Maeneo Bora kwa Kijana wa Miaka 18 Hadi 25 Kuwekeza

Maeneo Bora kwa Kijana wa Miaka 18 Hadi 25 Kuwekeza

Ni maeneo yapi yenye fursa kubwa zaidi ya kuwekeza kwa kijana wa miaka 18 hadi 25? Na ni kwa nini sehemu hizi zinachukuliwa kuwa bora kwa uwekezaji kwa vijana?
Hakikisha unapanga mipango ya miaka mi5 mbele,yani lzima utafika tu,so usiangalie return ya miezi 6 mbele,angalia return ya kuanzia moaka mi5 mbele.

Usijali na walausione miaka mi5 mbele ni mingi,kwani kama una miaka 18 basi the next 5yrs utakuwa na miaka 25 yaani bado ni kijijana.


Na kama una miaka 25 basi the nect 5yrs utakuwa na miaka 30 yaani bado ni kijana,so ni muhimu sana kwa kijana kuwa na mipango ya miaka mi5 hadi 10 mbele.

Vijana wengi hatuna consistency ya kusubiri na kufanya jambo kwa muda mrefu kama huo na ilhali tunajua kabisa kwamba tuna malengo ya kuwa hai mpaka muda huo na tunatarajia tutafika.

So kam tunaamini tutafika miaka 10 mbele bas ni kwa nini hatuna mipango iliyotarget muda wa miaka 10 mbele ?

Sasa ni muda wa vijana kubadilisha akili na kuanza kuwa na mipango ya muda mrefu.

2.kama kijana hakikisha unadumu na biashara moja na naijua vyema,biashara yoyote itaanza kukulipa pale ambapo utakapokuwa mjuzi wa biashara hiyo.

Hata gari itaanza kukulipa ama kukufikisha unapopataka pale ambapo utakuwa unajua kuendesha gari hiyo,hivyo usikate tamaa.

3.hakikisha unatafuta Urafiki na wafanya biashara,yani weka mikakti ya kutengeneza urafiki wenye tija na wafanyabiashara wenzako,hiyo itakuongezea connection na pia utakuwa umezungukwa na watu ambao wa aina yako.

4.hakikisha unasoma makala au vitabu vinavyohusiana na jambo unalojishughulisha nalo,usikubali kuwa layman kwenye kitengo chako.

Kama ni nyanya unalima basi hakikisha unatafuta makala zinazozungumzia ardhi na tabbia zake ama aina zake,soma sana kuhusu nyanya na sifa zake kulingana na ardhi n.k yaani kuwa mfukunyuku.

Katika kufanya hivyo kuna detail fulani ambayo inaweza kukutoa kimaisha kutokana na ulivyosoma.
 
Pia ni muhimu ktk umri huo kijana asiangalie zaidi kuhusu PESA bali ujuzi zaidi. Awe tayari kujitoa zaidi kupata Skills ambayo baadae itamletea Pesa mingi sana.

Imagine mtu kajifunza Ufundi garage au kuendesha mitambo flani, then akafanya hiyo kazi consecutively kwa miaka 5 tu atakua ame master kwa kiwango gani.
 
Kama utaweza weka nguvu kwenye uzalishaji...
....
Hii nchi Bado production Iko chini sana...usihangaike na Gucci au kukimbilia china, wewe ruhusu tuu Kila mtanzania akuchangie gharama za uzalishaji......
Just consider the four factors of production
Land, labour, entrepreneurship skills and capital

Utakuwa mo au bakhresa, ni utani tuu unaouma...
Nimekuelewa mkuu 👍👍👍
 
Biashara ya unenepeshaji ng'ombe
Hapa kijana atakuwa anatafuta ng'ombe waliokondeana na kwenda kuwanenepesha na kuwauza na life kusonga
Hii unaweza kuajiri mtu asifanye lakini si mpaka upate darasa la Chakula Bora chenye nutrition. Kinanunuliwa special au unatengeneza?
 
Labda hapa nichangie kidogo. Vijana wengi katika umri huu huwa hawana utambuzi wa kujitambua na hucheza sana na maisha. Wanapata fursa, lakini hawana uelewa wa kuzitumia. Huu ndio umri wa moto.

Kama unaweza, wekeza katika uhusiano wako na Mungu. Uhusiano huu utakupa nidhamu, ambayo ni muhimu sana kwa mafanikio.

Pili, kama unasoma, wekeza kwenye elimu yako. Soma kwa bidii. Elimu ni muhimu sana ikiwa uko katika nafasi ya kusoma.

