Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Nakubaliana na wewe kabisa lakini, je KATIBA MPYA iandikwe na sisi Wa-Tanzania wa kawaida huku chini au tukubali kukaa pembeni WATAALAM WA SHERIA wakatuandikie hiyo katiba kama ambavyo anyoonekana kupendekeza mwenzetu Jaji (Rtd) Bomani kwa watawala??????
 
ms anapendekeza kwamba ubalozi wa vatican ufutwe katika katiba mpya, vyuo vikuu vyote viwe vya umma, misaada ya kanisa lazima ipite kukaguliwa kama inavyokaguliwa ya waislam
Sawa hayo ni mawazo yako yakikubalika na wengi yanaingia kwenye mchakato wenyewe wa katiba ila usisahau katiba ni yetu sote na vizazi vijavyo si ya kukidhi matakwa ya leo angalia kama miaka 100 mbele uone kama uliyoyapendekeza yatakuwa bado yanafaida.
 
CJ joins debate on new Constitution Thursday, 09 December 2010 23:54

The Citizen Correspondents
Dar es Salaam. Chief Justice Augustino Ramadhani has weighed into the debate on the mounting clamour for constitutional reform, urging the government to consider the issue as a fundamental need of the entire nation.
He said debate on whether or not to write a new constitution for the country should not be suppressed, but should be encouraged so that the people reach a common ground for the benefit of the nation.Chief Justice Ramadhani was speaking at the Russian Cultural Centre in Dar es Salaam on Wednesday evening, when he launched a five-year strategic plan of the Tanzania Network of Legal of Legal Aid Providers (TANLAP) to provide legal aid to the poor and marginalised in the society.
His remarks come against the backdrop of the government's adamance and insistence that there is no need for change, as the current document aptly serves its purpose. Speaking a week ago, the minister for Constitutional Affairs and Justice, Ms Celina Kombani, played down calls for constitutional reform, saying the undertaking would be "unnecessarily expensive."
But on Wednesday, the Chief Justice said public discussion of the issue could yield a proper way to go about it.
He said a decision could be reached on whether to rewrite the Constitution or simply to amend some of the articles.
He said the public's sentiments could not be ignored, as they could give an indication that the people felt they were being governed by an invalid document.
The general feeling among those calling for reform is that the current Constitution has been patched up too many times, hence the need to have a new document that addresses emerging challenges.
Mr Justice Ramadhani said the government could also seek consensus to rectify, especially areas in the Constitution that "no longer sit well with the public".

A number of prominent Tanzanians have in the recent past called for an overhaul of the Constitution to bring it in line with the current realities and developments in the country. The chairman of the Commission for Human Rights and Good Governance (CHRGG), Mr Justice (Rtd) Amir Manento, said recently that there was a need for Tanzanian to have a new Constitution.
Mr Justice Manento said since past calls for a new constitution had not yielded anything, Tanzanians should chart a new course to ensure they attain their desire for a new law.
Tanganyika Law Society (TLS) president Felix Kibodya said the time for dialogue on legal reforms had come.
Mr Kibodya, speaking in Dar es Salaam last week, said the apparent shortcomings in the electoral process presented a strong case for an overhaul of the Constitution. This, he added, was necessary to enable Tanzania to hold fair and more credible elections.

"The TLS recommends that the government initiate a consultative review of the Constitution to ensure that the views of the citizens are adequately captured so that the Constitution keeps pace with the current needs of the people as well as international standards and best practices," he added.
He said the TLS would engage the government and other key players to spearhead the constitutional review process. "I can assure you that change of the Constitution and election laws is on top of our agenda."
For his part, a law lecturer at the University of Dar es Salaam, Prof Chris Peter Maina, said the development challenges facing Tanzania could not be adequately addressed without overhauling the current Constitution. The urgency of the task, he added, could not be gained.
Chadema's unsuccessful presidential candidate, Dr Wilibrod Slaa, who campaigned for the October 31 General Election on the platform of constitutional change, declared that his party will direct its efforts in Parliament and elsewhere towards pushing for the reform agenda.
Reported by Rosemary Mirondo and Rosina John
 
Balozi Mbuta ataka mabadiliko ya Katiba Thursday, 09 December 2010 20:54

BALOZI Hashim Mbita ambaye alikuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi ya uliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) amewashangaa wanasiasa wanaoogopa kuifanyia mabadiliko katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika Televisheni ya Taifa jana asubuhi, Balozi Mbita alisema: "Katiba yetu ina ukakasi, hivyo inahitaji kufanyiwa mabadiliko ili iweze kwenda na wakati na mfumo wa kisiasa ulipo sasa na kudumisha umoja wa kitaifa".

