Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Katiba iliyopo iliandaliwa chini ya utawala wa Rais Nyerere ambaye ni mkristo tangu mwaka 1977 ambapo marais wote waliofuata Waislamu kwa Wakristo wamekuwa wanaifanyia marekebisho ambayo naamini hayakufanywa kwa misingi ya kulinda dini moja dhidi ya nyingine. Kelele za katiba mpya, kama ingekuwa ni uchambuzi wa fikra mgando basi wengi tungefikiri kwamba mawazo ya nyerere ndani ya katiba yameondolewa kwa njia ya kuirekebisha mara 14 tangu utawala wa awamu ya kwanza.

Wakati katiba hii inaanzishwa mwaka 1977 Rais Kikwete alikuwa ana miaka mitatu tangu kumaliza chuo kikuu (UDSM) mwaka 1974 kwa mtazamo huo na yeye kaikuta kwa nini kuingiza suala la dini hapa? Leo hii amekuwa Rais unataka kuwadanganya Waislamu kwamba madai ya katiba mpya yamekaa mkao wa kidini!!!!!!!

Lete hoja ya kupinga au kukubali katiba mpya zilizojaa uzalendo utaeleweka.
 
Hashim Mbita, yule balozi maarufu naye kaunga mkono katiba mpya.


Tatizo la ndugu yangu Comrade Malalria Sugu ni kuwa haijui historia ya kudai katiba mpya.............vuguvugu za kudai katiba mpya ndiyo ziliisukuma serikali kuitia viraka 15 katiba hii iliyopo ya mwaka 1977...........Kumbuka government white paper wakati wa Mzee Rukhsa.........Muislamu mwenzio.....................hili hakuna udini ......mbona akina Profesa Karim Hirji wa Muhimbili jana alidai katiba mpya..........na huo ni udini ....................Je Profesa Shivji naye sasa wataka kumwita msaliti wa waislamu?

Na hawa je wataka kusema nao hakuna waislamu kwenye kudai katiba mpya?

Kongamano la Katiba leo


na Betty Kangonga


amka2.gif
WANANCHI pamoja na viongozi wa vyama vya siasa nchini wanatarajia kukutana kesho kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayoendelea nchini likiwemo na suala la Katiba Mpya.
Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa mkutano huo, Ibrahim Mwambuja, alisema wamealika watu zaidi ya 50 kuhudhuria mkutano huo.
Alisema wamefikia hatua hiyo, baada ya kuona kuna masuala muhimu yanayohitajika kujadiliwa ili kuhakikisha yanapatiwa ufumbuzi wa kudumu hasa katika suala la upatikanaji wa Katiba mpya ambayo itasaidia kuleta utatuzi.
Alisema viongozi wa vyama vya siasa pamoja na vyama vya kiraia, vitakavyoshiriki watahakikisha wanajadili pia masuala yanayohusu siasa, uchumi na jamii ili kuwawezesha wananchi kuwa na uelewa na kuweza kufikia malengo.
"Katika mkutano huo hatutakuwa na mgeni rasmi bali vyama vya siasa na vile vya kiraia vitajadili masuala yanayoendelea kwa sasa yakiwemo la Katiba, siasa, uchumi na jamii kwa ujumla," alisema.
Alisema hakuna kiingilio katika mkutano huo, bali wananchi wote wanaohitaji kuhudhuria wanakaribishwa ambapo wanategemea kuanza majadiliano hayo majira ya saa 8 mchana.


Malaria Sugu........tatizo lako huielewi historia ya nchi hii...na ndiyo maana hoja za JK za udini zisizo na mashiko umezishupalia.......................when will you learn to be your own man and stop being a JK surrogate soldier and stand for the truth for the benefit of the posterity?
 
Mh LIPUMBA 95 HADI 2005 alikuwa mkali sana na aliomba watz wamunge mkono kudai katiba mpya, Ilichukua miaka 10 . alilalama kwamba kura zake zimekuwa zakichina, amebiwa kura watu hawkumsukiliza lkn wanaharakati wa tz ambao tayari ofisi zao zilikuwa wazi. zilikaa kimya, zilifumba macho na kuona hakuna umuhimu wowote ule.Wakati ule ambapo rais alikuwa mh Mkapa, mashirika ya dini amabyo sasa yamekuja kwa sauti kubwa hayakuona umuhimu wa katiba mpya. hakuna aliehoji umuhimu wa katiba mpya, na wengine walikuwa wakali wakisikia wtu wanataka katiba mpya. lkn mara tu baada ya dk slaa kushindwa na kulalalmika huku wabunge wa chadema wakitoka Bungeni , wakidai kura zao zimechakachuliwa . sasa wanaharakati na viongozi wa dini wamekuja na mkakati huu wa katiba mypa chini ya Utawala wa JK, wale waliokuwa wanaona hakuna haja ya katiba mpya ndani ya utawala wa Mh mkapa ndio hawa wanaotakla mabadiliko wakati wa JK, waliokuwa wakiona tz ipo sawa tu ndio sasa wanaokuja na katiba mpya
JEE WATZ WAMEZALIWA UPYA?
Kwa mwendo huu katiba haitapatikana kamwe, kila atakayeingia atataka kuilinda katiba iliyopo kwa nguvu zote hata kutumia argument za imani kama MS
 
