Maeneo 479 yasiyofikiwa na miundombinu yamepatiwa umeme

Maeneo 479 yasiyofikiwa na miundombinu yamepatiwa umeme

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
MAENEO 479 YASIYOFIKIWA NA MIUNDOMBINU YAMEPATIWA UMEME

Mradi wa Kusambaza Umeme katika Vijiji na Miji Awamu ya Tatu (Peri Urban III) unalenga kusambaza umeme katika vijiji-miji, mitaa, na vitongoji 508 ambavyo havijafikiwa na miundombinu ya umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji.

Mradi huu utaenda katika mikoa nane (8) ya Geita, Kigoma, Kagera, Mbeya, Mtwara, Singida, Tabora na Tanga na unahusisha ujenzi wa njia za umeme wa msongo wa kati zenye urefu wa kilomita 379, ujenzi wa njia za umeme wa msongo mdogo zenye urefu wa kilomita 753, ufungwaji wa transfoma 314 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 16,369.

Hadi kufikia mwezi Aprili 2025, maeneo 479 kati ya 508 sawa na asilimia 94 yamefikiwa na umeme na wateja 14,864 kati ya 16,369 sawa na asilimia 91 wameunganishiwa huduma ya umeme.

 
Back
Top Bottom