Alifafanua kuwa katiba iliyopo inaweka sera za maendeleo mikononi mwa wahisani ambao huamua hatima ya nchi, hivyo kuzorotesha juhudi za maendeleo.
Balozi Mbita alitoa mfano kuwa wafadhili walishawahi kukataa utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka mkoani Shinyanga kwa kuwa haukuwa katika vipaumbele vyao.
Kauli hiyo ya Mbita inakuja wakati kumeibuka mjadala mkali katika jamii kwa wanaharakati na vyama vya upinzani vitaka mabadiliko ya katiba huku viongozi wa chama tawala wakiwemo wabunge na mawaziri wakipinga hatua hiyo.
Hivi karibuni, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani alisema katiba haiwezi kubadilishwa na kwamba hajui madai ya wapinzani kuhusu yanahusu nini na kwamba hawezi kushghulikia kwa vile hajapelekewa rasmi maelezo ya mambi yanayotakiwa kubadilishwa.

Wabunge wa Chadema walisimama na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kusima ili kutoa hotuba ya kufunga rasmi Bunge la kumi la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakidai kuwa hawakubaliani na katiba iliyomweka madarakani kwa kuwa ina kasoro nyingi.
Kitendo hicho kiliamsha changamoto mpya katika jamii ya Watanzania wakiwemo vijana na wasomi ambao wanasema sasa umefika wakati wa kuifanyia mabadiliko Katiba kwa manufaa ustawi taifa.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala, ambaye alishiriki katika kipindi hicho cha TBC alisema katiba mpya italinufaisha taifa kwa kuboresha misingi ya uongozi bora na siasa safi nchini kwa sababa iliyopo sasa haiendi na wakati, mfumo wa siasa na sera za taifa.

"Tatizo ni kwamba katiba inayotumika sasa ilitungwa mwaka 1977 ambayo ni ya mfumo wa chama kimoja. Katiba hii imeelekezwa katika mfumo chama kimoja, wakati nchi ni ya vyama vingi," alifafanua Profesa Mpangala.
Profesa Mpangala aliongeza kuwa katiba mpya itasadia kuufanya uamuzi wa kidemokrasia wa wananchi kuheshimiwe na kutochakachuliwa.
Hivi karibuni waziri Kombani alikaririwa na vyombo vya habari akisema suala la kuunda katiba mpya haliwezekani kwa kuwa serikali haina fedha na kwamba itaendelea na utaratibu uliozoeleka wa kufanya marekebisho ya katiba pale inapohitajika.
Naye Jaji Mark Bomani alisema kinachotakiwa sasa ni kufanyika kwa mapitio ya kina ya katiba iliyopo na kuainisha upungufu wote, kisha kufanya mabadiliko kwa mujibu wa mahitaji. "Nadhani ni woga ambao hauna msingi wowote, wanahofia kile ambacho watu watapendekeza katika katiba mpya, lakini mimi naamini watu wakikaa chini na kutulia, hawawezi kuja na vitu vya ajabu," alisema Jaji Bomani.

Madai ya serikali ya CCM kuhofia kitakachofuata baada ya kupatikana kwa katiba mpya, pia yalitolewa na Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Mujwahuzi Njunwa, ambaye aliongeza kuwa hata CCM kama wakija kushindwa katika uchaguzi mkuu, watakuwa mstari wa mbele kudai mabadiliko ya katiba.
"Hii ni tabia ya watawala wengi, kuwa na woga na kutokukubali mabadiliko, jambo hili linatoa picha kuwa serikali haipo kwa maslahi ya wananchi na taifa," alisema Profesa Njunwa.

