Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Nafikiri anavyofanya Mkapa hatofautiani na viongozi wengi duniani yaani kuwa muwazi anapotoka madarakani angalia kina Colin Powell na Condoleezza Rice walivyomgeuka Bush kuhusu vita vya Irak.
 
BWM umekosa mvuto umegundua dawa ni kurudi kwa wananchi. Shame on you. Isingekuwa kupora Kiwira ningekusamehe lakini kwa sasa sitoi msamaha labda nione unakunywa chai na Lissu
 
hilo la mahakama ya kadhi kuwa kwenye katiba, Mkapa anachezea amani ya nchi yetu!

Kwa washabiki wa katiba mpya mnapaswa kujiandaa na haya pia maana ukishafungua mlango mengi yatatoka na mengi yataingia.......mazuri na mabaya, ya amani na hatari, ya upendo na chuki......
 
Nafikiri anavyofanya Mkapa hatofautiani na viongozi wengi duniani yaani kuwa muwazi anapotoka madarakani angalia kina Colin Powell na Condoleezza Rice walivyomgeuka Bush kuhusu vita vya Irak.


Unapokuwa madarakani unachoengea kinakuwa ni sera na kwa kawaida sera ni lazima kuwe na makubaliano wa wote mlio madarakani....unapokuwa mstaafu unachoongea ni maoni yako na yana haki na wajibu sawa na maoni ya raia mwengine yoyote ingawa yanaweza kutofautiana kwa uzito wake.....
 
Kwa washabiki wa katiba mpya mnapaswa kujiandaa na haya pia maana ukishafungua mlango mengi yatatoka na mengi yataingia.......mazuri na mabaya, ya amani na hatari, ya upendo na chuki......

Wewe hushabikii Katiba Mpya?
 
Wakati wa utawala wake, siyo kwamba Mkapa hakujua kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na katiba mpya, bali kutokuwepo kwa katiba mpya hakukumpa taabu yeye kutawala. Kulikuwa na watu na viongozi wachache wa siasa na wasomi waliowahi kutamka kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na katiba mpya lakini haikuonekana wazi kuwa umma wa Watanzania ulikuwa unahitaji katiba mpya. Na hapa ndipo ambapo tunaona kazi kubwa aliyoifanya Dr. Slaa ukilinganisha na viongozi wenzie wa vyama vya siasa kama akina Prof. Lipumba, Mbatia, Mtikila, n.k. Dr. Slaa imeiondoa agenda ya katiba kutoka kuwa ya watu wachache na kuifanya kuwa ni hitaji la umma wa Watanzania, ikishafikia hapo hakuna mtu anayeweza kuzuia, lazima katiba mpya itapatikana, tena ikiwa na yale wanayoyataka Watanzania. Jukumu letu kubwa ni kuwaunganisha Watanzania wote ili kulifanya kuwa ni hitaji muhimu la kwanza, na yeyote ambaye anapinga, au kuzuia kwa namna yoyote ile tumfanye kuwa ni adui wa Watanzania wote.
 
Kwa washabiki wa katiba mpya mnapaswa kujiandaa na haya pia maana ukishafungua mlango mengi yatatoka na mengi yataingia.......mazuri na mabaya, ya amani na hatari, ya upendo na chuki......

Kilichokusukuma kuchangia hivi ni hilo suala la kadhi tu.....anyways,ila kadhi si jambo la hatari kiasi hicho
 
Kwenye bold umesema kweli suala likiondoka kuwa la kibnafsi na kuhamia kwa umma huwa ni kazi sana kulikwepa, kazi inayotakiwa sasa ni kuandaa vikundi kazi (task force) kama ilivyokuwa NCCR ya kabla ya vyama vingi 80s-90s ilivyo push kuwepo kwa vyama vingi. Hii kazi si ya kuachiwa mtu mmoja au chama kimoja, naelewa wapo wengi tu wanaotaka mabadiliko ya katiba hata humo CCM kwenyewe kinachotakiwa ni kuwa identify hao hasa watu wenye sauti kama huyu kama kina Warioba kuwaweka pamoja.