Tatu, jifunze kuhifadhi pesa. Anza kuwa na tabia ya kuweka akiba; utajishukuru sana ukiwa na miaka 30. Usije ukachezea pesa zako zote kwa pombe na wanawake. Vijana wengi katika umri huu hawana majukumu na hutumia pesa nyingi kwenye klabu na burudani. Ni kawaida sana kutumia laki moja au mbili kwa usiku mmoja.

Kuhusu akiba, tafuta saccos yenye sifa nzuri, fuata taratibu za kujiunga, na lipa ada za uanachama ili uwe mwanachama. Hii ni nzuri sana kwa kijana. Riba za saccos ni ndogo sana na unaweza kukopa mara 2 au mara 3 ya mtaji wako. Hii inaweza kukusaidia baadaye kama unapenda biashara. Ukiweka akiba kwa kuendelea, hata 10% ya kipato chako inatosha. Kwa mfano, ukiingiza laki 5, weka akiba elfu 50. Uwe mwaminifu na hii, na kwa muda mrefu itakulipa sana.

Nne, anza kujifunza biashara kwa kufanya biashara. Kumbuka, utaanza biashara na nyingi zitakufa mwanzoni. Ni kama kujifunza kuendesha baiskeli; utaanguka mara nyingi mwanzoni, lakini ukishajua, ni nadra sana kuanguka tena. Anzisha biashara unayoipenda na pambana nayo. Ikifa, utapata somo ambalo litaingia akilini vizuri sana. Unajifunza kwa njia ngumu.

Si lazima biashara ife au zife, lakini ikitokea, ni kawaida sana. Biashara haihitaji waganga, usiende kwa waganga. Ukishazoea biashara, utafurahia mwenyewe.
Well said 👏👏👏
 
Hii unaweza kuajiri mtu asifanye lakini si mpaka upate darasa la Chakula Bora chenye nutrition. Kinanunuliwa special au unatengeneza?
Kulingana na mtaji wa muwekezaji,soko na pia upatikanaji wa malighafi ya kutengenezea chakula na pia nyasi na vingine vya muhimu
 
ULIZA KUPITIA CHAT GPT
Sometimes we need to think rather than depending on Chat GPT kwakuwa JamiiForums ipo let us use it na kufanyia kazi mawazo ya watu mbalimbali Chat GPT ni extra tu ila mawazo ya watu yana nguvu than this machine.
 
Kulingana na mtaji wa muwekezaji,soko na pia upatikanaji wa malighafi ya kutengenezea chakula na pia nyasi na vingine vya muhimu
Hali kwenye soko ndo nakutana na madalali tena? Unauzoefu na hii project? Naweza ajiri mtu na nikapata matokeo mazuri. Isiwe kama kilimo Cha kwenye simu
 
Katika kukuza mtaji,inategemea vyanzo vya kipato chako ni vikubwa au vidogo kiasi gani.
Tafuta kikundi cha vikoba,watu waaminifu,mara nyingi wanaweka hisa kwa wiki.
Hii itakujengea nidhamu ya kuweka akiba, utaruhusiwa kukopa mara 2 ya hisa zako endapo una wazo la biashara ya kufanya,kama hutalazimika kukopa,mwisho ya mwaka utajikuta una angalau milioni moja.
Hii unaweza kuiweka UTT ambapo itakuwa inakuzalishia almost elfu kumi kila mwezi,
Na huku unaendelea na vikoba yako,baadae utajikuta una mtaji wa kuanzisha biashara.
 
Nyanya masika zitamsumbua sana, ila akifuzu atapata pesa nzuri.
Mi naona vitunguumaji ndio afadhali
Kuna mwana kapata mtaji wa mil10 kiutani tu masika alilima akaotea bei ya laki 2.5 then sahivi anafanya biashara ya mahindi
 
Mi naona vitunguumaji ndio afadhali
Kuna mwana kapata mtaji wa mil10 kiutani tu masika alilima akaotea bei ya laki 2.5 then sahivi anafanya biashara ya mahindi
Kupata mtaji wa biashara ni changamoto mtu unashindwa uanzie wapi kwenye kilimo, kuajiriwa, biashara ndogondogo, bodaboda watu wengi wangefanikiwa kwenye mambo mbalimbali ila tatizo mtaji unatukwamisha sana.
 
Hii unaweza kuajiri mtu asifanye lakini si mpaka upate darasa la Chakula Bora chenye nutrition. Kinanunuliwa special au unatengeneza?
Actually nahisi atasaidia ng'ombe kunenepa kwa uharaka na kutengeneza faida kubwa kwa muda mfupi
 
Back
Top Bottom