Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Mkuu(Bongo TZ) hivi kuna Petition mbili? hebu check again niliyoiona jana watu karibu 90 walikua wamesha sign hii ya leo naona 3 tu vp??
Hujakosea. Kuna Petition mbili zenye malengo tofauti. Petition ya jana yenye watu zaidi ya 100+, inahusu kuishinikiza serikali kuwekeza kwenye mradi wa umeme wa Stieglers Gorge. Petition yenyewe inapatikana hapa:TATIZO LA UMEME: TUPATIENI 'STIEGLERS GORGE' Petition

Hii ya leo ni kwa ajiri ya mambo ya Katiba tu. Sijui kama nimejibu swali lako mkuu?
 
Nimependa wazo la wakuu wa mikoa kupigiwa kura. Rais wa Tanzania ana madaraka mno ya kuijichagulia tu watu anaowataka yeye
 
Nimependa wazo la wakuu wa mikoa kupigiwa kura. Rais wa Tanzania ana madaraka mno ya kuijichagulia tu watu anaowataka yeye

Tutapigia kura vingozi wangapi wandugu? Sometimes muwe realistic! Na hao viongozi wa kuchaguliwa ndio huwa hawafanyi madudu?
 
nimefurahi sana,umechukua hatua na ni mfano kweli wa kuiga
 
Tutapigia kura vingozi wangapi wandugu? Sometimes muwe realistic! Na hao viongozi wa kuchaguliwa ndio huwa hawafanyi madudu?

I like that avatar,esp the actor himself mkuu,thanks kwa comment pia
 
Wale ambao hawajafanya hivyo, hima hima basi tuweke vidole vyetu kwenye petition; people's power=democracy
 
Tutapigia kura vingozi wangapi wandugu? Sometimes muwe realistic! Na hao viongozi wa kuchaguliwa ndio huwa hawafanyi madudu?
Mkuu, Buchanan: I think suala la kuwapigia wakuu wa mikoa kura, is a very realistic thing. So far tunapiga kura za aina tatu kama sikosei: (a) Udiwani (b) Ubunge, and (c) Urais. Kama Diwani anayeongoza Kata anapewa umuhimu wa kupigiwa kura, iweje useme kuwa kumpigia mkuu wa mkoa kura ni jambo lisilowezekana? Binafsi, nadhani pendekezo la mkuu wa mkoa kupigiwa kura, ni pendekezo la muhimu zaidi ya hata ya lile la kuwapigia kura madiwani, na wabunge.

And here is why: Endapo kama katiba itabadilishwa ili wakuu wa mikoa wapigiwe kura, possibility ni kwamba, hao watakaojiotokeza kugombea hizo nafasi, watazunguka katika sehemu zote za mikoa yao na kujionea dhiki inayowakabili watu wa huko mikoani. On top of that, huyo mgombea atalazimika kutoa maelezo/sera ya jinsi atakavyotatua hizo dhiki. Wananchi wakiona kuwa mapendekezo yake/sera zake ni mazuri, then watamchagua.

Na wakishamchagua, kwa kuwa ametoa ahadi kuwa atafanya hiki na kile akichaguliwa; akishindwa kutimiza hizo ahadi, wananchi watakuwa na maswali ya msingi ya kumuuliza kwenye uchaguzi ujao: "uliahidi kutufanyia hiki na hiki, mbona hukufanya hivyo?" Hiyo itamlazimu atoa maelezo kwanini hakufanya hivyo. Wananchi wakilidhishwa n maelezo yake, basi watamchagua tena. Wasipolidhishwa, watamchagua mtu mwingine mwenye sera nzuri zaidi yake. And that's what we call accountability.

Plus, hili litapunguza tatizo lililopo hivi sasa, ambapo Rais (kwasababau zisizoeleweka), amelewa madaraka [saaaaana] ya kutupachikia wastaafu wa jeshi kuwa wakuu wetu wa wilaya na mikoa.

Maana ukweli ni kwamba, wastaafu hawa wajeshi [wengi wao]hawana vision wala strategies nzuri za kuendeleza mikoa yetu. Matokeo yake, nchi nzima inakuwa too concentrated in Dar and Dodoma. That's why hata vyama vyetu vya mageuzi (Chadema included), vinadhani Tanzania ipo Dar peke yake. No, Tanzania iko huko Mtwara na Kigoma pia.
 
