kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
SI siri kwamba katika kampeni za urais za uchaguzi wa Oktoba 31, nilivutiwa zaidi na mgombea wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa kuliko wa CCM, Jakaya Kikwete.
Sababu ni nyingi lakini moja kubwa ni kwamba Dk. Slaa alikuwa ni alama ya mabadiliko tunayoyahitaji katika nchi yetu wakati ambapo Kikwete alikuwa ni alama ya muendelezo wa mambo yale yale (status quo).
Hata kwenye kampeni zao wawili hao walijipambanua kwa misingi hiyo hiyo Kikwete alikuwa anamwaga ahadi za kujenga hiki na kile (wakamwita Bwana Miradi) lakini Dk. Slaa yeye aliahidi kuleta mabadiliko ya kisera na kimuundo katika uendeshaji wa serikali.
Mabadiliko aliyoyaahidi Dk. Slaa ni pamoja na Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano na tume mpya huru ya taifa ya uchaguzi. Kwa hakika, Dk. Slaa alikwenda mbali zaidi kwa kuahidi kuwa angeuanza mchakato wa kuipa Tanzania katiba mpya ndani ya miezi sita tu ya kuingia kwake Ikulu.
Ni bahati mbaya kwamba Dk. Slaa hakuweza kuingia Ikulu, kwa sababu ya kuchakachuliwa kwa kura zake, lakini je; Watanzania tukubali kwamba kutoingia kwake Ikulu ndio uwe mwisho wa mabadiliko hayo mawili tunayoyahitaji kwa ustawi wa taifa letu?
Sijui wewe msomaji jibu lako ni lipi kwa swali hilo, lakini langu mimi ni hapana. Tunapaswa sote kuanzisha kampeni ya kitaifa ya kudai mambo hayo mawili; kwani ni dhahiri sasa CCM na serikali yake, haiwezi kuyaleta bila kushinikizwa.
Nasisitiza kwamba CCM na serikali yake haiwezi kuyaleta kwa hiari, kwa sababu viongozi wake si visionary wa kuweza kuona jinsi ukosefu wa mambo hayo mawili unavyoweza kuvuruga amani na usalama wetu huko mbele ya safari.
Na hapo ndipo ninapomkumbuka Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Enzi zake, Mwalimu aliyaheshimu mno mabadiliko ya nyakati na aliyasoma vyema maandiko ukutani, na kila alipoona kuna jambo linaloweza kutishia amani na umoja wa Watanzania, alichukua hatua kulirekebisha au kulikemea. Hakusubiri wananchi waanze kushinikiza mabadiliko hayo.
Ni kwa muktadha huo Mwalimu aliyaona mabadiliko ya nyakati na kuyasoma maandiko ukutani, na hivyo kupendekeza Tanzania iachane na mfumo wa chama kimoja cha siasa na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi; jambo ambalo, hatimaye, lilitimia mwaka 1992.
Ni kwa muktadha huo vilevile, Mwalimu aliyaona mabadiliko ya nyakati na kusoma maandiko ukutani, na kushauri iundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Iliwachukua watawala wetu karibu miaka 14 kuiona lojiki ya ushauri huo wa Mwalimu, na ndipo walipolitekeleza wazo hilo mwaka huu.
Kwa kumbukumbu hizo chache, nadiriki kusema kwamba kama Mwalimu Nyerere angelikuwepo leo hai, angelikuwa wa kwanza kuishauri CCM na serikali yake kuipa Tanzania Katiba mpya inayoendana na mazingira ya sasa, na pia kuipa tume mpya huru ya taifa ya uchaguzi. Asingelisubiri shinikizo la wananchi au wafadhili kuleta mabadiliko hayo.
Mwalimu angalipendekeza hivyo kwa sababu alikuwa kiongozi visionary anayeona hatari iliyopo mbeleni ya kuendelea kuwanyima Watanzania mabadiliko hayo mawili makubwa ya kimsingi.