Hata hivyo, akizungumzia hoja ya matumizi ya nguvu ya umma iliyotolewa na Chadema hivi karibuni, iwapo CCM watagoma kusikiliza hoja za mabadiliko ya katiba, Profesa Njunwa alisema serikali haiwezi kungojea hali hiyo itokee. Jaji Bomani ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria wa serikali, aliishauri serikali kuunda jopo la wataalam kutoka sekta mbalimbali watakao pitia sheria iliyopo na kuja na mapendekezo ya kuwa na katiba mpya, jambo ambalo alisema litamaliza mvutano uliopo. Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM katika Bunge lililopita, Aloyce Kimaro alisema ni vema serikali ikapewa muda wa kujipanga, lakini alisema kuna ulazima wa kuwa na mabadiliko kwa katiba. "Hakuna nafasi kwa serikali kutosikia, na kama wataziba masikio, wananchi watawalazimisha kusikia. Lazima kuwe na mfumo unaoleweka, hizi si zama za watu wachache kuamua juu ya mambo ya nchi," alisema Kimaro.

Naye Mhadhiri wa Kitivo cha sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina alipozungumza na Mwananchi Jumapili wiki iliyopita alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili, serikali mbili na katiba mbili, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984. Alisema kwamba hivi sasa kuna kero nyingi za Muungano.
 
Nakubaliana na wewe kabisa lakini, je KATIBA MPYA iandikwe na sisi Wa-Tanzania wa kawaida huku chini au tukubali kukaa pembeni WATAALAM WA SHERIA wakatuandikie hiyo katiba kama ambavyo anyoonekana kupendekeza mwenzetu Jaji (Rtd) Bomani kwa watawala??????

That's a no brainer! Nchi ni yetu sote na ni vema sote tukishiriki. Wanasheria hawajui kila kitu.
 
ms anapendekeza kwamba ubalozi wa vatican ufutwe katika katiba mpya, vyuo vikuu vyote viwe vya umma, misaada ya kanisa lazima ipite kukaguliwa kama inavyokaguliwa ya waislam

????
Unategemea kuwa kila kitu kimeanishwa kwa undani namna hiyo ndani ya katiba? Utofautishe katiba kama sheria mama kwa upande mmoja na Acts zingine kwa upande mwingine.
 
Mh LIPUMBA 95 HADI 2005 alikuwa mkali sana na aliomba watz wamunge mkono kudai katiba mpya,lkn wanaharakati wa tz ambao tayari ofisi zao zilikuwa wazi. zilikaa kimya, zilifumba macho na kuona hakuna umuhimu wowote ule.Wakati ule ambapo rais alikuwa mh Mkapa, mashirika ya dini hayakuona umuhimu wa katiba mpya. hakuna aliehoji umuhimu wa katiba mpya. lkn mara tu baada ya dk slaa kushindwa na kulalalmika . sasa wanaharakati na viongozi wa dini wamekuja na mkakati huu wa katiba mypa chini ya Utawala wa JK
Mods and administrators.. I BEG I BEG start a thread for the most offpoint posts hall of fame and permanently send MS's posts to tht area!
 
h.sep7.gif
master.gif

MABADILIKO YA KATIBA: Maaskofu waonya
• Wadai Katiba iliyopo inabeba chama tawala

