Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Mkuu huyu jamaa tuombe tu siku moja akubali watu watoe maoni yao mbele yake ndio atajaua hasira zetu. Aliichukua nchi kwenye hali mbali akabadilisha na kuifanya iwe decent kidogo, then katika siku za mwisho akaanza kuivuruga na kuitupa kabisa jalalani. The mess that we are in is mainly because of him, he knew waht was Tanzania going to face before he left the office and he kept quite and even blessed it.

Even worse alijua kabisa kuwa katiaba yetu famba halafu akaiacha famba bila hata kufanya effort ya kuibadilisha, then leo anasema hivyo, so pathetic.
Nafikiri anavyofanya Mkapa hatofautiani na viongozi wengi duniani yaani kuwa muwazi anapotoka madarakani angalia kina Colin Powell na Condoleezza Rice walivyomgeuka Bush kuhusu vita vya Irak.
 
BWM umekosa mvuto umegundua dawa ni kurudi kwa wananchi. Shame on you. Isingekuwa kupora Kiwira ningekusamehe lakini kwa sasa sitoi msamaha labda nione unakunywa chai na Lissu
 
hilo la mahakama ya kadhi kuwa kwenye katiba, Mkapa anachezea amani ya nchi yetu!

Kwa washabiki wa katiba mpya mnapaswa kujiandaa na haya pia maana ukishafungua mlango mengi yatatoka na mengi yataingia.......mazuri na mabaya, ya amani na hatari, ya upendo na chuki......
 
Nafikiri anavyofanya Mkapa hatofautiani na viongozi wengi duniani yaani kuwa muwazi anapotoka madarakani angalia kina Colin Powell na Condoleezza Rice walivyomgeuka Bush kuhusu vita vya Irak.


Unapokuwa madarakani unachoengea kinakuwa ni sera na kwa kawaida sera ni lazima kuwe na makubaliano wa wote mlio madarakani....unapokuwa mstaafu unachoongea ni maoni yako na yana haki na wajibu sawa na maoni ya raia mwengine yoyote ingawa yanaweza kutofautiana kwa uzito wake.....
 
Kwa washabiki wa katiba mpya mnapaswa kujiandaa na haya pia maana ukishafungua mlango mengi yatatoka na mengi yataingia.......mazuri na mabaya, ya amani na hatari, ya upendo na chuki......

Wewe hushabikii Katiba Mpya?
 
Wakati wa utawala wake, siyo kwamba Mkapa hakujua kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na katiba mpya, bali kutokuwepo kwa katiba mpya hakukumpa taabu yeye kutawala. Kulikuwa na watu na viongozi wachache wa siasa na wasomi waliowahi kutamka kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na katiba mpya lakini haikuonekana wazi kuwa umma wa Watanzania ulikuwa unahitaji katiba mpya. Na hapa ndipo ambapo tunaona kazi kubwa aliyoifanya Dr. Slaa ukilinganisha na viongozi wenzie wa vyama vya siasa kama akina Prof. Lipumba, Mbatia, Mtikila, n.k. Dr. Slaa imeiondoa agenda ya katiba kutoka kuwa ya watu wachache na kuifanya kuwa ni hitaji la umma wa Watanzania, ikishafikia hapo hakuna mtu anayeweza kuzuia, lazima katiba mpya itapatikana, tena ikiwa na yale wanayoyataka Watanzania. Jukumu letu kubwa ni kuwaunganisha Watanzania wote ili kulifanya kuwa ni hitaji muhimu la kwanza, na yeyote ambaye anapinga, au kuzuia kwa namna yoyote ile tumfanye kuwa ni adui wa Watanzania wote.
 
Kwa washabiki wa katiba mpya mnapaswa kujiandaa na haya pia maana ukishafungua mlango mengi yatatoka na mengi yataingia.......mazuri na mabaya, ya amani na hatari, ya upendo na chuki......

