Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katika facebook yake nape anasema kama ifuatavyo:-
"NAAMINI KATIBA MPYA HAIEPUKIKI,ITS A MATTER OF TIME. TUANZE KUJADILI CONTENTS ILI TUONE KAMA TUNA VITU VIPYA AMBAVYO HAVIMO KWENYE KATIBA YA SASA!"
Nape ni mmoja kati ya wana CCM ambao hawaogopi kusema yaliyo ya kweli. Kama Nape angepata ndani ya CCM like -minded youth wa kutosha wangeweza kuleta mabadilko makubwa. Tatizo vijana wenye mawazo makubwa kama hawa hawapewi nafasi ndani ya ccm. Ila ndani ya chadema vijana wana nafasi.
Wewe hushabikii Katiba Mpya?
Mimi sio mshabiki ingawa naamini kuwa ili kuweza kujenga Tanzania tunayotaka kuiona miaka hamsini ijayo ni muhimu tukatumia muda huu kuelekea maadhimisho ya miaka hamsini ya Tanzania (2014) kukaa pamoja na kuafikiana kuhusu jinsi gani tunaweza kujenga Tanzania tunayoitaka na KATIBA MPYA itakayopatikana katika mchakato wa uwazi na ushiriki mpana ndio ufunguo wake.
Huu mchakato upo na tuna kamati ya vijana wapiganaji tunakutana tena next Monday then tutaandaa press conference kuwaeleza waandishi wa habari nia yetu na jinsi tutakavyoifanikisha.
mkapa hana lolote ni msanii kuliko hao wasanii,alikua rais na ktk chaguzi zilizomuweka madarakani nikwakutumia hiyohiyo katiba anayoiona leo haifai,alikua anachakachua tena yeye alikua dikteta wakati wautawala wake ndio watu waliuawa zenj na nchi ikazalisha wakimbizi je hayo anayajua leo?au kwakua keshakula nakusaza?kweli twahitaji katiba mpya lakini kwa che nkapa anasema mdomoni tu ni sawa na chui alievaa ngozi yakondoo.Hiyo kauli imemtoka mdomoni au moyoni? Nahisi kama anachoongea sicho anachofikiri moyoni.
Siyo kosa kwa Mkapa kutoa mawazo yake anavyoona sasa na ambavyo labda hakuona alipokuwa madarakani. Ndiyo maana kuna wachezaji kama Julio walikuwa wanafanya makosa ya ajabu uwanjani walipokuwa wanacheza mpira lakini sasa hivi wanafundisha hata yale ambayo wao hawakuweza kuyafanya uwanjani. Hata hivyo ukisoma between the lines si lazima Mkapa anaisema Tanzania ambayo angalau imefanya marekebisho zaidi ya 14 kwenye Katiba yake. In fact, kwa marekebisho hayo Katiba yetu si ya kikoloni (kama za nchi hizo anazozisema Mkapa). Yetu ni kama mpya. Hata hivyo nadhani hata CCM hawaogopi au hawapingi moja kwa moja Katiba Mpya kabisa, tufuate taratibu na kukusanya resources, na Katiba Mpya tutaiandika tu.Yaani Mkapa alipokuwa madarakani hakuona tatizo hilo, baada ya kufaidika na katiba hiyo sasa ndipo anafungua macho na kuiona ina udhaifu? si ajabu kuwa hata Kikwete atakapoondoka madarakani ndipo atakaposema kuwa Tanzania inahitaji Katiba mpya
Aaache unafiki,aitishe press conference aliseme hili waziwazi.
Siyo kosa kwa Mkapa kutoa mawazo yake anavyoona sasa na ambavyo labda hakuona alipokuwa madarakani.
Ndiyo maana kuna wachezaji kama Julio walikuwa wanafanya makosa ya ajabu uwanjani walipokuwa wanacheza mpira lakini sasa hivi wanafundisha hata yale ambayo wao hawakuweza kuyafanya uwanjani.
Hata hivyo ukisoma between the lines si lazima Mkapa anaisema Tanzania ambayo angalau imefanya marekebisho zaidi ya 14 kwenye Katiba yake. In fact, kwa marekebisho hayo Katiba yetu si ya kikoloni (kama za nchi hizo anazozisema Mkapa).
Yetu ni kama mpya.
Hata hivyo nadhani hata CCM hawaogopi au hawapingi moja kwa moja Katiba Mpya kabisa, tufuate taratibu na kukusanya resources, na Katiba Mpya tutaiandika tu.
Nafikiri anavyofanya Mkapa hatofautiani na viongozi wengi duniani yaani kuwa muwazi anapotoka madarakani angalia kina Colin Powell na Condoleezza Rice walivyomgeuka Bush kuhusu vita vya Irak.