tatizo hapa kwanini baadhi ya viongzoi wa dini waliamka wakati wa mwiny na wakati wa jk tu?

Malaria Sugu hukumbuki wakati wa Mwinyi iliandaliwa WHITE PAPER.......................ambayo ndiyo ilizaa mabadiliko ya 13 ya katiba yetu.......wataka kuwatuhumu viongozi wa dini hawakushiriki kwenye hilo?
 
Siasa huwezi tenaganisha na dini, kichokatazwa kwa katiba yetu ni kutobauana kwa dini zetu. kama waumini watakatazwa kushiriki siana, ni nani sasa atashiriki?
 
Nakubaliana na wewe kabisa lakini, je KATIBA MPYA iandikwe na sisi Wa-Tanzania wa kawaida huku chini au tukubali kukaa pembeni WATAALAM WA SHERIA wakatuandikie hiyo katiba kama ambavyo anyoonekana kupendekeza mwenzetu Jaji (Rtd) Bomani kwa watawala??????

Watalaam hawawezi kujua mawazo yangu na nini nahitaji kiwemo kwenye Katiba mpaka pale watakaponiuliza. Sitaki sasa waniulize ilaq nataka niwaambie nini Watanzania tunahitaji kiwemo kwenye katiba hiyo Mpya. Tutawaambia sasa kwa kupitia makundi mbalimbali ya kijamii. Sitaki kuyarudia tayari yameshatajwa hapo juu
 
Nakubaliana na wewe kabisa lakini, je KATIBA MPYA iandikwe na sisi Wa-Tanzania wa kawaida huku chini au tukubali kukaa pembeni WATAALAM WA SHERIA wakatuandikie hiyo katiba kama ambavyo anyoonekana kupendekeza mwenzetu Jaji (Rtd) Bomani kwa watawala??????

Kwenye blue, nina mashaka na wataalamu wetu wa sheria nchi hii kwani wameshachakachuliwa na utaalamu umekuwa wa kisiasa na maslahi ya mafisadi angalia mfano wa mikataba ya manufaa kwa nchi kama madini,mafuta, gas, umeme wataalamu wamefanya utumbo mtupu na historia itakujawahukumu, mfano mwingine issue ya mgombea binafsi ilivyoamliwa kisiasa kwa kufurahisha watawala na si maslahio ya nchi
 
Tatizo letu ni moja tuu watanzania haijalishi Mtu amesoma au hajasoma tuna ubinafsi ambao hautatujenga hata kidogo katika maisha yetu kwani hatuwezi kuona jambo katika mapana yake na kujua kipi ni cha ubinafsi na kipi ni cha Taifa.

Kulikuwa na haja gani ya wachangiaji hapo juu kuanza kusema oooh MIchango ya WAISLAmu au wakristu ikaguliwe kwenye swala nyeti kama hili la KATIBA nachelea kusema kuna watu wamesoma ila helimu haiwasaidiii hata kidogo.

Ndugu zangu swala hili ni nyeti sana yakupasa kufikiri na kujua ni kwa maslai ya Tanzania ya miaka ijayo ambayo mimi au wewe pengine hata hatuta kuwepo ila watakuja kufaidi watoto wetu. Ingependeza kama tungekuwa na mawazo chanya kwenye mambo ya maendeleo na kuacha hizi fikira za ubinafsi kwakuwa Amesema askofu basi tunaanza mawazzo finyu yasio jenga, kwanini usiweke mbali tofauti zako na ukafikiri kama mtanzania asiye kuwa na dini wala kabila bali wote ndugu moja,?

Nina umea sana pale ninapo ona sisi wenye nguvu ya kupeleka taifa hili mbele tunakuwa na fikira finyu kiasi hiki i real doubt if we can reach far by this attitude.
 