Kilichokusukuma kuchangia hivi ni hilo suala la kadhi tu.....anyways,ila kadhi si jambo la hatari kiasi hicho
 
Wakati wa utawala wake, siyo kwamba Mkapa hakujua kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na katiba mpya, bali kutokuwepo kwa katiba mpya hakukumpa taabu yeye kutawala. Kulikuwa na watu na viongozi wachache wa siasa na wasomi waliowahi kutamka kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na katiba mpya lakini haikuonekana wazi kuwa umma wa Watanzania ulikuwa unahitaji katiba mpya. Na hapa ndipo ambapo tunaona kazi kubwa aliyoifanya Dr. Slaa ukilinganisha na viongozi wenzie wa vyama vya siasa kama akina Prof. Lipumba, Mbatia, Mtikila, n.k. Dr. Slaa imeiondoa agenda ya katiba kutoka kuwa ya watu wachache na kuifanya kuwa ni hitaji la umma wa Watanzania, ikishafikia hapo hakuna mtu anayeweza kuzuia, lazima katiba mpya itapatikana, tena ikiwa na yale wanayoyataka Watanzania. Jukumu letu kubwa ni kuwaunganisha Watanzania wote ili kulifanya kuwa ni hitaji muhimu la kwanza, na yeyote ambaye anapinga, au kuzuia kwa namna yoyote ile tumfanye kuwa ni adui wa Watanzania wote.
Kwenye bold umesema kweli suala likiondoka kuwa la kibnafsi na kuhamia kwa umma huwa ni kazi sana kulikwepa, kazi inayotakiwa sasa ni kuandaa vikundi kazi (task force) kama ilivyokuwa NCCR ya kabla ya vyama vingi 80s-90s ilivyo push kuwepo kwa vyama vingi. Hii kazi si ya kuachiwa mtu mmoja au chama kimoja, naelewa wapo wengi tu wanaotaka mabadiliko ya katiba hata humo CCM kwenyewe kinachotakiwa ni kuwa identify hao hasa watu wenye sauti kama huyu kama kina Warioba kuwaweka pamoja.

Mbali ya watu mashuhuri pia vikundi vingine muhimu ni vya dini tuwaendee viongozi hawa tusikie maoni yao juu ya katiba mimi ninahakika baada ya mwaka mmoja lazima kutakuwa na vuguvugu na changes zitaonekana.
 
Nimeoteshwa kuwa kuna katiba mpya soon..........viashiria hivyi hapa

  • JK ni mtu wa kupenda kusifiwa
  • Kuna presha inatengenezwa na wasaidizi watu wa kimaendeleo
  • CHADEMA umakini wao umestua wengi hasa wawekezaji
  • turn out ya 2010 imestua watu hata wale wasiopenda kuiona. Achaneni na Celina, ni mshabiki huyu.
Mikutano ya kampeni na tukio la juzi la kuwalk out na habari zake jinsi zilivozungumza zimeamsha watu. Mimi naiona hiyooooooo.

Time will tell.
Mkuu, it's so true kwamba "Time will tell." Lakini Louis-Hector Berlioz pia anatuonya kwamba, "Time is a great teacher, but unfortunately it kills all its pupils." Tangu mwaka 1992, miaka mingi imepita sasa. We don't have much time on our side kwakweli. Ndo' maana inabidi tufanye kila tuwezalo kuhakikisha kwamba hili suala la Katiba Mpya litafutiwa ufumbuzi mapema kabisa kabla kampeni za uchaguzi wa 2015 hazijaanza. Sign Petition here:TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
 
Hujakosea. Kuna Petition mbili zenye malengo tofauti. Petition ya jana yenye watu zaidi ya 100+, inahusu kuishinikiza serikali kuwekeza kwenye mradi wa umeme wa Stieglers Gorge. Petition yenyewe inapatikana hapa:TATIZO LA UMEME: TUPATIENI 'STIEGLERS GORGE' Petition

Hii ya leo ni kwa ajiri ya mambo ya Katiba tu. Sijui kama nimejibu swali lako mkuu?
Ya katiba iko wapi tu sign? tupe link baba/mama
 
