Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Kama kweli katiba watanzania wanaitaka kwa nini serikali isiwape, kwani tatizo ni nini hasa la kutokubali katiba mpya kwa serikali?
 
• Asema ndiyo njia ya kuondoa mifarakano

na Datus Boniface

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania.

Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na Balozi Liberata Mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na Katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.

Alisema kama nchi wanachama zikiwa na Katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia Katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.

Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye Katiba zilizopo.

Alisema Katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.

Alisema uundwaji wa Katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa.

"Tunakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuunganisha umoja wetu wa kitaifa… kuna baadhi wamegusia juu ya matatizo yetu ya kisiasa na baadhi yetu tunafikiri kuwa siku ya kuadhimisha uhuru ni kilele cha kujenga umoja wetu wa kitaifa… uhuru wetu wa Katiba tulizonazo ni ushahidi wa dhuluma hii.

"…hatuna Katiba zingine zaidi ya zile ambazo tumezirithi kutoka kwa wakoloni, Katiba ambazo hazina umakini, tunahitaji mpya," alisema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, Rais Mkapa alisema chaguzi nyingi zitakuwa huru na haki endapo kutakuwa na Katiba bora.

Akinukuu maneno ya mwandishi wa vitabu duniani (hakumtaja), ambaye pia ni mwanafalsafa aliyesema, ‘Chaguzi za Haki ni muhimu kwa Katiba bora.'

Alisema katika uundaji wa Katiba mpya, ni lazima kuwepo makubaliano maalum, kwa pande zote za kisiasa, kijamii na kijiografia, huku kanuni pamoja na mambo muhimu yakizingatiwa.

Alisema malumbano na migororo ndani ya nchi, yanasababishwa na muundo wa Katiba zinazoonekana kutokidhi haki na usawa.

"Katiba ndiyo moyo wa nchi, moyo wa mwanadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi… hivyo kwa kuangalia mbele tunahitaji kuundwa kwa Katiba na mihimili yote ya nchi, tunahitaji Katiba huru itakayotulinda katika hatari," alisema Mkapa.

Akitoa mfano, Rais Mkapa alisema kumekuwa na sakata la uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi katika nchi za Tanzania na Kenya, huku akisistiza kama lingekuwa ndani ya Katiba isingesababisha malumbano makubwa.

Kauli ya Rais Mkapa, imekuja wakati watu wa kada mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wasomi na wanaharakati wakiishinikiza serikali kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo, kwa madai kuwa haikidhi matakwa.

Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichoonekana kupingwa na watu wengi.
Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwani, serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.

Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani naye juzi alivunja ukimya na kusema kinachoisumbua serikali iliyoko madarakani ni woga ambao hauna msingi wowote.

Alisema Katiba iliyopo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati, kwani wakati huu inakinzana katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora.

Naye Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati maarufu, Issa Shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe Katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.

Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.
 
mkapa ni mnafiki mkubwa baada ya kustaafu ndio anakumbuka kuwa hii katiba yetu ni bomu! Alipokuwa madarakani aliona akae kimya ili kula kuku na nyama za kuchoma bila bugdha yoyote sio?

Apotelee mbali huyu mchawi aliesababisha nchi yetu kuwa na wakimbizi ktk nchi za nje baada ya kufanya mauaji ya halaiki huko zanzibar na iko siku itafika huyu mzee atafikishwa ktk mahakama ya kimataifa kwa mauaji ya raia zake ili yeye na chama chake wabaki madarakani!
 
Yaani Mkapa alipokuwa madarakani hakuona tatizo hilo, baada ya kufaidika na katiba hiyo sasa ndipo anafungua macho na kuiona ina udhaifu? si ajabu kuwa hata Kikwete atakapoondoka madarakani ndipo atakaposema kuwa Tanzania inahitaji Katiba mpya
 
Msiwe na wasiwasi, hata Kikwete, Sitta, Makinda, Pinda, Werema (AG), Makame na Kiruvi watakuja kusema mwaka 2016 kuwa Tanzania inahitaji katiba mpya. Na watalipigia kelele hili swala kuzidi Slaa na wapinzani wengine.
 