na Kulwa Karedia


amka2.gif
WAKATI jana taifa lilikuwa linaadhimisha miaka 49 ya uhuru, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wameendelea kuikaba koo serikali kuwa kuna haja ya kufanya haraka marekebisho ya Katiba mpya ili inaendana na mazingira ya sasa.
Viongozi hao, wamesema Katiba iliyopo imepitwa na wakati, ndiyo maana wananchi, wasomi na wanasiasa kila kukicha wamekuwa wakipiga kelele za kutaka mabadiliko baada ya kubaini upungufu mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Wakizungumza na Tanzania Daima mjini Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti, viongozi walisema serikali haina budi kukubali matakwa ya wananchi kama ilivyokuwa wakati wa kuanzishwa mfumo wa vyama mwaka 1992.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk. Steven Munga, alisema umefika sasa wa serikali kuona mabadiliko ya Katiba ni sehemu ya maisha ya wananchi.
“Jamii imebadilika, mfumo wa maisha umebadilika… sasa ni wazi kwamba Katiba iliyopo nayo lazima ibadilike, serikali ifikie hatua ikubali jambo,” alisema Askofu Munga.
Alisema watu wasiposikilizwa kilio chao kukiwa na amani, wanaweza kuleta mabadiliko ya lazima ambayo yanaweza kuchochea ghasia zisizokuwa na msingi wowote.
“Nakwambia mwandishi kama watu hawakusikilizwa katika mazingira ya amani… wanaweza wakasikilizwa ndani ya mazingira machafuko ambapo hakutakuwa na maelewano kabisa, tunasema hatutaki vita sisi, suala hili haliepukiki hata kidogo,” alisema Askofu Munga.
Alisema mabadiliko yaliyofanyika Zanzibar na kuiweka serikali ya umoja wa kitaifa, yanaonyesha wazi kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano lazima ifanyiwe marekebisho.
“Mtakumbuka kule Zanzibar kumefanyika mabadiliko ambayo yameondoa vyeo kama vile Waziri Kiongozi ambaye alikuwa anatambulika vyema ndani ya Katiba, sasa iweje Katiba ya Jamhuri isifanyiwe marekebisho? Alihoji Askofu Munga.
Naye Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Bukoba, Methodius Kilaini, aliwataka wanasiasa kuorodhesha mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye mabadiliko hayo, kisha wayapeleke kwao ili nao waongeze nguvu ya mabadiliko.
“Sisi tunawategemea sana wanasiasa watwambie maeneo ambayo yana upungufu, waorodheshe walete kwetu, tutawasaidia kuchochea hili kwani haliepukiki hata kidogo,” alisema Askofu Kilaini.
Akitoa mfano alisema, nchi kama Zambia, Malawi Kenya wapinzani waliingia madarakani kisha kubadilisha Katiba, hivyo hata Tanzania inawezekana.
Naye Askofu wa Kanisa la GRC la Ubungo Kibangu, Antony Anthony Lusekelo, alisema Katiba mpya lazima ipatikane kwa serikali kuhakikisha inafuata utaratibu wa kushirikisha wananchi kutoa mapendekezo yao.
Alisema kipindi hiki ni muhimu kuwa na Katiba itakayokuwa na mawazo ya kila mdau, kama ilivyokuwa kipindi cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, ambapo hakuna madhara yaliyojitokeza kwani kila mwananchi alishirikishwa.
“Lazima tuone mbali na serikali ione hilo… ni muhimu katika hili kuhakikisha kunakuwa na mjadala mpana utakaoshirikisha watu wote kama ilivyotokea kipindi cha vyama vingi ambapo kila mwananchi alishirikishwa,” alisema Askofu Lusekelo.
Alisema kama Katiba ikipatikana kwa amani, hakutakuwa na madhara, lakini iwapo serikali itapuuza matakwa ya wengi kuna uwezekano wa Katiba kuleta maafa jambo ambalo halipendezi hata kidogo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT), David Mwasota, alisema suala hilo hivi sasa halina mjadala hasa kwa jamii yenye akili timamu.
Alisema Katiba iliyopo haikuweka ili idumu milele, bali ilitungwa kipindi ambacho hakukuwa na uanzishwaji wa vyama vingi.
“Hao wanaokataa mabadiliko ya Katiba, wana maslahi yao binafsi, lakini kwa watu walio na maono ya mbali ni lazima ibadilike maana hii iliyopo inakipa nguvu chama kimoja, wakati tuko ndani ya mfumo wa vyama vingi,” alisema Mwasota.
Naye Mtume Prosper Ntepa, alisema Katiba si mama wa chama tawala pekee, bali ni kwa ajili ya kusaidia jamii nzima hivyo ni muhimu serikali ikasikiliza kilio hicho ili kuhakikisha kinakidhi mahitaji.
“Serikali isipuuze kilio cha wananchi maana ni kilio halali na kimekuja kipindi husika; ni lazima Katiba ibadilishwe bila kuhofu hasa kwa wale wote wanaoitakia mema nchi na wapenda demokrasia,” alisisitiza Ntepa.
Hivi karibuni viongozi mbalimbali walijitokeza kueleza msimamo wao kuhusu kubadilishwa kwa Katiba, akiwemo Mwanazuoni na mwanaharakati mashuhuri nchini, Profesa Issa Shivji, Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.
Mkapa ambaye alivunja ukimya na kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania. Wakati viongozi mbalimbali wakionyesha nia ya kuhitaji mabadiliko ya Katiba, hivi karibuni Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichopingwa na watu wengi. Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwa vile serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.
 