“Nadhani ni woga ambao hauna msingi wowote, [CCM/Serikali] wanahofia kile ambacho watu watapendekeza katika katiba mpya, lakini mimi naamini watu wakikaa chini na kutulia, hawawezi kuja na vitu vya ajabu" ~ Jaji Bomani (Dec, 2010)

Jaji Bomani: Mabadiliko ya [Katiba] tishio kwa CCM
Saturday, 04 December 2010 22:48 Claud Mshana, Mwananchi

SIKU chache baada ya Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Cellina Kambani kuseam hakuna haja ya kuwa na katiba moya, Jaji Mkuu Mstaafu, Mark Bomani amesema kinachoisumbua serikali ya CCM ni uwoga ambao hauna msingi wowote. Katiba inyotumiwa hivi sasa, kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati na inakinzana yenyewe katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora. Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani wiki hii alikaririwa na vyombo vya habari akisema suala la kuunda katiba mpya haliwezekani kwa kuwa serikali haina fedha na kwamba itaendelea na utaratibu uliozoeleka wa kufanya marekebisho ya katiba pale inapohitajika.

Jaji Bomani alisema kinachotakiwa hivi sasa ni kufanyika kwa mapitio ya kina ya katiba iliyopo na kuainisha upungufu wote, kisha kufanya mabadiliko kwa mujibu wa mahitaji. “Nadhani ni woga ambao hauna msingi wowote, wanahofia kile ambacho watu watapendekeza katika katiba mpya, lakini mimi naamini watu wakikaa chini na kutulia, hawawezi kuja na vitu vya ajabu," alisema Jaji Bomani.

Madai ya serikali ya CCM kuhofia kitakachofuata baada ya kupatikana kwa katiba mpya, pia yalitolewa na Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Mujwahuzi Njunwa, ambaye aliongeza kuwa hata CCM kama wakija kushindwa katika uchaguzi mkuu, watakuwa mstari wa mbele kudai mabadiliko ya katiba. “Hii ni tabia ya watawala wengi, kuwa na woga na kutokukubali mabadiliko, jambo hili linatoa picha kuwa serikali haipo kwa maslahi ya wananchi na taifa,” alisema Profesa Njunwa.

Hata hivyo, akizungumzia hoja ya matumizi ya nguvu ya umma iliyotolewa na Chadema hivi karibuni, iwapo CCM watagoma kusikiliza hoja za mabadiliko ya katiba, Profesa Njunwa alisema serikali haiwezi kungojea hali hiyo itokee. “CCM wanabusara, hawatapenda kuona nchi ikiingia katika matatizo, nina uhakika hivi sasa wanaangalia upepo unavyovuma na kasi ya watu kudai katiba mpya,” alifafanua Profesa Njunwa. Jaji Bomani ambaye aliwahi pia kuwa Mwanasheria wa serikali, aliishauri serikali kuunda jopo la wataalam kutoka sekta mbalimbali watakao pitia sheria iliyopo na kuja na mapendekezo ya kuwa na katiba mpya, jambo ambalo alisema litamaliza mvutano uliopo. Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM katika Bunge lililopita, Aloyce Kimaro alisema ni vema serikali ikapewa muda wa kujipanga, lakini alisema kuna ulazima wa kuwa na mabadiliko kwa katiba. “Hakuna nafasi kwa serikali kutosikia, na kama wataziba masikio, wananchi watawalazimisha kusikia. Lazima kuwe na mfumo unaoleweka, hizi si zama za watu wachache kuamua juu ya mambo ya nchi,” alisema Kimaro. Utata wa katiba.

