Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania."Nakubaliana na harakati za CHADEMA na vyama vingine vya upinzani kudai katiba mpya ni wakati sasa CCM ifikiri juu ya kuwapa wa tanzania katiba mpya kwani kelele zimekuwa nyingi sana"
Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na Balozi Liberata Mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na Katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.
Alisema kama nchi wanachama zikiwa na Katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia Katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.
Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye Katiba zilizopo.
Alisema Katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.
Alisema uundwaji wa Katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa.
“Tunakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuunganisha umoja wetu wa kitaifa… kuna baadhi wamegusia juu ya matatizo yetu ya kisiasa na baadhi yetu tunafikiri kuwa siku ya kuadhimisha uhuru ni kilele cha kujenga umoja wetu wa kitaifa… uhuru wetu wa Katiba tulizonazo ni ushahidi wa dhuluma hii.
“…hatuna Katiba zingine zaidi ya zile ambazo tumezirithi kutoka kwa wakoloni, Katiba ambazo hazina umakini, tunahitaji mpya,” alisema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, Rais Mkapa alisema chaguzi nyingi zitakuwa huru na haki endapo kutakuwa na Katiba bora.
Akinukuu maneno ya mwandishi wa vitabu duniani (hakumtaja), ambaye pia ni mwanafalsafa aliyesema, ‘Chaguzi za Haki ni muhimu kwa Katiba bora.’
Alisema katika uundaji wa Katiba mpya, ni lazima kuwepo makubaliano maalum, kwa pande zote za kisiasa, kijamii na kijiografia, huku kanuni pamoja na mambo muhimu yakizingatiwa.
Alisema malumbano na migororo ndani ya nchi, yanasababishwa na muundo wa Katiba zinazoonekana kutokidhi haki na usawa.
“Katiba ndiyo moyo wa nchi, moyo wa mwanadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi… hivyo kwa kuangalia mbele tunahitaji kuundwa kwa Katiba na mihimili yote ya nchi, tunahitaji Katiba huru itakayotulinda katika hatari,” alisema Mkapa.
Akitoa mfano, Rais Mkapa alisema kumekuwa na sakata la uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi katika nchi za Tanzania na Kenya, huku akisistiza kama lingekuwa ndani ya Katiba isingesababisha malumbano makubwa.
Kauli ya Rais Mkapa, imekuja wakati watu wa kada mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wasomi na wanaharakati wakiishinikiza serikali kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo, kwa madai kuwa haikidhi matakwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichoonekana kupingwa na watu wengi.
Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwani, serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.
Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani naye juzi alivunja ukimya na kusema kinachoisumbua serikali iliyoko madarakani ni woga ambao hauna msingi wowote.
Alisema Katiba iliyopo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati, kwani wakati huu inakinzana katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora.
Naye Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati maarufu, Issa Shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe Katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.
 
Mnafiki ni nani au Wabe unayejificha kama Mwanamageuko kwa mgongo wa dini nani asiyejua.

Mkuu kwa chuki, mpaka unaaibisha, nimekuacha mbali sana kwa kila kitu believe me! mwanamageuko kasema nini kibaya? halafu unasema mwanamageuko ni mimi! LOL! kuna wengi sana humu kama akina mwanamageuko na mimi, sitawataja, wengine wako likizo tu. wewe jifurahishe na mawazo yako finyu, ksiki cha mpingo hiki! angalia nimejiunga lini na nina thanks ngapi, na wewe nakupa siku humu kwa speed yako hii ya chuki, vihoro, vijiba na kimukemuke cha wasiwasi na kupata popularity! utapata presha kaka.

Note my word, nitakuuliza tena where are you in next two years, tuone kama utakuwa bado uko hivi, vinyongo humu utakoma, utakuwa hauli wala hupumui, watu wanapiga kwenye ukweli.

Narudia sijaona tatizo la post ya mwanamageuko ambayo ninaiunga mkono, na sijaona umuhimu wa post yako ambayo imejaa uwongo mwingi, bado una hasira. Nitaanza kuku-treat kama mtu mzima sasa na utapaona pachungu hapa. ask!!
 
hata kikwete akitoka ikulu ndipo atauona uozo wa katiba, baada ya kuona mrithi wake anavyofaidi
 
Mimi nasubiria kauli ya MZEE WARIOBA tu....huyu akiongea ndio atamaliza kila kitu maana ndiye mhusika mkuu wa hiyo tuliyonayo ya 1977
 
wewe jifurahishe na mawazo yako finyu, ksiki cha mpingo hiki! angalia

nimejiunga lini na nina thanks ngapi,

na wewe nakupa siku humu kwa speed yako hii ya chuki, vihoro, vijiba na kimukemuke cha wasiwasi na kupata popularity! utapata presha kaka.