nilijua tu mada ya hovyo kama hii itakuwa imeanzishwa na wewe Malaria Sugu
 
It's a shame we still call JF a home of great thinkers!!!! perhaps Tinkers should be right word!!
 
Mh LIPUMBA 95 HADI 2005 alikuwa mkali sana na aliomba watz wamunge mkono kudai katiba mpya,lkn wanaharakati wa tz ambao tayari ofisi zao zilikuwa wazi. zilikaa kimya, zilifumba macho na kuona hakuna umuhimu wowote ule.Wakati ule ambapo rais alikuwa mh Mkapa, mashirika ya dini hayakuona umuhimu wa katiba mpya. hakuna aliehoji umuhimu wa katiba mpya, na wengine walikuwa wakali wakisikia wtu wanataka katiba mpya. lkn mara tu baada ya dk slaa kushindwa na kulalalmika huku wabunge wa chadema wakitoka Bungeni . sasa wanaharakati na viongozi wa dini wamekuja na mkakati huu wa katiba mypa chini ya Utawala wa JK, wale waliokuwa wanaona hakuna haja ya katiba mpya ndani ya utawala wa Mh mkapa ndio hawa wanaotakla mabadiliko wakati wa JK

Mpumbavu mkubwa wee!
Fikiria impact ya maneno unayoanzisha!...
Nilishauliza huwa unalipwa bei gani kwa kazi-bure hii?
 
Tatizo la ndugu yangu Comrade Malalria Sugu ni kuwa haijui historia ya kudai katiba mpya.............vuguvugu za kudai katiba mpya ndiyo ziliisukuma serikali kuitia viraka 15 katiba hii iliyopo ya mwaka 1977...........Kumbuka government white paper wakati wa Mzee Rukhsa.........Muislamu mwenzio.....................hili hakuna udini ......mbona akina Profesa Karim Hirji wa Muhimbili jana alidai katiba mpya..........na huo ni udini ....................Je Profesa Shivji naye sasa wataka kumwita msaliti wa waislamu?

Na hawa je wataka kusema nao hakuna waislamu kwenye kudai katiba mpya?

Kongamano la Katiba leo


na Betty Kangonga


amka2.gif
WANANCHI pamoja na viongozi wa vyama vya siasa nchini wanatarajia kukutana kesho kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayoendelea nchini likiwemo na suala la Katiba Mpya.
Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa mkutano huo, Ibrahim Mwambuja, alisema wamealika watu zaidi ya 50 kuhudhuria mkutano huo.
Alisema wamefikia hatua hiyo, baada ya kuona kuna masuala muhimu yanayohitajika kujadiliwa ili kuhakikisha yanapatiwa ufumbuzi wa kudumu hasa katika suala la upatikanaji wa Katiba mpya ambayo itasaidia kuleta utatuzi.
Alisema viongozi wa vyama vya siasa pamoja na vyama vya kiraia, vitakavyoshiriki watahakikisha wanajadili pia masuala yanayohusu siasa, uchumi na jamii ili kuwawezesha wananchi kuwa na uelewa na kuweza kufikia malengo.
"Katika mkutano huo hatutakuwa na mgeni rasmi bali vyama vya siasa na vile vya kiraia vitajadili masuala yanayoendelea kwa sasa yakiwemo la Katiba, siasa, uchumi na jamii kwa ujumla," alisema.
Alisema hakuna kiingilio katika mkutano huo, bali wananchi wote wanaohitaji kuhudhuria wanakaribishwa ambapo wanategemea kuanza majadiliano hayo majira ya saa 8 mchana.