Watawala waliopo madarakani wanapinga mabadiliko ya katiba kwani wanapenda kuendelea kuwa madarakani waendelee kuwaibia watanzania.Miaka 50 ya uhuru hakuna maendeleo yoyote tuliyopata zaidi ya kushuhudia watawala wakiiba pesa zetu na kutuachia umaskini.CCM imekuwa machunguo ya kijani ambayo mafisadi wanatumia mwamvuli wake kuvuna pesa za walipa kodi na wanakuwa wakali sana wanaposikia mabadiliko ya katiba kwani wanafahamu kuwa watatenguliwa na kuwekwa kando ya mfumo unaowapa utamu wa asali
 
Uhuru wa nchi 1 kujiunga na mashirika ya dini kama Uhusiano wa TANZANIA na vatican, OIC3) 2 siku za mapumziko nDANI YA KATIBAIBARA ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi juu ya uhuru wa kuabudu na kueneza dini (hapa tunatakiwa tuangalie nini maana ya kashifa kwani tayari kuna mtu alifungwa kwa kusema yseu sio Mungu) Sheria ya Ugaidi nambari 21 ya mwaka 2002. Inafaa watu wajiulize kwanini Sheria hiyo isipitishwe baada ya Tanzania na Kenya kuathirika vibaya na ugaidi mwaka 1998. Badala yake imepitishwa baada ya ugaidi uliofanywa Marekani? 3 Jee ni kweli sheria hii imewekwa kwa maslahi ya Watanzania?jee hii haithiri misaada ya baadhi ya waumini na meandeleo yao nchini


1) VATICAN NI NCHI SIO SHIRIKA LA KIDINI 2) UNATAKA MAPUMZIKO, (uakumbuka enzi ya Mwinyi sikukuu ikiwa j2 ina hamishiwa j3 na was it practical, nafikiri tunahiji ufanya kazi zaidi kuliko kupumzika, kwani kupumzika itakufanya uende AHERA, nafikiri tuna sikukuu nyingi mno nafikiri iadi zipunguzwe hata kama ni za kikristo 3) ni ujinga na mawazo mgando kuendlea kufikilia misaada ndo tutajenga nchi yetu think twice:hungry:
 
Sidanganyiki - Leo ndio mnajua Tanzania inahitaji katiba mpya? Mambo mengine yanashangaza sana; leo kila mmoja wa watu mashuhuri anatafuta gia ya "kutokea"; mwisho Rais na wajumbe wa Kamati Kuu nao watakuja na kusema "wanataka Katiba Mpya". Nimekaa naangalia wanaojitokeza kudai katiba mpya na wanaripotiwa huku wakibeba ujiko wa ofisi na vyeo vyao; ati kuanzia Mkapa na sasa Jaji Mkuu na wote wengine katikati yao ati wote sasa "wanataka Katiba Mpya"! Really? Why?Ati leo viongozi wa dini nao wanajitokeza na kudai Katiba Mpya! Mwisho wataanza kuja na wabunge wa CCM wakidai Katiba Mpya! Utani mwingine jamani!Katiba Mpya? Kwani hii iliyopo imegunduliwa ina matatizo gani ambayo hawakuyaona miaka 20 iliyopita? Kwamba mwaka 2010 ndio wamegundua kuwa Katiba ina matatizo? Naam, watasema imejulikana kuanzia 1992. Watasema kuwa miaka yote hii kumekuwa na "kilio" cha Katiba Mpya na wengine watatuambia jinsi walivyojaribu kuzungumzia hili miaka yote hii wakituambia juu ya Ripoti ya Nyalali n.k Lakini miaka yote hiyo hawakujitokeza hawa kwa nguvu hivi kudai "katiba mpya". Lakini cha kuudhi na ambacho naamini ni cha uzugaji uliokubuhu ni kuwa wote hawa hawakuwa na ujasiri wa kudai Katiba Mpya kabla ya uchaguzi. Tangu 2005 hadi ulipofika uchaguzi huu wengi tumeandika na wengine wamelalamikia matatizo mbalimbali. Suala la ubovu wa tume ya uchaguzi halikuibuliwa kwenye uchaguzi wa 2010; wengine tulishabeza wapinzani kwenda kwenye uchaguzi huu uliopita wakiwa na tume ile ile na mfumo ule ule na tukasema mapema wasije kulalamika "tume ya uchaguzi, tume ya uchaguzi". Tulisema wamekubali kucheza kwa kanuni za mchezo na refa ambaye tayari alishajionesha kuwa ana upendeleo akiwavuruga wasilalamike. Sijui walisahau wapi yaliyotokea Kiteto? Walisahau vipi yaliyotokea Tunduru?Lakini sasa siyo wapinzani tu hata viongozi wengine wa serikali na hata wa CCM wanaanza kudai Katiba Mpya. Kilichonishangaza ni kuwa Rais Mkapa anadai naye Katiba Mpya! Really? I mean Really? Alikuwa Rais kwa miaka 10; alisimamia mabadiliko ya Katiba ya 2005 - lakini hakutaka Katiba mpya then? Lakini wote hawa wanaojitokeza kudai Katiba Mpya hawataki kusema kitu kilichowazi; Hawataki kusema hasa kwanini sasa baada ya uchaguzi wamepata ujasiri wa kudai Katiba Mpya. Walijua sheria ya uchaguzi, walijua mfumo wa tume ya uchaguzi; walijua malalamiko ya Katiba mpya lakini kwa miaka karibu ishirini walikaa kimya. Lakini sasa kuna kitu kimetokea; kitu ambacho hawana ujasiri wa kukisema au kukiita kwa jina lake. Hoja ya kuandika upya katiba haiwezi kunogeshwa kwa kutokuwa tayari kuita ukweli kwa jina lake. Ni nini kilitokea baada ya uchaguzi; au swali sahihi zaidi ni nini kilitokea wakati wa uchaguzi ambacho kimewafanya watu waamke na kudai Katiba Mpya. Wakiseme kwanza na waseme wasimung'unye maneno; vinginevyo wapo ambao watawasaidia kukisema hicho kinachofanya hoja ya Katiba Mpya iwe na nguvu sasa kuliko 1992. Dare to say it otherwise.. naomba tuachane na hoja ya Katiba Mpya hadi tutakapokuwa tayari kusema hasa ni kwanini tunataka Katiba Mpya hasa baada ya uchaguzi wa 2010.

