Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

THUBUTUUU....... Kwa Ruhusa ya nani??? JK??? Hakubali Ng'o?????? Atamuuliza mbona yeye Hakuitaka kipindi chake?????

Suala la katiba ni la watanzania wote. Tunapomwachia mtu au kikundi cha watu waamue hatima yetu ni makosa. Nashangaa hata wanaoshiriki uchaguzi kwa katiba iliyopo
 
Baada ya kuonja shubiri ya katiba ya sasa kwa jinsi JK alivyoitumia ndio anaomba katiba mpya? Kwa nini hakufanya hilo yeye? Kama kweli amedhamiria hilo aje na kulianzisha kwenye vikao vya NEC ya CCM.
 
Mnafiki kwanini hakufanya hivyo wakati akiwa rais wa JMT??au hakuiona kipindi hicho?viongozi wote wakiafrika ndivyo walivyo.
 
Katiba sio msahafu, inaweza kutengenezwa upya.

Wanaomsakama JMK kuwa inatakiwa katiba mpya nadhani wanataka au wanania ya kumlaumu au kumfanya kuwa yeye ndie anaekataa kuwa na katiba mpya, wakati ukweli si hivyo.

JMK hana sababu yoyote ya kuzuwiya kuwepo na katuiba mpya. Kama uongozi, yeye ni Rais na anamamlizia kipindi chake cha mwisho. Katiba mpya kwa manufaa ya uma kwake itakuwa ni sifa kubwa. Na hilo si tatizo kwake.

Wabunge wa CCM na waupinzani waandae utaratibu wa kufikisha hili suala la katiba Bungeni na lipitishwe na ianzwe kazi ya kuitayarisha katiba mpya.

Katiba mpya, inabidi watu wawe makini kujitayarisha na kuitunga kwani ni kitu muhimu sana na si cha mchezo mchezo wala mzaha.

Naomba wote wanaomsakama JMK, waache kufanya hivyo na waanze kuwasakama wabunge, kwani wao ndio wenye jukumu la kutunga na kuzipitia sheria.
 
Mimi ni Mtanzania na pia najivunia kuwa Mtanzania lakini sjawahi kuiona Katiba ya nchi yangu!!!! katiba ninayoijua na ambayo nimeisoma ni Katiba ya Jamhuri ya Kenya. Hebu fikiria uzalendo wangu uko wapi!! Tafadhalini watanzania wenzangu hasa watawala wangu niwezeshe kuijua na kuiona katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyo nzuri kama hii.
 
Katiba sio msahafu, inaweza kutengenezwa upya.

Wanaomsakama JMK kuwa inatakiwa katiba mpya nadhani wanataka au wanania ya kumlaumu au kumfanya kuwa yeye ndie anaekataa kuwa na katiba mpya, wakati ukweli si hivyo.

JMK hana sababu yoyote ya kuzuwiya kuwepo na katuiba mpya. Kama uongozi, yeye ni Rais na anamamlizia kipindi chake cha mwisho. Katiba mpya kwa manufaa ya uma kwake itakuwa ni sifa kubwa. Na hilo si tatizo kwake.

Wabunge wa CCM na waupinzani waandae utaratibu wa kufikisha hili suala la katiba Bungeni na lipitishwe na ianzwe kazi ya kuitayarisha katiba mpya.

Katiba mpya, inabidi watu wawe makini kujitayarisha na kuitunga kwani ni kitu muhimu sana na si cha mchezo mchezo wala mzaha.

Naomba wote wanaomsakama JMK, waache kufanya hivyo na waanze kuwasakama wabunge, kwani wao ndio wenye jukumu la kutunga na kuzipitia sheria.

Inaonekana unaongea kinadharia zaidi ya hali halisi ilivyo. Hebu nipe mfano mmoja tu wa sheria iliyowahi kutungwa na bunge bila muswada kutoka serikalini na bunge kuipisha. Kama hakuna basi JK lazima asakamwe kwenye hili kwani bunge letu si kama la marekani ambapo mbunge au kundi la wabunge wanaweza andika muswada na kuuwakilisha na kisha kupitishwa hata kama Rais hata tia saini.
 
u r right 100%, nikuchekeshe, sabasaba 2007 nilifika banda la wizara ya sheria nikaomba katiba, ilikuwa JK Nyerere temeke grounds, watumishi wakanipa, wakasema ficha usimwoneshe mtu, hatugawi hovyo, nikachukua katiba yangu, nilishangaa kweli, yaani hata kutoa nakala to citizens ya hii katiba mzee hawataki, ni baada ya ku press hard ndio nilipewa, wakati umefika tunataka katiba mpya, ila mm nashangaa JK jamani kwanini watu wanalia mno kila jambo ww kimya hapa unaniboa sana JK, kila jambo kubwa ww kimya, hata la Dowans ww kimya, aiseeee
watu wakiandamana ndio mpaka ujue kuna shida? nachoka kabisa