Mbali ya watu mashuhuri pia vikundi vingine muhimu ni vya dini tuwaendee viongozi hawa tusikie maoni yao juu ya katiba mimi ninahakika baada ya mwaka mmoja lazima kutakuwa na vuguvugu na changes zitaonekana.
 
Mkuu, it's so true kwamba "Time will tell." Lakini Louis-Hector Berlioz pia anatuonya kwamba, "Time is a great teacher, but unfortunately it kills all its pupils." Tangu mwaka 1992, miaka mingi imepita sasa. We don't have much time on our side kwakweli. Ndo' maana inabidi tufanye kila tuwezalo kuhakikisha kwamba hili suala la Katiba Mpya litafutiwa ufumbuzi mapema kabisa kabla kampeni za uchaguzi wa 2015 hazijaanza. Sign Petition here:TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
 
Ya katiba iko wapi tu sign? tupe link baba/mama
 
“Nadhani ni woga ambao hauna msingi wowote, [CCM/Serikali] wanahofia kile ambacho watu watapendekeza katika katiba mpya, lakini mimi naamini watu wakikaa chini na kutulia, hawawezi kuja na vitu vya ajabu" ~ Jaji Bomani (Dec, 2010)

 
Ndugu TRUTH, nadhani hatutofautiani sana katika hili la KITU GANI KIFANYIKE kwa sasa kuleta sauti za wadai-KATIBA-MPYA kwa pamoja.

Ikumbukwe kwamba hakuna mahala kumetajwa CDM kuunda KATIBA MPYA isipokua wazo iliotoka ni kwamba kuwepo na chombo fulani kinacholeta sauti hizo mbalimbali kwa pamoja ndipo kudai kule kwa KATIBA MPYA kuende vizuri zaidi.

Nadhani hupingani na ukweli kwamba sauti zikiendelea kujitokeza kila kona ya nchi lakini bila kuleta fikra zao kwa pamoja haina tofauti na kusema kwamba 'TUNAPIGA TU KELELE BARABARNI' kama ambavyo mama Kombani aliwahi kunukuliwa akisema. Hebu fikiria leo CHADEMA wamesema wataka Katiba Mpya na Tume Huru halafu wakabakia hapo, kesho Tanganyika Law Society wakasema serikali iharakishe juhudi halafu wakapumzika zao, kaja Mzee Mkapa na kuongeza muda ni mwafaka halafu ndio hivo, kesho kutwa yake Vijana tumesema hivi JF na majaji wastaafu nao wakasema kivyao na ....

Chombo cha kuratibu haya mawazo kwa pamoja ni muhimu sana. Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba chombo kama hicho kikishaundwa kwa ajili ya kudai hayo mambo ya msingi kwetu basi moja kwa moja kinakua ni chombo chetu sote kama taifa na wala si mali binafsi ya CHADEMA.

Tukumbuke; GOOD IDEAS NEVER STAND FOR THEMSELVES TO INTENDED FRUITATION UNLESS SOMEONE STANDS BY THEM AND FIGHTS FOR THEM round the clock (Ni ukweli usiopingika kwamba mawazo maridhawa kamwe hayawezi kuleta tija yoyote kwa kujitenga na waleta wazo wenyewe kuwa na utayari wa kuyatumikia hayo mawazo yao ili mafanikio yaweze kupatikana katika jamii.

Ni kweli kabisa kwamba unao haki na mawazo yako na ndio maana hoja huletwa hapa ili sote tukalijadili kwa pamoja na tuone njia gani ni sahihi zaidi kwetu. Lakini, waheshimiwa hivi kweli kwa mtindo huo ndio mambo yaendelee kweli????

