Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Aaache unafiki,aitishe press conference aliseme hili waziwazi.
 
Katika facebook yake nape anasema kama ifuatavyo:-

"NAAMINI KATIBA MPYA HAIEPUKIKI,ITS A MATTER OF TIME. TUANZE KUJADILI CONTENTS ILI TUONE KAMA TUNA VITU VIPYA AMBAVYO HAVIMO KWENYE KATIBA YA SASA!"

Nape ni mmoja kati ya wana CCM ambao hawaogopi kusema yaliyo ya kweli. Kama Nape angepata ndani ya CCM like -minded youth wa kutosha wangeweza kuleta mabadilko makubwa. Tatizo vijana wenye mawazo makubwa kama hawa hawapewi nafasi ndani ya ccm. Ila ndani ya chadema vijana wana nafasi.


Mara zote huyu Kijana huwa na mawazo chanya. Ni wengi sasa ndani ya ccm ambao ukiongea nao pembeni watakwambia wanaona umuhimu wa Katiba mpya, ila nashangaa kwanini wasipeleke mawazo hayo kwenye vikao vyao vya chama? Heri yako wewe Nape umeweza kusoma alama za nyakati mapema!


 
Wewe hushabikii Katiba Mpya?

Mimi sio mshabiki ingawa naamini kuwa ili kuweza kujenga Tanzania tunayotaka kuiona miaka hamsini ijayo ni muhimu tukatumia muda huu kuelekea maadhimisho ya miaka hamsini ya Tanzania (2014) kukaa pamoja na kuafikiana kuhusu jinsi gani tunaweza kujenga Tanzania tunayoitaka na KATIBA MPYA itakayopatikana katika mchakato wa uwazi na ushiriki mpana ndio ufunguo wake.
 
Mimi sio mshabiki ingawa naamini kuwa ili kuweza kujenga Tanzania tunayotaka kuiona miaka hamsini ijayo ni muhimu tukatumia muda huu kuelekea maadhimisho ya miaka hamsini ya Tanzania (2014) kukaa pamoja na kuafikiana kuhusu jinsi gani tunaweza kujenga Tanzania tunayoitaka na KATIBA MPYA itakayopatikana katika mchakato wa uwazi na ushiriki mpana ndio ufunguo wake.

kwa maneno mengine ni shabiki wa katiba mpya ila hutaki kuonekana ni shabiki mno kama wengine... lol
 
MM katiba mpya ni PAI, ili uonekane walau una ubongo lazima ukubali katiba mpya ni lazima sasa. Watafuata tu hata wasioelewa mhimu tupaze sauti tu ktk hili
 
Huu mchakato upo na tuna kamati ya vijana wapiganaji tunakutana tena next Monday then tutaandaa press conference kuwaeleza waandishi wa habari nia yetu na jinsi tutakavyoifanikisha.

Next week iliyosemwa imeishapita. Lini tunawasikia?
 
Hiyo kauli imemtoka mdomoni au moyoni? Nahisi kama anachoongea sicho anachofikiri moyoni.
mkapa hana lolote ni msanii kuliko hao wasanii,alikua rais na ktk chaguzi zilizomuweka madarakani nikwakutumia hiyohiyo katiba anayoiona leo haifai,alikua anachakachua tena yeye alikua dikteta wakati wautawala wake ndio watu waliuawa zenj na nchi ikazalisha wakimbizi je hayo anayajua leo?au kwakua keshakula nakusaza?kweli twahitaji katiba mpya lakini kwa che nkapa anasema mdomoni tu ni sawa na chui alievaa ngozi yakondoo.
 
Imeripotiwa hapa JF kuwa Mkapa anaona umuhimu wa katiba mpya. Pia imeripotiwa kuwa Jaji Bomani naye amezungumzia umuhimu wa katika mpya.

Kwa upande mmoja ni hali inayoleta faraja, kwa upande mwengine inatia shaka kwa wana CCM kujitokeza hadharani na kukiri kuwa kuna umuhimu wa katiba mpya.

Sina mashaka sana na Jaji Bomani, lakini Napata tabu kuamini kuwa Mkapa anakusudia au anaamini anachokitamka.

Tunazikumbuka kauli zake za” ukweli na uwazi “au siyo?
Jee alihakikisha kuwa utawala wake kiutendaji unasimama juu ya kauli hiyo?

Watajitokeza wana CCM wengine ambao wataingia katika orodha ya watu wanaotoa kauli kuwa kuna umuhimu wa katiba mpya. Halafu wataishia hapo kwenye kauli.