Malaria Sugu........tatizo lako huielewi historia ya nchi hii...na ndiyo maana hoja za JK za udini zisizo na mashiko umezishupalia.......................when will you learn to be your own man and stop being a JK surrogate soldier and stand for the truth for the benefit of the posterity?
 
Sugu, hebu tulia kidogo kwani ninalo jambo la muhimu sana kwa maisha yako hapa. Huu ni ushauri wa bure kwako.

Ukitaka kufurahia mijadala yoyote hata na mkeo chumbani kwenu, jitahidi saaaannnaaa kutokua na MAJIBU KICHWANI hata kabl mwenzio hajaongea. Pindi utakapojizoelesha na kawaida hii watu wengi watapenda sana ushiriki wako nao katika maongezi na wala si vinginevyo.

Kwa upande wa Mhe Prof Lipumba na madai yako, s kweli kwamba hatuna jibu sahihi la kukupa hapa. Hivi kweli hata wewe hapo mkutano unapoanza na kwanza unasikia tu maneno 'TAKHBIR' (maneno ambayo nayaheshimu sana wenzangu mnapoyatumia katika nyumba zenu za ibada), sasa nimekuja kwenye mhadhara wa kisiasa ili nikasikilize sera na kujiamulia mra TAKHBIR inatawala kote hewani na wala nisisikie Prof mwenyewe akikemea hilo sasa unataka na mimi niibuke na YESU WANGU hapo hapo hoja fulani ikiniingia uzuri baadaye unategemea nini kutoka kwa wale wanaosimama karibu na mimi ambao ndio wengi sikuzote kwenye mihadhara ya Mhe Lipumba???

Hakuna aliyekataa kumunga mkono katika kudai katiba isipokua ni yeye mwenyewe ndio alitufanya TUJIHISI HATUKO KATIKA MIHADHARA SAHIHI KWETU kamwe. Tena pale mlipoibuka na sera ya 'Jino kwa Jino' ndio kabisa binafsi nilikua sithubutu hata kumtuma mtoto dukani mnapokua na mikutano maeneo. Sasa hili la kumunga mkono kudai katiba mpya mwenzangu tungekutania wapi wakati hata mikutano yake tayari alishatupiga marufuku kimtindo??

Sasa na mimi pia nikuulize swali hapo hapo; je Prof Lipumba alikua akidai katiba mpya kwa sababu Rais wa wakati huo alikua ni MKRISTO na wala si kwamba alikua anasukumwa maswala fulani ya msingi kwa Wa-Tanzania wote kwa ujumla wetu sio???? Eeehhhh, naona Sugu hapa ndipo ninakokupendea siku zote kuleta sebuleni yale ya chumbani!!! Kumbe ndio maana tangu sera ya CUF Jino kwa Jino tangu igeuke CUF-CCM-Ufisadi DENDA YA KISIASA ya 'Ulimi kwaUlimi' midomoni mwao wala Prof Lipumba hapati hamu tena ya kudai katiba kwa sababu Raisi kipenzi ni wa dini yake eeeehhhh?????

Kama hilo ndilo jibu basi wala sitokaa nishangae mtu kichwa kama Lipumba aliyesaidia kukwamua uchumi wa Uganda ikasimama na kungara iweje hapa nyumbani anageuka a CAREER PRESIDENTIAL CANDIDATE wa kiti cha urais ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania!!!!! Nadnani wala nisikuchoshe na swali nyingine zaidi kama yeye na Maalim Seif Shariff Hamad watakwemo (Mungu naomba uwajalie afya njema) katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu 2015 au hapana.
 