Nitaanza kuku-treat kama mtu mzima sasa na utapaona pachungu hapa. ask!!
Maneno ya umbea umbeaaa tu yamekujaa kichwani mwako eti Zitto ana kiwanda cha kokoto uongo wa hali ya juu karibu utapewa PhD ya umbea humu, eti mwaka jana ukatuambia wewe ni Lecturer wa chuo Ha ha haa labda chuo cha madrasa.

wewe unaona thanks ndio ujiko wengine huwa tunatoa thanks kwa kutambua ujinga uliotoa.

Utamtisha nani wewe hatishiwi nyau mtu hapa peleka udini wako kule kwa kutumia majina bandia toka uachane na Kubwajinga sasa unatumia Mwana nani sijui ili ujifiche kwenye udini tumeshakutambua.
 
Mhh hayo maneno mekundu hayapo kwenye gazeti mzee umetoa wapi au wewe ni mwandishi wa habari hii mhariri akayatoa hayo,tujuze pls
 
hilo la mahakama ya kadhi kuwa kwenye katiba, Mkapa anachezea amani ya nchi yetu!
 
Hata JK nae atalipekesha liende ili mabadiliko katiba.kuua muungano....kuporwa urais na CDM vyote anaombea vitokee yeye akiwa nje madaraka.....yote atahakikisha hayatokei yeye akiwa Pres.....ndio hata BWM alivyohakikisha hakuna bomu linatokea yeye akiwa Pres
 
hilo la mahakama ya kadhi kuwa kwenye katiba, Mkapa anachezea amani ya nchi yetu!
Cha msingi hiyo katiba iwe wazi kuwa nchi hii haimilikiwi na dini fulani, yaani si taifa la kikristo wala kiislam au .... whatever, ingawa ni kiota cha watu wote wa dini na kabila zote!
 
[QUOTE= Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.

Hakuna sababu ya kumsakama BWM kwa kauli yake ya sasa. Labda 'ameokoka'. Tunakosea tunapowahukumu walokole wanaotoa ushuhuda kuwa 'zamani' walikuwa majambazi/wachawi na sasa wameachana na dhambi na kurudi kwa Bwana Yesu. Inavyoonesha baadhi yatu tunataka watu wasibadilike, wabaki vile vile 'yaani wahusika bapa, wasioweza kupinda na kwenda kulingana na wakati. tatizo hapa la Mkapa ni kupenda kusemea mambo makubwa nje ya nchi, akiamua kulinena hili hapa nchini, mimi sitakuwa na mashaka naye hata kidogo. Mkapa njoo front. Gonga kifua chako, sema: Ninataka katiba mpya, 'Chonya of Chilonwa me' au Chinga of Ntwara Me
 
sio bure atakuwa ameambiwa na watu fulani aseme hayo...mbona mkapa anasema kitu ambacho alikuwa na uwezo nacho 6 years back..au ndio ukitoka kwenye kiti macho yanaona ...zaidi
 
unafiki mtupu !!!!!!!!!hana uthubutu wa kuongea mbele ya kikwete.he is more of international figure and a coward ,traitor in his homeland.
YOTE YANA MWISHO,IKO SKU TUTAPATA UHURU WETU NA KATIBA MPYA.
 
sio bure atakuwa ameambiwa na watu fulani aseme hayo...mbona mkapa anasema kitu ambacho alikuwa na uwezo nacho 6 years back..au ndio ukitoka kwenye kiti macho yanaona ...zaidi

Mkuu umesahau Mh. Waziri Mkuu mstaafu Sumaye hakujua kwanini Tanzania ni masikini kwa miaka yote kumi aliyokuwa madarakani MPAKA alipoenda kusoma Marekani ndipo alipogundua kwanini watanzania ni masikini!!

labda pengine viongozi na wanasiasa wetu wanahitaji refresher course kila baada ya miezi sita!!
 