CCM kama chama na serikali za CCM kama watawala hawana mazoea au utamaduni wa kuwaacha wanachama wake , na kuwaruhusu watendaji wake kutoa mawazo yao kwa uwazi hadharani. Utamaduni wao ni kuzungumzia katika vikao vya ndani vya Chama chao na Vikao vya uongozi wao.

Sasa kunani?

Lakini la kutia wasiwasi zaidi ni kuwa kauli ya Bw. Mkapa imetolewa akiwa nje ya nchi. Kwa mulio karibu naye mpitishieni ujumbe. Kama ni kweli anaamini anayoyasema basi aitishe mkutano na waandishi wa habari ili atowe kauli yake hiyo na watanzania wamsikie na hapo wanahabari watapata nafasi ya kumuuliza masuali kwa vipi anaona hiyo katiba mpya itapatikana na muda ambao anaona iwe tayari kutumika.

Kwa wanahabari au zile taasisi za kuandaa midahalo, majadiliano ni vyema kuandaa mkutano kwa kuanzia japo mmoja wa kuwaweka pamoja, kuwakutanisha hawa wote kwa pamoja ambao ni CCM ili nchi nzima ipate kuwasikia na kujuwa kuwa ndani ya CCM pia wapo wanaotaka , au wanaoona umuhimu wa katiba mpya na tuweze kusikia hoja zao.

Hofu yangu mimi ni kuwa CCM wameanza propaganda ili ionekane kuwa watalishughulikia suala la katiba. Wanajaribu kulihodhi, kuliteka nyara suala la katiba mpya. Wanajaribu ku-preempt wapinzani na wale wote ambao wamekuwa na kilio hiki cha kutaka katiba mpya kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Nitafurahi sana ikitokea kualikwa kwa Jaji Warioba katika mjadala huo, yeye ndiye alishiriki kikamilifu kuiandika hii katiba inayotiwa viraka, kwa hivyo atasaidia, kama hatoweka Uccm mbele, kuonesha mapungufu yaliyomo katika katiba hiyo,( tayari yanajulikana), lakini ataweza kuchangia kwa nini iliandikwa vile ilivyoandikwa. Na kwa nini sasa ni busara kuandika katiba mpya.

Wananchi, wanaharakati, wapinzani , vyama vya kitaaluma na asasi za kiraia zisije zikaingizwa mkenge huu kuona kuwa wanaCCM pia wanaunga mkono katika kudai katiba mpya.

Kwa CCM, linapokuja suala la CCM na Taifa , basi chaguo ni maslahi ya CCM first, baadae ndio maslahi ya taifa.
CCM na serikali zake kupitia waziri wa sheria na katiba wameshatoa msimamo wao kuwa hakuna ulazima wa katiba mpya, ila wataendelea kuweka viraka pale panapohitajika.

Tukiamini kiulaini kauli tunazozisikia basi tuelewe kuwa tunauziwa mbuzi ndani ya gunia.
 
Kumbe huwa unaamini kauli? sijawhai kuamini kauli ya mwanasiasa yeyote awe ccm awe cdm, nccr, cuf n.k

Hata msukumo wa kudai katiba na NEC huru wa chadema unaweza ukawa ni geresha tu!! kwani before election hawakujua katiba na nec vina matatizo?

Lets wait and see how far the can go
 
Yaani Mkapa alipokuwa madarakani hakuona tatizo hilo, baada ya kufaidika na katiba hiyo sasa ndipo anafungua macho na kuiona ina udhaifu? si ajabu kuwa hata Kikwete atakapoondoka madarakani ndipo atakaposema kuwa Tanzania inahitaji Katiba mpya
Siyo kosa kwa Mkapa kutoa mawazo yake anavyoona sasa na ambavyo labda hakuona alipokuwa madarakani. Ndiyo maana kuna wachezaji kama Julio walikuwa wanafanya makosa ya ajabu uwanjani walipokuwa wanacheza mpira lakini sasa hivi wanafundisha hata yale ambayo wao hawakuweza kuyafanya uwanjani. Hata hivyo ukisoma between the lines si lazima Mkapa anaisema Tanzania ambayo angalau imefanya marekebisho zaidi ya 14 kwenye Katiba yake. In fact, kwa marekebisho hayo Katiba yetu si ya kikoloni (kama za nchi hizo anazozisema Mkapa). Yetu ni kama mpya. Hata hivyo nadhani hata CCM hawaogopi au hawapingi moja kwa moja Katiba Mpya kabisa, tufuate taratibu na kukusanya resources, na Katiba Mpya tutaiandika tu.
 