Naye Mhadhiri wa Kitivo cha sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina alipozungumza na Mwananchi Jumapili, alifafanua kwa kina baadhi ya maeneo yenye utata katika katiba iliyopo. Profesa Maina alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili, serikali mbili na katiba mbili, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984. Alisema kwamba hivi sasa kuna kero nyingi za muungano. “Tunaweka vyombo visivyo vya kikatiba kuyashughulikia mambo haya mazito,ukiangalia kamati ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kamati hii haina chanzo chake kwenye Katiba wala sheria yoyote ile. Hivyo uhai wa Kamati hii haufahamiki, kwa mfano kwa sasa Zanzibar haina Waziri Kiongozi kikatiba ni nani anawakilisha Zanzibar katika Kamati hiyo, Makamu wa Kwanza au wa Pili wa Rais au ndiyo imekufa?,” alihoji Profesa Maina na kuongeza:

“Hivi karibuni Katiba ya Zanzibar ilifanyiwa mabadiliko ya Kumi ya mwaka 2010, mabadiliko haya yakaanzisha Serikali ya umoja wa Kitaifa. Mabadiliko haya yapo tofauti kabisa na serikali ya Zanzibar inavyoelezwa katika sura ya nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Sura hii ina Sehemu Tatu, inahusu Serikali ya Mapinduzi na Rais wa Zanzibar; Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi – Ibara ya 102 hadi 207). Hivyo, Katiba hizi mbili zinaongea vitu viwili tofauti na hivyo kuchanganya wananchi”.

Maina alitaja mgongano mwingine wa kisheria katika katiba iliyopo ni mabadiliko ya kumi yaliyofanywa katika katiba ya Zanzibar.

Katika mabadiliko hayo, Mahakama ya Rufaa imeondelewa uwezo, lakini mahakama hiyo ilianzishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kutangazwa kuwa ni chombo cha muungano (Union Matter).

“Pia mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar yamevichanganya vyama vya siasa. Kwa mfano, Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande mmoja (Zanzibar) ni sehemu ya utawala kama mshirika katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Lakini, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kinataka kiwe sehemu ya upinzani dhidi ya chama tawala ambacho ni mshirika wake huko Zanzibar”.

Kwa mujibu wa Prof Maina, kuna Ibara na vifungu kadhaa vimefutwa katika katiba zote mbili na kuachwa hivi hivi.

“Angalia kwa mfano Ibara ya 10; 80; 82 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano; na Vifungu 98; 102A; 103 vya Katiba ya Zanzibar. Vile vile, kuna vifungu vya Katiba ambavyo havitumiki na haviwezi kutumika katika hali halisi ya nchi yetu,” alisema Prof Maina. Pia alitoa mfano wa sehemu inayohusu Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo wanaoweza kushtakiana ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano tu (Sehemu ya Saba ya Sura ya Tano ya Katiba – Ibara ya 125 hadi 128) na kuangaliza kuwa katiba ya nchi haitakiwi iwe hivyo.

“Hivyo, kuna haja ya kuachana na mabadiliko na kutafuta utaratibu wa kutafuta Katiba zilizo bora kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano,” alishauri.

Katika juhudi za kupata katiba mpya Mwaka 1991, Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa vyama vingi vya siasa, na kupendekeza kuwepo kwa katiba mpya na si kurithi katiba ya chama kimoja ambayo muhimili wake ulikuwa tofauti. Hoja hizo hazikupewa majibu na vyama vingi vya siasa viliingizwa ndani ya katiba ya mwaka 1977, kupitia mabadiliko ya Nane ya mwaka 1992, yaliyotungiwa Sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya 1992. “Mwaka 1998 Kamati ya White Paper ilipoundwa chini ya Jaji wa Mstaafu wa Rufani Robert Kisanga pia ilipendekeza umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Lakini kamati hiyo ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa eti imevuka mipaka yake kwa sababu ilikuwa Kamati na siyo Tume.
 
Ndugu TRUTH, nadhani hatutofautiani sana katika hili la KITU GANI KIFANYIKE kwa sasa kuleta sauti za wadai-KATIBA-MPYA kwa pamoja.

