Maendeleo ya afya ya Profesa Jay

Maendeleo ya afya ya Profesa Jay

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Baada ya ukimya wa siku kadhaaa, taarifa kutoka kwa watu wa karibu na msanii wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ni kuwa anaendelea vizuri kiafya tofauti na ilivyokuwa wiki iliyopita.

Hakuna mwanafamilia ambaye amejitokeza kuweka hadharani zaidi ya taarifa za awali ambazo zilieza Jay ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Mikumi, alipoanza kuugua alipelekwa katika hospitali mitaa ya Tegeta, akahamishwa kupelekwa Lugalo na baadaye akahamishiwa Muhimbili ambapo ndipo alipo hadi sasa.

Wasanii mbalimbali wamekuwa wakijitokeza hadharani kumpa pole licha ya kutoweka wazi nini hasa ambacho kinamsumbua.
 
Apone haraka
Hii Taarifa Ikisomwa Inaonekana Ina Pictures Ila Hatuioni
 
Figo wanasema zilifeli, Mungu amsaidie maana wengine figo zikifeli unakuwa mtihani mkubwa.
 
Dawa zetu za kiume ndio shida kwa wengi.
 
Mungu ampe afya njema Pro J.

Serikali ya CCM imejitahidi sana kuiboresha hospitali ya Muhimbili kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu mazuri na ya uhakika.

Au mnasemaje ndugu zangu wana JF.
 
duh mnajua exactly anaumwa nini wakati hakuna hata aliyepewa taarifa sahihi na either familia ama mkewe? speculating thinkers
 
Huenda ni miongoni mwa wanafamilia pia..
 
Nitajihisi nimetenda dhambi kubwa kama nitashindwa kumchangia japo kidogo nilichonacho my legend, the best to ever do..., Leo naahidi kabla sijalala nitakuwa nishamchangia
 
Pamoja sana
 
Wameona nimekonda ghafla wakasema naumwa ukimwi .....ayo kayaimba mwemyew nawakumbusha tu ARV ukitumia kwa mda mrefu zinaharibu figo
 
Barikiwa sana
 
Wengi wametumia zaidi ya miaka kadhaa na hawana tatizo la figo
 
Baada ya ukimya wa siku kadhaaa, taarifa kutoka kwa watu wa karibu na msanii wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ni kuwa anaendelea vizuri kiafya tofauti na ilivyokuwa wiki iliyopita.

Hakuna mwanafamilia ambaye amejitokeza kuweka hadharani zaidi ya taarifa za awali ambazo zilieza Jay ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Mikumi, alipoanza kuugua alipelekwa katika hospitali mitaa ya Tegeta, akahamishwa kupelekwa Lugalo na baadaye akahamishiwa Muhimbili ambapo ndipo alipo hadi sasa.

Wasanii mbalimbali wamekuwa wakijitokeza hadharani kumpa pole licha ya kutoweka wazi nini hasa ambacho kinamsumbua.
Get well soon mbunge mstaafu
 
Nitajihisi nimetenda dhambi kubwa kama nitashindwa kumchangia japo kidogo nilichonacho my legend, the best to ever do..., Leo naahidi kabla sijalala nitakuwa nishamchangia

You took the words out of my mouth. Nilisema lazima nimchangie Prof. Tumekulia mziki wake.
 
Back
Top Bottom