Wana-JF, naomba mjadala uendelee kuhusu njia sahihi ya kufuata hadi sasa ili tukapate KATIBA MPYA na Tume huru ya Uchaguzi.
 

Excellent move, best idea, instead to wait hadi serikali ikubali, Chadema inatakiwa ianze mchakato, where constitution should be ammended, na wapi vitu vipya viongezwe, mapendekezo yao yawe kitaifa zaidi si kichama lakini, hii safffiiiiiiiiii, +ve keep going buddy
 

Hapa naona kuna mawazo mazuri Mheshimiwa Rais wangu. Ni vema kutoa mwanga zaidi CHADEMA kufanya nini na au wasifanye yepi kama ambavyo tayari wengi tumeanzo kuelezea. Isitoshe, CCM ilikua ikibana njia ya kuletwa mabadiliko ya kweli tunayotaka sisi vijana lakini kwa maneno ya Ndugu Wasira kwenye gazeti la 'Mwananchi' ni kwamba tayari wameachia.

Kwangu mimi nasema kwamba si lazima wanabadiliko kuendelea na ratiba ya hiyo serikali ya sisiem bali ni chombo kitakachoundwa kitaifa zaidi hicho ndio kitujumuishe sote na kutuongoza katika hili.

Pia, chombo hiki kisisahau kuwaalika CCM na serikali kwenye mchakato kwani hivyo vyombo viwili navyo ni washikadau katika taifa letu wenye maslahi katika KATIBA MPYA na Tume Huru ya Uchaguzi sawa sawa na wadau wengine tu !!!
 
CCK yajiunga kilio cha katiba


Na Zamzam Abdul

CHAMA Cha Kijamii (CCK), kimeandaa waraka ambao utachambua kasoro zilizopo kwenye katiba na kuzifikisha kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Celina Kombani ili aweze kutoa hoja rasmi kwa nini Tanzania inahitaji katiba mpya.Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa
Taifa wa chama hicho, Bw. Constantine Akitanda, alisema matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita, yalitokana na kasoro zilizopo kwenye katiba ambayo inatumika hivi sasa.

“Mambo mengi ambayo tumeyaona kuanzia muundo wa tume, usimamizi wa uchaguzi na utangazaji matokeo, yanahitaji kuangaliwa upya, haya yote yanaweza kusahihishwa na kutengenezwa vizuri kama katiba yetu itafanyiwa maboresho na kuandaliwa upya,” alisema.

Alisema chama hicho kipo mbioni kufanikisha lengo lake la kupata usajili wa kudumu ili kiweze kutoa mchango wa kifikra na kiuongozi nchini.

“Tumejipanga vizuri na tunaendelea kuwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili kuhakikisha tunapata usajili wa kudumu, wanachama wapya pamoja na ofisi,” 'alisema Bw. Akitanda.

Amewataka wanachama wa chama hicho, kutoa ushirikiano wakati wote wa uhakiki ili usaili huo usikumbwe na matatizo yasiyokuwa ya lazima.
Alisema mbali ya kusubili mchakato wa kupata usajili, chama hicho kitaendelea kupiga vita vitendo vya ufisadi ambavyo bado vimekithiri nchini.
Bw. Akitanda alisema mfumo wa uchaguzi haukidhi mahitaji ya Taifa kuanzia uandikishaji, kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

Msimamo wa chama hicho umekuja baada ya Bi. Kombani kusema kuwa hakuna haja ya kubadilisha katiba iliyopo kwa kuwa hakuna chama au kundi la watu ambalo limetoa madai rasmi ya kutaka katiba mpya.
 
CCK??....CCJ??...I get a cofusion!

Kwahiyo shida ni hiyo tu, ya kukosekana kwa kundi la kijamii lililopeleka rasmi hoja ya kudai katiba mpya!!
Kama ni hiyo, basi we are just around the corner bringing the stuff!
 
Mwandishi kapotosha habari na Mhariri alikuwa anasinzia.

Bi. Kombani hakusema hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…