Ikumbukwe kwamba hakuna mahala kumetajwa CDM kuunda KATIBA MPYA isipokua wazo iliotoka ni kwamba kuwepo na chombo fulani kinacholeta sauti hizo mbalimbali kwa pamoja ndipo kudai kule kwa KATIBA MPYA kuende vizuri zaidi.

Nadhani hupingani na ukweli kwamba sauti zikiendelea kujitokeza kila kona ya nchi lakini bila kuleta fikra zao kwa pamoja haina tofauti na kusema kwamba 'TUNAPIGA TU KELELE BARABARNI' kama ambavyo mama Kombani aliwahi kunukuliwa akisema. Hebu fikiria leo CHADEMA wamesema wataka Katiba Mpya na Tume Huru halafu wakabakia hapo, kesho Tanganyika Law Society wakasema serikali iharakishe juhudi halafu wakapumzika zao, kaja Mzee Mkapa na kuongeza muda ni mwafaka halafu ndio hivo, kesho kutwa yake Vijana tumesema hivi JF na majaji wastaafu nao wakasema kivyao na ....

Chombo cha kuratibu haya mawazo kwa pamoja ni muhimu sana. Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba chombo kama hicho kikishaundwa kwa ajili ya kudai hayo mambo ya msingi kwetu basi moja kwa moja kinakua ni chombo chetu sote kama taifa na wala si mali binafsi ya CHADEMA.

Tukumbuke; GOOD IDEAS NEVER STAND FOR THEMSELVES TO INTENDED FRUITATION UNLESS SOMEONE STANDS BY THEM AND FIGHTS FOR THEM round the clock (Ni ukweli usiopingika kwamba mawazo maridhawa kamwe hayawezi kuleta tija yoyote kwa kujitenga na waleta wazo wenyewe kuwa na utayari wa kuyatumikia hayo mawazo yao ili mafanikio yaweze kupatikana katika jamii.

Ni kweli kabisa kwamba unao haki na mawazo yako na ndio maana hoja huletwa hapa ili sote tukalijadili kwa pamoja na tuone njia gani ni sahihi zaidi kwetu. Lakini, waheshimiwa hivi kweli kwa mtindo huo ndio mambo yaendelee kweli????

Wana-JF, naomba mjadala uendelee kuhusu njia sahihi ya kufuata hadi sasa ili tukapate KATIBA MPYA na Tume huru ya Uchaguzi.
 
Ni kweli hamasa ya CHADEMA kwa Wananchi kudai (1) Katiba Mpya na (2) Tume Huru ya Uchaguzi umeshika kasi ajabu miongoni mwetu wananchi. Wengi zaidi sasa hujitokeza hadharani, bila woga wala kificho kudai kilicho chao.

Lakini sasa kadri sauti hizo zinavyoendelea kuongezeka, ni vema CHADEMA kuendelea kuziratibu kwa kasi hiyo hiyo ili tusije tukawacheleweshia wananchi MABADILIKO YA KWELI wanayoihitaji hivi sasa.

Kwa mantiki hiyo, CHADEMA anzeni kuratibu sauti mbalimbali ambazo zinaendelea kujitokeza kwa sasa na kukubaliana zaidi na madai yetu ya ya MSINGI juu ya kudai kuandikwa upya KATIBA MPYA na kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Mara baada ya kuratibu sauti hizo mbali mbali, undeni National Constitutional Assembly of Tanzania (NACAT). Kazi ya kwanza ya hiki chombo cha NACAT ni kwamba watoe RATIBA KAMILIFU inayoonyesha mambo gani yatafanyika lini, na kitengo gani chini yake ili kazi ya kuandika upya (1) KATIBA, (2) kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na pia (3) kutunga sheria mbalimbali walau miaka miwili kabla ya 2015, tayari kwa uchaguzi mkuu wa wakati huo.

