mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729
MAENDELEO YA UJENZI WA SGR: "Vituo vya Reli hii ni vya kisasa na siyo kwaajili ya kushusha na kupandisha abiria pekee bali itakua ni sehemu ya biashara na huduma za kijamii zikiwemo za kibenki na 'Supermarkets' hali itayosaidia TRC kuongeza mapato yake," Mkurugenzi Mkuu TRC, Masanja Kadogosa
Aidha Kadogosa amesema mradi huu wa ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro umefikia asilimia 77 na Morogoro hadi Makutopora ya Singida umefikia zaidi ya asilimia 30.
Mkurugenzi Mkuu, Masanja Kadogosa ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anayeendelea kukagua ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa alipowasili katika Kituo cha Soga, Pwani na kisha kupanda treni hiyo ya kisasa ya majaribio kuelekea Kilosa Morogoro.