MS nadhani wewe tatizo lako ni moja tu - Unatafasiri kila kitu ktk mtazamao wa dini jambo ambalo si sahihi.
Pamoja na hayo post yako hapo juu ina maswali ya msingi na ningeomba uone hoja unazopewa na wanaJF.
Unajua pia lazima ukubali kwamba huwa kuna majira na nyakati kwa kila kitu. Sasa wewe ukishupaza shingo kinyume na majira basi utaumia bila shaka. Hata katika maisha ya kawaida kuna mabadiliko tunayafanya ili kuitikia matakwa ya wakati.

Kama utakumbuka wakati Tritel na Mobitel zimeingia simu ya mkononi ilionekana ya watu wenye fedha tu and my friend kama una Mobitel lako (Kuuuuubwa) ukapanda daladala watu wangekushangaa maana walijiuliza kwa nini usipande Taxi!!! Sasa jiulize why do you have a mobile phone now and not then..?? Nyakati zimetusukuma kaka and whoever is shouting is simply responding to that force!!

Kitu cha pili joto la kisiasa lililopo sasa huwezi kulifananisha na wakati wowote kati ya 1995 na 2005. Ukiangalia hakuna wakati watanzania wamefuatilia kwa karibu siasa za nchi kama uchaguzi 2010, mikutano ya Lipumba na Slaa imetuonyesha hilo. Cheyo na Lipumba ni kweli waliwahi kulalamikia kuibiwa kura lakini kipindi hicho hatukujua ni kwa kiwango gani siasa zinaathiri maisha yetu ya kila siku. Leo hii najua ni siasa kwa sababu kitoweo nilichohifadhi kwa taabu kwenye kafriji kangu toka China kimeoza sababu ya Tanesco=Richmond,IPTL,Dowans.

Wewe ni shahidi kuwa CUF na CDM wagombea wao kibao ushindi wao umechakachuliwa (mikoa ya Lindi, Shinyanga, Rukwa, Iringa, Pwani, Kagera n.k) na wananchi wamejua wameibiwa ndio maana wengi wameamu wasisubiri mahubiri ya 2015 ni bora vita vianze asubuhi.
Kwa hiyo wewe usijali nani anaongea cha msingi tuangalie kama kuna mantiki katika wanachosema.

Nashawishika kuwa this time around KATIBA itapatikana kwa sababu kuu zifuatazo (baadhi tu):
1. Kikwete hana cha kupoteza kutokana na mabadiliko yoyote
2. Nobody can swim against this wave (katiba mpya) hata JK anajua
3. Kikwete anataka akumbukwe na hakuna kitakachomfanya akumbukwe zaidi ya hili
4. Nadhani atapenda awe kwenye orodha ya Mo Ibrahim ambayo kina Mkapa wameikosa- $5m si mchezo

So MS welcome aboard!!!!!!
 
