Sidanganyiki - Leo ndio mnajua Tanzania inahitaji katiba mpya? Mambo mengine yanashangaza sana; leo kila mmoja wa watu mashuhuri anatafuta gia ya "kutokea"; mwisho Rais na wajumbe wa Kamati Kuu nao watakuja na kusema "wanataka Katiba Mpya". Nimekaa naangalia wanaojitokeza kudai katiba mpya na wanaripotiwa huku wakibeba ujiko wa ofisi na vyeo vyao; ati kuanzia Mkapa na sasa Jaji Mkuu na wote wengine katikati yao ati wote sasa "wanataka Katiba Mpya"! Really? Why?Ati leo viongozi wa dini nao wanajitokeza na kudai Katiba Mpya! Mwisho wataanza kuja na wabunge wa CCM wakidai Katiba Mpya! Utani mwingine jamani!Katiba Mpya? Kwani hii iliyopo imegunduliwa ina matatizo gani ambayo hawakuyaona miaka 20 iliyopita? Kwamba mwaka 2010 ndio wamegundua kuwa Katiba ina matatizo? Naam, watasema imejulikana kuanzia 1992. Watasema kuwa miaka yote hii kumekuwa na "kilio" cha Katiba Mpya na wengine watatuambia jinsi walivyojaribu kuzungumzia hili miaka yote hii wakituambia juu ya Ripoti ya Nyalali n.k Lakini miaka yote hiyo hawakujitokeza hawa kwa nguvu hivi kudai "katiba mpya". Lakini cha kuudhi na ambacho naamini ni cha uzugaji uliokubuhu ni kuwa wote hawa hawakuwa na ujasiri wa kudai Katiba Mpya kabla ya uchaguzi. Tangu 2005 hadi ulipofika uchaguzi huu wengi tumeandika na wengine wamelalamikia matatizo mbalimbali. Suala la ubovu wa tume ya uchaguzi halikuibuliwa kwenye uchaguzi wa 2010; wengine tulishabeza wapinzani kwenda kwenye uchaguzi huu uliopita wakiwa na tume ile ile na mfumo ule ule na tukasema mapema wasije kulalamika "tume ya uchaguzi, tume ya uchaguzi". Tulisema wamekubali kucheza kwa kanuni za mchezo na refa ambaye tayari alishajionesha kuwa ana upendeleo akiwavuruga wasilalamike. Sijui walisahau wapi yaliyotokea Kiteto? Walisahau vipi yaliyotokea Tunduru?Lakini sasa siyo wapinzani tu hata viongozi wengine wa serikali na hata wa CCM wanaanza kudai Katiba Mpya. Kilichonishangaza ni kuwa Rais Mkapa anadai naye Katiba Mpya! Really? I mean Really? Alikuwa Rais kwa miaka 10; alisimamia mabadiliko ya Katiba ya 2005 - lakini hakutaka Katiba mpya then? Lakini wote hawa wanaojitokeza kudai Katiba Mpya hawataki kusema kitu kilichowazi; Hawataki kusema hasa kwanini sasa baada ya uchaguzi wamepata ujasiri wa kudai Katiba Mpya. Walijua sheria ya uchaguzi, walijua mfumo wa tume ya uchaguzi; walijua malalamiko ya Katiba mpya lakini kwa miaka karibu ishirini walikaa kimya. Lakini sasa kuna kitu kimetokea; kitu ambacho hawana ujasiri wa kukisema au kukiita kwa jina lake. Hoja ya kuandika upya katiba haiwezi kunogeshwa kwa kutokuwa tayari kuita ukweli kwa jina lake. Ni nini kilitokea baada ya uchaguzi; au swali sahihi zaidi ni nini kilitokea wakati wa uchaguzi ambacho kimewafanya watu waamke na kudai Katiba Mpya. Wakiseme kwanza na waseme wasimung'unye maneno; vinginevyo wapo ambao watawasaidia kukisema hicho kinachofanya hoja ya Katiba Mpya iwe na nguvu sasa kuliko 1992. Dare to say it otherwise.. naomba tuachane na hoja ya Katiba Mpya hadi tutakapokuwa tayari kusema hasa ni kwanini tunataka Katiba Mpya hasa baada ya uchaguzi wa 2010.
MS nadhani wewe tatizo lako ni moja tu - Unatafasiri kila kitu ktk mtazamao wa dini jambo ambalo si sahihi.
Pamoja na hayo post yako hapo juu ina maswali ya msingi na ningeomba uone hoja unazopewa na wanaJF.
Unajua pia lazima ukubali kwamba huwa kuna majira na nyakati kwa kila kitu. Sasa wewe ukishupaza shingo kinyume na majira basi utaumia bila shaka. Hata katika maisha ya kawaida kuna mabadiliko tunayafanya ili kuitikia matakwa ya wakati.
Kama utakumbuka wakati Tritel na Mobitel zimeingia simu ya mkononi ilionekana ya watu wenye fedha tu and my friend kama una Mobitel lako (Kuuuuubwa) ukapanda daladala watu wangekushangaa maana walijiuliza kwa nini usipande Taxi!!! Sasa jiulize why do you have a mobile phone now and not then..?? Nyakati zimetusukuma kaka and whoever is shouting is simply responding to that force!!
Kitu cha pili joto la kisiasa lililopo sasa huwezi kulifananisha na wakati wowote kati ya 1995 na 2005. Ukiangalia hakuna wakati watanzania wamefuatilia kwa karibu siasa za nchi kama uchaguzi 2010, mikutano ya Lipumba na Slaa imetuonyesha hilo. Cheyo na Lipumba ni kweli waliwahi kulalamikia kuibiwa kura lakini kipindi hicho hatukujua ni kwa kiwango gani siasa zinaathiri maisha yetu ya kila siku. Leo hii najua ni siasa kwa sababu kitoweo nilichohifadhi kwa taabu kwenye kafriji kangu toka China kimeoza sababu ya Tanesco=Richmond,IPTL,Dowans.
Wewe ni shahidi kuwa CUF na CDM wagombea wao kibao ushindi wao umechakachuliwa (mikoa ya Lindi, Shinyanga, Rukwa, Iringa, Pwani, Kagera n.k) na wananchi wamejua wameibiwa ndio maana wengi wameamu wasisubiri mahubiri ya 2015 ni bora vita vianze asubuhi.
Kwa hiyo wewe usijali nani anaongea cha msingi tuangalie kama kuna mantiki katika wanachosema.
Nashawishika kuwa this time around KATIBA itapatikana kwa sababu kuu zifuatazo (baadhi tu):
1. Kikwete hana cha kupoteza kutokana na mabadiliko yoyote
2. Nobody can swim against this wave (katiba mpya) hata JK anajua
3. Kikwete anataka akumbukwe na hakuna kitakachomfanya akumbukwe zaidi ya hili
4. Nadhani atapenda awe kwenye orodha ya Mo Ibrahim ambayo kina Mkapa wameikosa- $5m si mchezo
So MS welcome aboard!!!!!!