Mkuu bongo tz nimeshatekeleza wito wako kwa kusain petition, asante kwa kuchukua hatua na tutawasha huuu moto mpaka kieleweke. Mimi nadhani wenye ripoti ya jaji nyalali watupostie na jaji kisanga tunataka kufanya reference. Katika mambo mengine takukuru iwe independent, lakini pia ninapendekeza rais wa nchi atangazwe mshindi kwa kupata kura zaidi ya 50% za wote waliojiandikisha kupiga kura.
 
mchakato wa katiba nimeupenda-ila sijaona alezungumzia swala la muungano-naombeni pia liwe kwenye priorities zetu
 
Wale ambao hawajafanya hivyo, hima hima basi tuweke vidole vyetu kwenye petition; people's power=democracy
Thanks Seniorita kwa kuwahimiza watu wasaini petition. Nawashuru wale wote ambao wamefanya hivyo tayari. I mean, hapa JF kuna ideas nzuri sana. Lakini tusipoamka na kuanza kutranslate hizo aideas kwenda kwenye vitendo, tutakuwa tunaifanyia nchi yetu disservice. Please go and sign the petition.
 
mchakato wa katiba nimeupenda-ila sijaona alezungumzia swala la muungano-naombeni pia liwe kwenye priorities zetu
Mkuu, Edward Teller: unaruhusiwa pia kutoa mapendekezo yako kuhusu ni nini ungependa kiwemo kwenye Katiba Mpya tunayodai. Ukisha sign petition, kuna sehemu inakuruhusu kuweka comment, please put your comment there. Hizo comment zitapitiwa na watu wenye utaalamu kwenye mambo ya sheria, then comment zote zilizokaa vizuri, zitaingizwa kwenye hard copy ya petition. Naona Dr. Wilbroad Slaa ameitikia wito na kusaini petition. Naomba akina Zitto, Lissu,na Mbowe pia waige mfano wa mzee wetu, wasaini petition. Hope nimejibu swali lako.
 
mkuu point zako nzuri sana,ila naomba nipingane na wewe kwenye suala la kupinga matokeo ya urais mahakamani maana kma unavyotujua sisi watanzania hatuna utamaduni kukubali kusema tumeshindwa hata kma kila kitu kinaonesha tumeshindwa kihalali.

Mfn mzuri ni hizi timu zetu za mpira utakuta wamezidiwa kila kitu na wamefungwa ukiwauliza watakupa sababu za kitoto kbs,hii ni hv hv mpk kwa wanasiasa,kwaiyo me naona kama tukiweka suala la kupinga majibu mahakamani NCHI HAITA TAWALIKA,me nazan kuna na NEC huru inatosha kbs. Hayo ndo mawazo yako.m

Lakini pia naomba niongeze kitu ktk iyo list yako, naomba pia tushinikize kua wanasiasa walipe kodi pia. Maana hawa watu (rais,makamu wa rais,waziri mkuu, mawaziri na wabunge)hawalipi kodi kabisa,me naona hili ni ttz maana kma mtu ulipi kodi huwez kuwashinikiza wawekezaji walipe kodi maana wewe u don't feel tha pitch. Nazan wakilazinishwa kulipa kodi watawashika mashati na hao wawekezaji pia
 
Thanks again bro this is what i was fighting for........ Vipi kuhusu ile issue ya kuwa na hard copy as well.

You know majority ya watu hawapo online... and Once Dr. Slaa nilivyomuuliza kuhusu hii issue alisema tukipata kama 5million people wanaweza wakawa enough sasa that number kuipata online peke yake itakuwa tabu.

So I was suggesting kama una hard copy ili watu waziprint na kuzitoa copies na kuwapata watu mitaani na vijijini ili wazisaini all is needed ni address ya kuzipost pindi baada ya kuzijaza. Thanks again. Together we shall overcome
 
mkuu, edward teller: Unaruhusiwa pia kutoa mapendekezo yako kuhusu ni nini ungependa kiwemo kwenye katiba mpya tunayodai. Ukisha sign petition, kuna sehemu inakuruhusu kuweka comment, please put your comment there. Hizo comment zitapitiwa na watu wenye utaalamu kwenye mambo ya sheria, then comment zote zilizokaa vizuri, zitaingizwa kwenye hard copy ya petition. naona dr. Wilbroad slaa ameitikia wito na kusaini petition. naomba akina zitto, lissu,na mbowe pia waige mfano wa mzee wetu, wasaini petition. Hope nimejibu swali lako.
nimekusoma mkuu-nitafanya hivyo
 
Back
Top Bottom