Hata baba wa Taifa alitaka vyama vingi baada ya kutoka madarakani? Ukiwa madarakani katiba ya sasa inakulinda lakini ukitoka unaona mzigo wake kwa taifa.
 
Nape tunahitaji kukuona zaidi na zaidi katika mstari wa mbele kabisa kudai mabadiliko ya kweli. Ni mwanzo mzuri but not enough at all!!!
 
Siyo kosa kwa Mkapa kutoa mawazo yake anavyoona sasa na ambavyo labda hakuona alipokuwa madarakani.

Acha Uwongo, Mkapa alijua kabisa umuhimmu wa katiba mpya lakini hapa ni wazi anatafuta tu pa kutokea kuficha aibu iliyomganda kama kupe. Mkapa alikuwa na kiburi na dharau isiyo kipimo na hakupenda kuwekewa mipaka ya mamlaka ati kwa kisingizio cha katiba mpya.

Ndiyo maana kuna wachezaji kama Julio walikuwa wanafanya makosa ya ajabu uwanjani walipokuwa wanacheza mpira lakini sasa hivi wanafundisha hata yale ambayo wao hawakuweza kuyafanya uwanjani.

Acha upuuzi huo, Mkapa alikuwa Raisi wa Jamhuri ya Tanzania na huwezi kumfananisha na mchezaji wa mpira. Ni yeye aliteua wachezaji na ni yeye alikuwa na maamuzi ya mwisho mchezo uchezwe vipi. Katiba mpya ingemwekea vikwazo ambavyo vilikuwa haviendani na hulka yake.

Hata hivyo ukisoma between the lines si lazima Mkapa anaisema Tanzania ambayo angalau imefanya marekebisho zaidi ya 14 kwenye Katiba yake. In fact, kwa marekebisho hayo Katiba yetu si ya kikoloni (kama za nchi hizo anazozisema Mkapa).

Hii nayo si kweli, ni Tanzania tu ambapo tunaendelea na chama kile kile, mfumo ule ule, watu wale wale na katiba ile ile ya viraka toka uhuru. Marekebisho yaliyoweza kufanyika hadi leo ni yale yanayokiwezesha chama tawala kuwa mwamuzi, mshika kibendera na mchezaji kwa wakati moja - serikali chama.

Yetu ni kama mpya.

Are you for real ? Hakika nashindwa kukuelewa unaishi karne gani kwani angalau mkoloni aliheshimu utawala wa kisheria lakini Tanzania mh ! Katiba inayolinda maslahi ya wezi hadi serikali kuogopa nguvu za mafisadi ! Hebu fikiria hadi Waziri Mkuu anatoa machozi bungeni kwa kushindwa kutimiza wajibu kwa kuwaogopa wezi na wauaji.
Hata hivyo nadhani hata CCM hawaogopi au hawapingi moja kwa moja Katiba Mpya kabisa, tufuate taratibu na kukusanya resources, na Katiba Mpya tutaiandika tu.

Watu wengine bwana sijui mnakunywa nini kwani nani asiyejua kuwa kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa katiba mpya ni CCM kwa kulinda maslahi binafsi. Accountant, nadhani lengo kubwa la kuanzishwa kwa JF lilikuwa kutetea maslahi ya taifa na kama memba jitahidi ufanye hivyo, acha kabisa ukereketwa wa kutetea upuuzi.
 
Nafikiri anavyofanya Mkapa hatofautiani na viongozi wengi duniani yaani kuwa muwazi anapotoka madarakani angalia kina Colin Powell na Condoleezza Rice walivyomgeuka Bush kuhusu vita vya Irak.

Wow. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Colin, Condy na Mkapa. Colin and Condy walifanya kazi at the pleasure of the president. On the other hand Mkapa was the president.
 
Katiba siyo CCM AU CDM.Katiba ni ya watz wote.tunahitaji kuuangana bila kujali itikadi zetu mbalimbali katika kudai katiba mpya ambayo uandishi wake utashirikisha wananchi.
 
Katiba siyo ya CCM AU CDM.Katiba ni ya watz wote.tunahitaji kuuangana bila kujali itikadi zetu mbalimbali katika kudai katiba mpya ambayo uandishi wake utashirikisha wananchi.
 
Back
Top Bottom