Excellent move, best idea, instead to wait hadi serikali ikubali, Chadema inatakiwa ianze mchakato, where constitution should be ammended, na wapi vitu vipya viongezwe, mapendekezo yao yawe kitaifa zaidi si kichama lakini, hii safffiiiiiiiiii, +ve keep going buddy
 
Excellent move, best idea, instead to wait hadi serikali ikubali, Chadema inatakiwa ianze mchakato, where constitution should be ammended, na wapi vitu vipya viongezwe, mapendekezo yao yawe kitaifa zaidi si kichama lakini, hii safffiiiiiiiiii, +ve keep going buddy

Hapa naona kuna mawazo mazuri Mheshimiwa Rais wangu. Ni vema kutoa mwanga zaidi CHADEMA kufanya nini na au wasifanye yepi kama ambavyo tayari wengi tumeanzo kuelezea. Isitoshe, CCM ilikua ikibana njia ya kuletwa mabadiliko ya kweli tunayotaka sisi vijana lakini kwa maneno ya Ndugu Wasira kwenye gazeti la 'Mwananchi' ni kwamba tayari wameachia.

Kwangu mimi nasema kwamba si lazima wanabadiliko kuendelea na ratiba ya hiyo serikali ya sisiem bali ni chombo kitakachoundwa kitaifa zaidi hicho ndio kitujumuishe sote na kutuongoza katika hili.

Pia, chombo hiki kisisahau kuwaalika CCM na serikali kwenye mchakato kwani hivyo vyombo viwili navyo ni washikadau katika taifa letu wenye maslahi katika KATIBA MPYA na Tume Huru ya Uchaguzi sawa sawa na wadau wengine tu !!!
 
CCK yajiunga kilio cha katiba


Na Zamzam Abdul

CHAMA Cha Kijamii (CCK), kimeandaa waraka ambao utachambua kasoro zilizopo kwenye katiba na kuzifikisha kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Celina Kombani ili aweze kutoa hoja rasmi kwa nini Tanzania inahitaji katiba mpya.Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa
Taifa wa chama hicho, Bw. Constantine Akitanda, alisema matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita, yalitokana na kasoro zilizopo kwenye katiba ambayo inatumika hivi sasa.

“Mambo mengi ambayo tumeyaona kuanzia muundo wa tume, usimamizi wa uchaguzi na utangazaji matokeo, yanahitaji kuangaliwa upya, haya yote yanaweza kusahihishwa na kutengenezwa vizuri kama katiba yetu itafanyiwa maboresho na kuandaliwa upya,” alisema.

Alisema chama hicho kipo mbioni kufanikisha lengo lake la kupata usajili wa kudumu ili kiweze kutoa mchango wa kifikra na kiuongozi nchini.

“Tumejipanga vizuri na tunaendelea kuwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili kuhakikisha tunapata usajili wa kudumu, wanachama wapya pamoja na ofisi,” 'alisema Bw. Akitanda.

Amewataka wanachama wa chama hicho, kutoa ushirikiano wakati wote wa uhakiki ili usaili huo usikumbwe na matatizo yasiyokuwa ya lazima.
Alisema mbali ya kusubili mchakato wa kupata usajili, chama hicho kitaendelea kupiga vita vitendo vya ufisadi ambavyo bado vimekithiri nchini.
Bw. Akitanda alisema mfumo wa uchaguzi haukidhi mahitaji ya Taifa kuanzia uandikishaji, kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

Msimamo wa chama hicho umekuja baada ya Bi. Kombani kusema kuwa hakuna haja ya kubadilisha katiba iliyopo kwa kuwa hakuna chama au kundi la watu ambalo limetoa madai rasmi ya kutaka katiba mpya.
 
CCK??....CCJ??...I get a cofusion!

Kwahiyo shida ni hiyo tu, ya kukosekana kwa kundi la kijamii lililopeleka rasmi hoja ya kudai katiba mpya!!
Kama ni hiyo, basi we are just around the corner bringing the stuff!
 
Mwandishi kapotosha habari na Mhariri alikuwa anasinzia.

Bi. Kombani hakusema hivyo.
 
Back
Top Bottom