwe katika katiba, hii itasaidia wale wanaopita comment hizo kuona wapi wengi wamewekea mkazo; because it is one thing kusaini katiba irekebishwe bila comment; but it is of essence kuweka wazi wapi katiba ya sasa unatulemea...; na hao wanaopita watakusanya zile items ambazo majority ya waliosaini wameweka kama priorities....a democratic move to change; sauti ya wengi wape
 
Sawa sawa, mkuu! Nimekupata. In fact, jana usiku niliamua kuoutline baadhi ya mambo makuu tunayotaka yafanyiwe marekebisho. I think ukingia kwenye petition utaona hayo mabadiliko. Plus, nitaendelea kufanya updates kadri mawazo mpya na mazuri yanavyozidi kutolewa. Shukrani kwa ushauri mzuri.
 
Back
Top Bottom