Mkapa anayo haki kama mtanzania yeyote kusema kile anachofikiri ni safi kwa nchi yake. Nampongeza angalau kwa kukubali kuona umuhimu wa katiba mpya kuliko wale ambao mpaka sasa wanatwambia hakuna umuhimu wa katiba mpya!

Kwa pamoja tanzania itapata katiba mpya. TAFAKARI!
 
Msiwe na wasiwasi, hata Kikwete, Sitta, Makinda, Pinda, Werema (AG), Makame na Kiruvi watakuja kusema mwaka 2016 kuwa Tanzania inahitaji katiba mpya. Na watalipigia kelele hili swala kuzidi Slaa na wapinzani wengine.
infwact Kikwete naye anataka katiba mpya na mchakato utaanza karibuni ili siku anaondoka 2015 tutakuwa na Katiba Mpya, ndio maana Celina kasema hilo jambo linazungumzika na isiwe ni hoja ya kisiasa ingawa mwisho wa siku sisiemu wataitumia kama mtaji wa kisiasa.
 
infwact Kikwete naye anataka katiba mpya na mchakato utaanza karibuni ili siku anaondoka 2015 tutakuwa na Katiba Mpya, ndio maana Celina kasema hilo jambo linazungumzika na isiwe ni hoja ya kisiasa ingawa mwisho wa siku sisiemu wataitumia kama mtaji wa kisiasa.
Sitajali kama CCM watatumia upatikanaji wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kama mtaji wao wa kisiasa. Umuhimu ni kwamba Watanzania ndio watakaofaidika na mtaji huo.
 
Hii inatoa picha halisi kuwa ni Muhimu sana Katiba Mpya ipatikanike kabla ya uchaguzi wa 2015.
 
Yaani Mkapa alipokuwa madarakani hakuona tatizo hilo, baada ya kufaidika na katiba hiyo sasa ndipo anafungua macho na kuiona ina udhaifu? si ajabu kuwa hata Kikwete atakapoondoka madarakani ndipo atakaposema kuwa Tanzania inahitaji Katiba mpya

Kichuguu, simtetei Mkapa na wala hanipi hamu ya kumtetea. Ila kwa hili la katiba mpya, nitasimama na watu kama Mkapa kwa muda wote kuliko manafiki kama Mwinyi.

Mwalimu alileta msukumo wa katiba Mpya wakati anaondoka madarakani baada ya kuitumia katiba kwa zaidi ya miaka 22. Hayo mabadiliko aliyoyaleta Mwalimu ndiyo kidogo yanatupa ahueni sasa na kujua kuwa watu kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawatadumu zaidi ya vipindi viwili vya utawala wao. Mwinyi hakupenda, na alinung'unika sana.

Mkapa kaona faida na hasara ya katiba iliyopo, na kwa kiasi fulani (kama kweli anasema haya kwa nia njema) yuko katika nafasi nzuri sana ya kusukuma na kuleta mabadiliko. Angependa iendelee hii Katiba iliyopo angeweza kukaa kimya kama Mwinyi, au hata kupinga mabadiliko kama Moi alivyofanya Kenya.

Mkapa aungane na wale wote wanaolilia Katiba Mpya......kwa nia njema.
 
Kama watanzania wangekuwa wanataka KATIBA mpya wasingeweza kuichagua CCM, kwanza hawakuweka swala la katiba katika ILANI yao ya uchaguzi. Kwanza watu 'wamefurahia' sana hotuba ya Kikwete bungeni ambayo katika vipaumbele vyake Katiba haimo. Niliwahi kusema kuirudisha CCM madarakani ni sawa na kusema UFISADI hakuna Tanzania, KATIBA mpya hatuitaji.

Labda swala la kujiuliza ni kweli watanzania waliichagua CCM, au mizengwe ndo imekiweka chama cha mapinduzi madarakani?. Tukijiuliza watu milioni 20 waliokuwa na jazba ya kupiga kula na leo tunaambiwa wamepiga kula milioni 8, je? haitupi mashaka kwamba Tanzania hatuchagui viongozi. Hata hao ambao tunajidanganya kuwapigia kura za referendum si wateule wa kikundi fulani kinachotuletea wateule wao,
mfano mzuri Anna Makinda amechaguliwa na wabunge kuwa spika au kikundi fulani chenye malengo yake kimemleta na wabunge wakafanya kupitisha jina.Huo siyo uchaguzi na ndo unaoendelea ngazi zote
wale wanaotakiwa na wananchi hutengewa mizegwe na hatimaye tunachaguliwa viongozi hivyo basi
watanzania hatuwezi kulaumiwa kwamba tumeichagua CCM, bali mizegwe ndo imekiingiza ccm madarakani.
 