Mpumbavu mkubwa wee!
Fikiria impact ya maneno unayoanzisha!...
Nilishauliza huwa unalipwa bei gani kwa kazi-bure hii?
hehehe!
naona braza umekasirika kidogo hapo:nerd::nerd:
 
Huyu Agustino ni mnafiki sana - kwa nini kesi za kuvunja katiba anasema ni za kisiasa na kuzitupia kwenye Bunge?
 
Malaria Sugu, hebu tulia kidogo kwani ninalo jambo la muhimu sana kwa maisha yako hapa. Huu ni ushauri wa bure kwako. Usichanganye itikadi za kidini na madai ya Katiba mpya please!!

Ukitaka kufurahia mijadala yoyote hata na mkeo chumbani kwenu, jitahidi saaaannnaaa kutokua na MAJIBU KICHWANI hata kabl mwenzio hajaongea. Pindi utakapojizoelesha na kawaida hii watu wengi watapenda sana ushiriki wako nao katika maongezi na wala si vinginevyo.

Kwa upande wa Mhe Prof Lipumba na madai yako, s kweli kwamba hatuna jibu sahihi la kukupa hapa. Hivi kweli hata wewe hapo mkutano unapoanza na kwanza unasikia tu maneno 'TAKHBIR' (maneno ambayo nayaheshimu sana wenzangu mnapoyatumia katika nyumba zenu za ibada), sasa nimekuja kwenye mhadhara wa kisiasa ili nikasikilize sera na kujiamulia mra TAKHBIR inatawala kote hewani na wala nisisikie Prof mwenyewe akikemea hilo sasa unataka na mimi niibuke na YESU WANGU hapo hapo hoja fulani ikiniingia uzuri baadaye unategemea nini kutoka kwa wale wanaosimama karibu na mimi ambao ndio wengi sikuzote kwenye mihadhara ya Mhe Lipumba???

Hakuna aliyekataa kumunga mkono katika kudai katiba isipokua ni yeye mwenyewe ndio alitufanya TUJIHISI HATUKO KATIKA MIHADHARA SAHIHI KWETU kamwe. Tena pale mlipoibuka na sera ya 'Jino kwa Jino' ndio kabisa binafsi nilikua sithubutu hata kumtuma mtoto dukani mnapokua na mikutano maeneo. Sasa hili la kumunga mkono kudai katiba mpya mwenzangu tungekutania wapi wakati hata mikutano yake tayari alishatupiga marufuku kimtindo??

Sasa na mimi pia nikuulize swali hapo hapo; je Prof Lipumba alikua akidai katiba mpya kwa sababu Rais wa wakati huo alikua ni MKRISTO na wala si kwamba alikua anasukumwa maswala fulani ya msingi kwa Wa-Tanzania wote kwa ujumla wetu sio???? Eeehhhh, naona Sugu hapa ndipo ninakokupendea siku zote kuleta sebuleni yale ya chumbani!!! Kumbe ndio maana tangu sera ya CUF Jino kwa Jino tangu igeuke CUF-CCM-Ufisadi DENDA YA KISIASA ya 'Ulimi kwaUlimi' midomoni mwao wala Prof Lipumba hapati hamu tena ya kudai katiba kwa sababu Raisi kipenzi ni wa dini yake eeeehhhh?????

Kama hilo ndilo jibu basi wala sitokaa nishangae mtu kichwa kama Lipumba aliyesaidia kukwamua uchumi wa Uganda ikasimama na kungara iweje hapa nyumbani anageuka a CAREER PRESIDENTIAL CANDIDATE wa kiti cha urais ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania!!!!! Nadnani wala nisikuchoshe na swali nyingine zaidi kama yeye na Maalim Seif Shariff Hamad watakwemo (Mungu naomba uwajalie afya njema) katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu 2015 au hapana.
 