Mkuu, pole sana! Lakini nilipokuwa Nairobi, Nakala za katiba ya Kenya zilikuwa zinauzwa na wauza magazeti tu, tena ile ya zamani nadhani hii impya itakuwa ikigawiwa bure hata kwa wanafunzi wa nursery-Tanzania! Tanzania! Sikupenda kwa Moyo wangu wote! Jina lako si tamu sanaaa! Mh, nimeshausahau kabsaa siku hizi
 
hapa JF kuna swahili na english electronic versions za hiyo katiba ya JMT. mimi binafsi niliinunua mwaka 2006 pale duka la vitabu vya serikali lililopo Jamhuri Street Posta mpya, sijui kama bado lipo. kama ukiwa na nia ya kweli utajua inauzwa wapi.
 
Asema ndiyo njia ya kuondoa mifarakano

na Datus Boniface
RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania. Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na Balozi Liberata Mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na Katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.
Alisema kama nchi wanachama zikiwa na Katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia Katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.
Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye Katiba zilizopo.
Alisema Katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.
Alisema uundwaji wa Katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa.
"Tunakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuunganisha umoja wetu wa kitaifa… kuna baadhi wamegusia juu ya matatizo yetu ya kisiasa na baadhi yetu tunafikiri kuwa siku ya kuadhimisha uhuru ni kilele cha kujenga umoja wetu wa kitaifa… uhuru wetu wa Katiba tulizonazo ni ushahidi wa dhuluma hii.
"…hatuna Katiba zingine zaidi ya zile ambazo tumezirithi kutoka kwa wakoloni, Katiba ambazo hazina umakini, tunahitaji mpya," alisema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, Rais Mkapa alisema chaguzi nyingi zitakuwa huru na haki endapo kutakuwa na Katiba bora.
Akinukuu maneno ya mwandishi wa vitabu duniani (hakumtaja), ambaye pia ni mwanafalsafa aliyesema, ‘Chaguzi za Haki ni muhimu kwa Katiba bora.'
Alisema katika uundaji wa Katiba mpya, ni lazima kuwepo makubaliano maalum, kwa pande zote za kisiasa, kijamii na kijiografia, huku kanuni pamoja na mambo muhimu yakizingatiwa.
Alisema malumbano na migororo ndani ya nchi, yanasababishwa na muundo wa Katiba zinazoonekana kutokidhi haki na usawa.
"Katiba ndiyo moyo wa nchi, moyo wa mwanadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi… hivyo kwa kuangalia mbele tunahitaji kuundwa kwa Katiba na mihimili yote ya nchi, tunahitaji Katiba huru itakayotulinda katika hatari," alisema Mkapa.
Akitoa mfano, Rais Mkapa alisema kumekuwa na sakata la uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi katika nchi za Tanzania na Kenya, huku akisistiza kama lingekuwa ndani ya Katiba isingesababisha malumbano makubwa.
Kauli ya Rais Mkapa, imekuja wakati watu wa kada mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wasomi na wanaharakati wakiishinikiza serikali kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo, kwa madai kuwa haikidhi matakwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichoonekana kupingwa na watu wengi.
Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwani, serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.
Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani naye juzi alivunja ukimya na kusema kinachoisumbua serikali iliyoko madarakani ni woga ambao hauna msingi wowote.
Alisema Katiba iliyopo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati, kwani wakati huu inakinzana katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora.
Naye Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati maarufu, Issa Shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe Katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.


Source Tz Daima
 
angalizo tu hapa: ktk mchakato mzima suala la imani litenganishwe kabisa na katiba. I mean mambo ya dini kila mtu awe huru as long as haingilii uhuru wa mwananchi mwinge wala kuleta madhara kwa nchi. Maana kuna wapuuzi wachache wanaweza kutaka kutumoa nafasi kama hii kuingiza ajenda zao za udini na ukabila.
Good point, YeshuaHaMelech! I think kale kamsemo ka zamani "nchi yetu haina dini," ni mahala pazuri pakuanzia. Ila natambua kuna baadhi watataka suala la Kadhi mkuu litambuliwe Kikatiba (na hapo ndipo manung'uniko/mpasuko wa kidini utakapoanza). But, anyway, hiyo ndo' gharama ya demokrasia...
 
hapa JF kuna swahili na english electronic versions za hiyo katiba ya JMT. mimi binafsi niliinunua mwaka 2006 pale duka la vitabu vya serikali lililopo Jamhuri Street Posta mpya, sijui kama bado lipo. kama ukiwa na nia ya kweli utajua inauzwa wapi.

tafadhali tutundikie sisi nasi tuone katiba yetu hata kama ina matatizo!!!!
 