Asema ndiyo njia ya kuondoa mifarakano

na Datus Boniface
RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania. Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na Balozi Liberata Mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na Katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.
Alisema kama nchi wanachama zikiwa na Katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia Katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.
Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye Katiba zilizopo.
Alisema Katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.
Alisema uundwaji wa Katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa.
“Tunakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuunganisha umoja wetu wa kitaifa… kuna baadhi wamegusia juu ya matatizo yetu ya kisiasa na baadhi yetu tunafikiri kuwa siku ya kuadhimisha uhuru ni kilele cha kujenga umoja wetu wa kitaifa… uhuru wetu wa Katiba tulizonazo ni ushahidi wa dhuluma hii.
“…hatuna Katiba zingine zaidi ya zile ambazo tumezirithi kutoka kwa wakoloni, Katiba ambazo hazina umakini, tunahitaji mpya,” alisema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, Rais Mkapa alisema chaguzi nyingi zitakuwa huru na haki endapo kutakuwa na Katiba bora.
Akinukuu maneno ya mwandishi wa vitabu duniani (hakumtaja), ambaye pia ni mwanafalsafa aliyesema, ‘Chaguzi za Haki ni muhimu kwa Katiba bora.’
Alisema katika uundaji wa Katiba mpya, ni lazima kuwepo makubaliano maalum, kwa pande zote za kisiasa, kijamii na kijiografia, huku kanuni pamoja na mambo muhimu yakizingatiwa.
Alisema malumbano na migororo ndani ya nchi, yanasababishwa na muundo wa Katiba zinazoonekana kutokidhi haki na usawa.
“Katiba ndiyo moyo wa nchi, moyo wa mwanadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi… hivyo kwa kuangalia mbele tunahitaji kuundwa kwa Katiba na mihimili yote ya nchi, tunahitaji Katiba huru itakayotulinda katika hatari,” alisema Mkapa.
Akitoa mfano, Rais Mkapa alisema kumekuwa na sakata la uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi katika nchi za Tanzania na Kenya, huku akisistiza kama lingekuwa ndani ya Katiba isingesababisha malumbano makubwa.
Kauli ya Rais Mkapa, imekuja wakati watu wa kada mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wasomi na wanaharakati wakiishinikiza serikali kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo, kwa madai kuwa haikidhi matakwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichoonekana kupingwa na watu wengi.
Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwani, serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.
Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani naye juzi alivunja ukimya na kusema kinachoisumbua serikali iliyoko madarakani ni woga ambao hauna msingi wowote.
Alisema Katiba iliyopo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati, kwani wakati huu inakinzana katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora.
Naye Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati maarufu, Issa Shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe Katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.

Source Tz Daima

Hata yeye, inachekesha sana.Mbona katika miaka yaje kumi ya ungozi hakufanya lolote.Hawa jamaa u-freemason unawasumbua sana.
 
ameona naye aseme hili haonekane wa maana kwa kuwa tume ya J kisanga aliiweka kapuni heri alieweka kapuni mamake CCM wangeumia sana na yeye angeangamizwa kuwa mshitakiwa wa kwanza kwa kufanya ikulu kuwa kitivo cha biashara badala kuwa Mahali patakatifu, naye mwenzake akaja na Richie ya RA na EL wote hawa wangekuwa ndani, hivyo kuendelea kuibana ni sawa na kupumulia ICU bora waiachie mapema ili waje waizoeee jela kawa itakayotungwa itaruhusu rais kushitakiwa na kupunguziwa madaraka heri yake waziri wa sheria na katiba Dada Ces haouni umuhimu maana wa kwanza kuumia ni wakuu wake
 
Mkapa represents truly African leaders who are opportunistic and reactive/curative to central issues of public/national interest. Mkapa as the then President of URT could have initiated the process of amending or having a new constitution when serving for the Presidency. Those utterances depicts his hypocrisy, facade and mendaciousness at the highest degree. Shame to him and his scandalous shits when in office as the President of URT.
 
Ni upotoshaji kusema kuwa madai ya katiba mpya ni harakati za CHADEMA. Ieleweke kuwa Watanzania walianza kudai katiba mpya tangu zamani. Actually, mmoja wa wanasiasa wa kwanza kudai katiba mpya alikuwa ni Christoper Mtikila wa DP ambaye alisema way back baada ya vyama vingi kuruhusiwa in 1992 kuwa asingeshiriki kwenye uchaguzi wa 1995 bila kuwepo kwa katiba mpya kwa kuwa iliyopo ilitungwa na makada wa CCM mwaka 1977 chini ya utawala wa chama kimoja. Laiti vyama vyote vya upinzani vingesimama pamoja tangu 1995 na kukataa kushiriki kwenye uchagizi mkuu basi tungekuwa na katiba mpya sasa hivi.

CHADEMA kimetoa msukumo mpya kudai katiba mpya, lakini kamwe harakati hii haikuasisiwa na CHADEMA. Ni wananchi wenyewe wa Tanzania wanaodai katiba mpya, pia NGO zote zinaunga mkono wazo hili.
 
Back
Top Bottom