Kwa sasa hatuna tena kiongozi visionary wa sampuli ya Nyerere anayeweza kusimamia mchakato wa kuleta mabadiliko hayo bila shinikizo la wananchi au wafadhili (wazungu).
Binafsi, niliisikiliza hotuba ya Rais Kikwete ya Alhamisi iliyopita ya kuzindua Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano nikiwa na matarajio kwamba angelizungumzia changamoto hizo kubwa za kidemokrasia zinazoikabili nchi yetu kwa sasa na kuahidi kwamba atazishughulikia. Kwa mshangao mkubwa, Kikwete hakuzungumzia kabisa suala la Katiba mpya wala Tume huru ya taifa ya uchaguzi; japo anajua Watanzania wengi wanalilia mambo hayo mawili pamoja na kufutwa kwa sheria zile 40 kandamizi.
Ni dhahiri rais wetu haioni hatari iliyoko mbele yetu endapo tutaingia katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 tukiwa na katiba hii hii na tukiwa na tume hii hii ya uchaguzi.
Nilieleza wiki iliyopita kwamba yaliyotokea katika uchaguzi wa Oktoba 31 ni maandiko tosha ukutani yanayoashiria mambo mabaya zaidi kwenye chaguzi zijazo kama mabadiliko hayatafanyika ya kuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Kauli tata iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi (JWTZ), Luteni Jenerali Shimbo, siku chache kabla ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, madai kwamba Usalama wa Taifa ulishirikishwa kwenye uchakachuaji wa kura na madai kwamba huko Kagera polisi waliwapiga wananchi mabomu ya kutoa machozi ili kujenga mazingira ya kuchakachua kura, si viashiria vyema kwa taifa lililopania kulinda amani na usalama wake.
Tungekuwa na viongozi visionary, wangeliona kwamba wananchi wameshaanza kupoteza imani na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tuliyonayo sasa. Wangeliona pia kwamba wananchi hawaridhiki na Katiba yetu ya tangu Uhuru na wanataka mpya.
Nisisitize tena kwamba tungelikuwa na viongozi visionary, wasingeendelea kutahadharisha tu kuhusu kupotea kwa amani na usalama; ilhali wanajua kwamba kuendelea kuwanyima Watanzania mabadiliko hayo (ya Katiba na Tume mpya ya uchaguzi), ni kupanda mbegu za kutowesha amani na utulivu huo ambao wameapa kuvilinda.
Nihitimishe kwa kusema kwamba kwa kuwa watawala wetu hawaioni hatari iliyoko mbeleni ya kuendelea kuwanyima Watanzania mabadiliko hayo, umma uchukue jukumu la kuwashinikiza (kwa njia za amani) kuleta mabadiliko hayo ili kuiepusha nchi yetu na vurugu zozote zinazoweza kusababisha umwagaji damu.
Ni rai yangu, hivyo basi, kwa Watanzania wote, wabunge, wanasiasa, waandishi wote wa habari, asasi zote sisizo za kiserikali zinazopigania haki za binadamu n.k, na kwa kushirikiana na wahisani wetu wa kigeni tuunganishe nguvu kuyadai mabadiliko haya muhimu ya kidemokrasia kutoka kwa watawala wetu.
Ni jambo la kutia moyo kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania, Jaji Kiongozi Mstaafu, Amiri Manento, aliwasha moto wa aina hiyo wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa haki za binadamu na Utawala Bora, Jaji Manento alisema hivi: Ni vyema Watanzania wote sasa tukaamka na kusema tunataka Katiba mpya.
Mimi nakubalina kabisa na Jaji Manento kwamba wakati umefika Watanzania tuamke na kudai mabadiliko hayo muhimu ya kidemokrasia, na ndiyo maana napendekeza mwaka ujao wa 2011 wimbo uwe mmoja tu: Katiba mpya, Tume mpya!