Peoples power hiyo inasumbua kila mmoja ataropoka hovyoi mwisho wa siku Peoples power itashinda
 
Mpaka akasemea akiwa nje ya Tanzania? Did he ever make any statement hapa kwetu au ndio masifa wakitoka nje ya nchi!!!! Jamani Watanzania hawadanganyiki tena, tuendelee kuelimishana hap aand beyond!!!! Knowledge will lead us to proper decisions/actions and that shall make us free at the end...Mwacheni Ben ajifurahishe huko nje maana sasa hana sana umaarufu, akitoka n akufanya such statement then anapata some fulfillment maana atatolewa kwenye mitambo kama mzalendo kumbe kupata mafuta nje ya chupa or something...
 
Mkuu Adili, nimekupata. In fact, hicho ndicho precisely tunachokifanya hivi sasa. (i.e. kuwashirikisha wananchi wote mijini na vijijini katika zoezi hili). Ila inabidi tuwe realistic hapa kaka, wataalamu wa sheria/Katiba wana sehemu yao pia, ambayo ni kuyapiga msasa maoni tutakayoyatoa. And I don't think we should entirely dismiss them. Otherwise, nakubaliana 100% na kile ulichosema/andika. Thank you.
Ndugu BongoTz,
Hoja yangu ni - tutafanya makosa kuwa na wataalamu wa katiba wakati hata hatujui watanganyika wanataka nini...
. Umesema ---"kuwashirikisha wananchi wote mijini na vijijini katika zoezi hili......." Kwa petition link uliyotuelekeza sioni vipi utamhusisha kaka Karumanzila ambaye hata simu ya mkononi hana uwezo wa kuipata kujiunga na kupeana mawazo kupitia njia uliyotuelekeza..
Naomba kusahihishwa.......
 
Sawa sawa, mkuu! Nimekupata. In fact, jana usiku niliamua kuoutline baadhi ya mambo makuu tunayotaka yafanyiwe marekebisho. I think ukingia kwenye petition utaona hayo mabadiliko. Plus, nitaendelea kufanya updates kadri mawazo mpya na mazuri yanavyozidi kutolewa. Shukrani kwa ushauri mzuri.

You are welcom, vita ni vyetu wote na watoto wetu na hata wale watakaokuja after us; we must leave legacy behind, whether we are recognized or not; we shall do the right thing. Thanks for the link, nitaicheki right away
 
• Asema ndiyo njia ya kuondoa mifarakano

na Datus Boniface

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania.

Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.
Luteni nakupa heko pamoja na kuwa ni taarifa za magazeti mabandiko unayochagua kupost yamekwenda shule yana, hoja za msingi great thinkers kujadili.
 
mkapa ni mnafiki mkubwa baada ya kustaafu ndio anakumbuka kuwa hii katiba yetu ni bomu! Alipokuwa madarakani aliona akae kimya ili kula kuku na nyama za kuchoma bila bugdha yoyote sio?

Apotelee mbali huyu mchawi aliesababisha nchi yetu kuwa na wakimbizi ktk nchi za nje baada ya kufanya mauaji ya halaiki huko zanzibar na iko siku itafika huyu mzee atafikishwa ktk mahakama ya kimataifa kwa mauaji ya raia zake ili yeye na chama chake wabaki madarakani!

"Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa."
 
YeshuaHaMalech

umesema..."Yesu ni Bwana, Kila goti litapigwa ... Huna unachoweza kufanya juu ya hilo! "
Mimi nafikiri -- hapa mduniani uwezo tunao. Tupunguze mara ngapi tutapiga magoti kwa kuondoa mfumo wa utawala mkoani
Naomba kuwasilisha hoja,,

Adili
 
Back
Top Bottom