Mh LIPUMBA 95 HADI 2005 alikuwa mkali sana na aliomba watz wamunge mkono kudai katiba mpya,lkn wanaharakati wa tz ambao tayari ofisi zao zilikuwa wazi. zilikaa kimya, zilifumba macho na kuona hakuna umuhimu wowote ule.Wakati ule ambapo rais alikuwa mh Mkapa, mashirika ya dini hayakuona umuhimu wa katiba mpya. hakuna aliehoji umuhimu wa katiba mpya, na wengine walikuwa wakali wakisikia wtu wanataka katiba mpya. lkn mara tu baada ya dk slaa kushindwa na kulalalmika huku wabunge wa chadema wakitoka Bungeni . sasa wanaharakati na viongozi wa dini wamekuja na mkakati huu wa katiba mypa chini ya Utawala wa JK, wale waliokuwa wanaona hakuna haja ya katiba mpya ndani ya utawala wa Mh mkapa ndio hawa wanaotakla mabadiliko wakati wa JK

kwa hiyo, unataka kuwaambia watanzania kwamba, Lowassa alipojiuzuru Uwaziri Mkuu na Mkapa kushambuliwa sana kuhusu sakata la Kiwira ilikuwa ni mpango wa dini moja kuingusha dini nyingine? Hizi ni fikra dhaifu za kale kabisa enzi za zama za mawe za kati.

Katiba si kitabu cha dini fulani ni kitabu cha watanzania wote, kilikuwepo, kipo na kitaendela kuwepo. Marekebisho ya katiba au katiba mpya ikikubarika itaendelea kuwepo hata baada ya Rais wa dini moja kuondoka Ikulu na kuingia Rais wa dini nyingine kadri watanzania watakavyoona inafaa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imerekebishwa mara 14 wakati huo wote haikuwa suala la dini moja bali mahahitaji ya wakati.

Je, Malaria Sugu unataka kusema katiba ya sasa ni ya dini fulani hadi unaogopa kwamba kilichopo ndani yake hakizungumziki na kikiguswa ni sawa na kugusa msahafu? nini kinakutia hofu kuiboresha katiba ambayo Rais aliopo madarakani aliikuta imeandaliwa na serikali ya awamu ya kwanza chini ya Rais Mkristo. Leo hii wanaohoji kuhusu katiba hiyo, unaona wanapinga uislamu ni mawazo mgando.

Sina uelewa mkubwa sana katika mambo ya katiba, sijui niunge mkono kundi lipi kati ya linalodai katiba mpya au linalopinga katiba mpya lakini baada ya kueleweshwa na kuelewa niko tayari kuunga mkono mtazamo wa moja ya makundi hayo mawili.
 
haya mimi mpumbavu ndio nikawa jf. Lkn swala la katiba mpya limeanza wakati gani? Na kwnini?
ok, jee haya mashirika ya dini mbona yalikuwa kimya kuhusu kudai katiba mpya hata ya zanzibar? Miaka nenda miak a rudi hadi znz wenyewe walipoamua?HATA MATAIFA YA NJE YALIONA UMUHIMU WA KATIBA HIYO. LKN WALIKAA KIMYA. Jee mbona yanaibuka sana kwa kasi hii.
Taarifa zako hizi ndugu yangu mpendwa Malaria Sugu hazina ukweli wowote ule kwenye historia ya nchi hii.....wewe tafsiri yako ni kuwa wanampinga JK lakini ukumbuke ya kuwa waliotupotosha ya kuwa JK ni chaguo la Mwenyezi Mungu ni hao hao Viongozi wa madhehebu ya kikristu wakiongozwa na mbabaishaji Askofu Kilaini..................

Kumbuka pia suala la vuguvugu ya kudai katiba mpya kamwe halitahatarisha ajira ya JK ya Uraisi kwa miaka mitano......ijayo...............na katiba mpya kama ikipitishwa itatugusa sote kwa miaka zaidi ya mitano ya JK ambayo yaelekea inakupa homa ya kuandika makala hii..........JK kama waliomtangulia ataondoka kipindi chake kikiisha kama Mola hatamtanguliza mapema kwenye hukumu hususani tukuzingatia jinsi anavyodondoka dodonka kila mahali.....................yaashiria hayuko mbali na mauti........................................

Pengine hata hii miaka mitano huenda asiimalize................ila namwombea JK wa Malaria Sugu bukheri wa afya.....................
 
Back
Top Bottom