Wakati wanaharakati na wananchi wa kawaida wakitoa kilio juu ya kuundwa kwa katiba mpya,hali iko tofauti ampapo raisi amekuwa kimya kuhusu suala hilo,hata katika uzinduzi wa bunge,suala hili wengi wetu tulilitegemea kuzungumziwa lakini hali haikuwa hivyo,hebu wana JF tujadili kwa nini raisi yuko kimya kuhusu suala serious kama hili.
 
Ngoja kwanza akae kimya, anaweza haribu hali ya hewa hapa?
 
ngoja kwanza akae kimya, anaweza haribu hali ya hewa hapa?
kweli wacha anyamaze tuu anaweza kusababisha machafuko bure!
Aangalie kwanza upepo unaendaje ingawaje tunajua msimamo wake kuwa katiba iliyopo inafaa!
 
hayuko kimya bwanamaongee mara ngapi?ameshatoa tamkolake thru mama celina kombani,unless yule mama aliongea kivyake vyake bt as far as i knw ni mawazo ya boss wake,jk angeiga mfano hata wa obama kila swala(ambalo ni muimu na nyeti) linalowahusu wananchi lazima obama umuone anatoa press confrence na anapokea maswali toka kwa waandishi ila jk hii kitu haipo kabisaa uwiii tz hali ni mbaya sana
 
Wakati wanaharakati na wananchi wa kawaida wakitoa kilio juu ya kuundwa kwa katiba mpya,hali iko tofauti ampapo raisi amekuwa kimya kuhusu suala hilo,hata katika uzinduzi wa bunge,suala hili wengi wetu tulilitegemea kuzungumziwa lakini hali haikuwa hivyo,hebu wana JF tujadili kwa nini raisi yuko kimya kuhusu suala serious kama hili.

Mkuu,

Nyasatu amesema hivi,"hayuko kimya bwana, aongee mara ngapi?ameshatoa tamko lake thru mama Celina Kombani, unless yule mama aliongea kivyake vyake but as far as i know ni mawazo ya boss wake"

Hiyo, inawezekana ni sababu moja.

Ya pili, wakati wa kampeni alisema Tz kuna vyama vya msimu. Pengine hivi "vilio" vya katiba mpya yeye anavichukulia kuwa ni kelele za msimu. Na kwa hiyo, zitapotea kivyake vyake kama ilivyojitokeza huko nyuma. Kelele hizi husikika kila baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

As long as there is not a well organized force to bring about the new constitution, hivi vilio na statements za watu kupitia vyombo vya habari kudai katiba mpya, zinabakia kuwa ni kekele za mlango.. tena za msimu. na wakubwa wameshatuambia mara nyingi kuwa kekele za mlango haziwazui kupata usinginzi.

We are not yet ready for a new constitution, I guess!
 
JK hawezi kusema kitu kwani yeye ni mnufaika wa katiba bomu hii inayolalamikiwa na mamilioni ya watanzania. JK hakubaliani na wazo la katiba mpya kwani yeye ni mroho wa madaraka na katiba mpya itamnyang'anya sehemu ya madaraka yake ya kifalme anayoyafaidi hivi sasa.Mtu yoyote mwenye asili ya udikteta kama alivyo JK na viongozi wote waanadamizi katika chama na serikali yake hawako tayari kuona mabadiliko ya katiba.
 
JK hawezi kusema kitu kwani yeye ni mnufaika wa katiba bomu hii inayolalamikiwa na mamilioni ya watanzania. JK hakubaliani na wazo la katiba mpya kwani yeye ni mroho wa madaraka na katiba mpya itamnyang'anya sehemu ya madaraka yake ya kifalme anayoyafaidi hivi sasa.Mtu yoyote mwenye asili ya udikteta kama alivyo JK na viongozi wote waanadamizi katika chama na serikali yake hawako tayari kuona mabadiliko ya katiba.


Japo na visasi vyake hasa pale workout ya CDM bungeni atasema tu no option this time. Atabana lakini ataachia tu!! Ile Workout ya CDM bungeni msg yake ilienda mbali sio pale bungeni. Achana na akina Zito.
 
myself i do believe that "the time is always right to do what is right" jk wake up, its ur time man(soma alama za nyakati). lakini nasisitiza tena tena kwa jeuri na kiburi walichonacho ccm watajifanya kama vile hawana masikio ila wakumbuke waswahili walisema kufa kwa kenge mpaka damu itoke masikioni. wasubiri yanakuja hayo yote soon.
 
Back
Top Bottom