Uchaguzi 2020 Maendeleo ya watu ndiyo Sera inayakubalika sasa. Je, kodi zetu ndio zimejenga barabara, reli na kununua vitu vilivyotuacha hohehahe?

Uchaguzi 2020 Maendeleo ya watu ndiyo Sera inayakubalika sasa. Je, kodi zetu ndio zimejenga barabara, reli na kununua vitu vilivyotuacha hohehahe?

USA wamejenga kwa miaka 250 nyie mnataka mjenge kwa miaka mitano huku mnapigamo na 10% za kumwaga. Msitufanye wajinga sisi.
Kwa sababu USA imejenga barabara kwa miaka 250 mkulima wa pamba, korosho, kahawa nk asubiri hiyo miaka ndiyo aweze kusafirisha mazao yake kwenda kwenye masoko? Je, huyu mkulima atapata wapi kipato cha kumudu maisha yake? Unajifanya hamnazo au ndio ukweli?
 
Hivi Kuna nchi gani hapa duniani watu wameendelea bila kuwa na vitu,

Yaani unakuta hakuna hospitali, hakuna bara bara, hakuna madaraja, hakuna hata usafiri wa ndege lakini wananchi wote Wana PHD na fedha zimejaa kwenye akaunti zao, nitajie.

Ni nchi nyingi sana maendeleo huanzia kwa watu kisha watu wakajenga vitu
Huwezi kujenga bila kuwa na maendeleo
 
Ni kutokujielewa tu. Yakiletwa maendeleo ya watu mleta uzi atasema mbona hakuna maendeleo ya vitu.

Ujerumani ya Hiltler ilijenga Treni za umeme nchi nzima, leo hii mtu anaishi Hamburg na biashara zake anafanyia Ulm. Ni sawa mtu aishi Pangani Tanga halafu biashara zake anafanyia Mtwara mjini.

Wanaoishi mijini huwa na ubinafsi wa kudhani a kwamba maisha yao ni muhimu wakisahau kuwa Tanzania ni kubwa sana na kila eneo lina mahitaji muhimu.
 
Ni nchi nyingi sana maendeleo huanzia kwa watu kisha watu wakajenga vitu
Huwezi kujenga bila kuwa na maendeleo

Mkuu zigii, inaanza kujenga miundo mbinu halafu ndio uchumi wa mtu mmoja mmoja unajengwa.

Vitu ndio vinavyochagiza maendeleo ya watu..zinajengwa nguzo za makampuni ya simu ndipo watu wanaweza kutumia simu za mkononi katika eneo husika.

Zinajengwa reli za kisasa ndipo watu wanaweza kusafirisha mazao na kuyafikisha bandarini Dar.

Ni akili ya kawaida tu.
 
Wanabodi,

Wananchi hawashibi barabara, ndege, madaraja au hospitali. Wananchi wanahitaji chakula na pesa mwaka huu 2020. Hili chama changu cha CCM ndio tunapaswa kulihubiri kwenye kampeni sasa"Maisha bora na maendeleo ya watu"....
Unajua fika kuwa unapotosha. Unaweza email kusema Barabara hazimsaidii mtanzania wa kawaida?

Umeshindwa tayari
 
Kwani hiyo ni ndege ya ATC mnazotusimanga nazo kama kwamba ela yake ya manunuzi zimetoka mifukoni mwenu??!!.

haahaha kwahio mmebadilisha mada saaahv, mlikua mnasema ndege hazina umuhimu saaahv mnasema ndege za atcl, kazi kweli kweli kwenye hio saccoss
 
Mkuu zigii, inaanza kujenga miundo mbinu halafu ndio uchumi wa mtu mmoja mmoja unajengwa.

Vitu ndio vinavyochagiza maendeleo ya watu..zinajengwa nguzo za makampuni ya simu ndipo watu wanaweza kutumia simu za mkononi katika eneo husika.

Zinajengwa reli za kisasa ndipo watu wanaweza kusafirisha mazao na kuyafikisha bandarini Dar.

Ni akili ya kawaida tu.

Mkuu ni sawa useme keti ya yai na kuku kipi hutanguli? Huwezi kujenga nguzo za simu au vyote vyote vile bila kuwa na hela ya kununua simu watu kama hawana hela nguzo zitakua ni asara tu vyote hivi vinategemeana treni ikiwepo watu wakakosa hela ni hasara mfano mdogo haya madege watu hawayapandi kwa sababu hawana hela
Mlishe ngombe upate maziwa
 
Vitu ni lazima viwepo ili maendeleo ya watu yaweze kurahisishwa.
Hatua ya kujenga vitu kwa mataifa makubwa waliipita miaka mingi wakati walipokuja kututawala.
Sisi ni lazima tuipite na hatuwezi kuikwepa hata tukijidanganya lakini ukweli ndio huo.
 
Mkuu tusibishane sana kuhusu hili nijuavyo mm ni kwanza uchumi mzuri kwa watu kisha kwa vitu hata ulaya walianza kuwatoa watu njaa kisha wakaja kwenye vitu mkoloni alijenga reli baada ya kuona mazao ya kusafirisha yapo
 
Tatizo wanaoongea vitu kwanza ni watu wa mijini tu waliozoea maisha ya kujikimu pasipo kuiangalia Tanzania kwa mapana yake.

Serikali inaponunua mbolea nzuri na kuwapatia wakulima inakuwa imeboresha vitu ili watu wapate chakula Kingi siku za usoni.

Unapojenga reli unakuwa umemuwezesha mkulima kutoa mazao bara na kuyafikisha bandarini, ni maendeleo ya vitu kwa faida ya watu.

Wafanyabiashara wa minofu ya samaki wanapoitumia ndege kupeleka mizigo Ulaya wanakuwa ni watu wanaofaidika na maendeleo ya vitu.

Watanzania walipokwama India wakati wa corona walifuatwa na Air Tanzania..maendeleo ya vitu yakaokoa watu.

Ubinafsi ndio unatufanya kutotazama umuhimu wa maendeleo ya vitu.
 
Back
Top Bottom