WATANZANIA TUSIONE AIBU KUDAI KATIBA MPYA KWA KASI ZAIDI HIVI SASA

Asante sana Mzee Mkapa kwa kuongeza sauti yako, kwa MUDA MWAFAKA KABISA, juu ya madai yetu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katibapya!! Nasema asante kwa kila sauti inayozungumza HAKI ZAIDI kwa wananchi wote wa taifa letu.


Kwa umakini mkubwa na subiri na bado sijajua kwa nini sautti za waheshimiwa hawa bado kusikika: Juu ya mahitaji yetu ya mabadiliko ya kweli na mchakato kuanza mara moja, je Balozi Salim Ahmed Salim yeye anasemaje? Bob Makani, Prof Sarungi, Mzee Mwinyi, Mzee George Kahama, Asha-Rose Migiro, Prof Tibaijuka, Dr Magufuli, Dr Mwakyembe, Mzee Edwin Mtei, Imman Simba, Askofu Pengo,Salim Amur, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Prof Luhanga, Fredrick Msuya, Fredrick Sumaye, John Samuel Malecela wao wanasemaje juu ya dhuluma za KATIBA ya sasa hivi na Madai yetu kuandika kipya bila viraka zaidi??? Jaja Samata yuko wapi, Augustino Ramadhani bado hatujamsikia, mbona Mzee Mkono bado kimya??


Vijana tunataka mabadiliko ya kweli sasa hivi bila kusubiri zaidi!!!



Who the hell is Fredrick Msuya? Eti Mama Maria Nyerere hivi amewahi hata kuisoma hiyo Katiba anajua ni wapi panahitaji marekebisho, Prof. Sarungi????? Mama Karume?????!!! na wengine uliowataja hawawezi kutoa tamko kuhusiana na mabadiliko ya katiba wakati chama chao mama hakiyataki na wala hakikubali kama katiba ina mapungufu.

Mtu kama Balozi Salim, Mwinyi, Migiro, Malecela, Mufti Simba, Pengo wanaweza kusema kwani kwa sasa hawategemei chakula chao kutoka CCM na pia ni respected figures kwenye jamii hata kwenye siasa.

Jaji Samatta ni majuzi tu nilimuona iringa akisapoti katiba, Jaji Ramadhani ni ngumu kuweka hadharani mawazo yake kwakuwa yupo kwenye system.

Prof. Luhanga ataongea nini jamani hivi na vyuma na nyaya za ukandarasi navyo vinahitaji katiba , am joking lakini sitegemei kutoka kwake kwani sio mwanasiasa wala kutoka kwa Mukandara yeye ni ccm damu na ccm haitaki mabadiliko.

Mtei na makani wao nafikiri mawazo yao yako wazi yamejkaa kichama zaidi.

Mkapa anataka kuiokoa the sinking ship so anatapatapa ikumbukwe alimwachia uraisi Kikwete kwa shingo upande
 
As for me,i strongly believe that the most important yardstick of efficiency in government is whether citizens get value for their money. Do we get services? Does our quality of life improve? Are there jobs available for the youth?

The current katiba has created only penury and misery. A country that was vibrant at independence in the 60’s is now tottering under the weight of corruption, tribalism, poverty and bad governance.


Believe it or not, like Ripley says, the faulty constitution has played a BIG role in this era of misfortune. Often the only role. Our terrible winter of discontent MUST end.

This alone is a good reason to change. Change is therefore inevitable,no doubt that we NEED A NEW CONSTITUTION
....Let us ignore some nonesensical comments from doomy frantic politicians!


http://jukwaa.proboards.com/index.cgi?board=general&action=display&thread=4157#ixzz17JbNe25N
 
Je alipokuwa madarakani hakujua kama katiba mpya ndio suluhisho la migogoro?
Je wakati majeshi yake yanauwa na kupiga wapinzani katiba ilikuwa nzuri na haina migogoro?
Leo hayuko kwenye madaraka ndipo anakumbuka kuwa katiba mpya ndio suluhisho?
Unafiki wa wanasiasa ooops- tuliambiwa tumuache mzee apumzike! samahanini
 
Je alipokuwa madarakani hakujua kama katiba mpya ndio suluhisho la migogoro?
Je wakati majeshi yake yanauwa na kupiga wapinzani katiba ilikuwa nzuri na haina migogoro?
Leo hayuko kwenye madaraka ndipo anakumbuka kuwa katiba mpya ndio suluhisho?
Unafiki wa wanasiasa ooops- tuliambiwa tumuache mzee apumzike! samahanini
Mnafiki ni nani au Wabe unayejificha kama Mwanamageuko kwa mgongo wa dini nani asiyejua.
 
Back
Top Bottom