Kuna maeneo fulani nimepita ya mkoa wa dodoma wilayani huko; nimekuta kuna msururu mrefu sana wa vyombo vya moto kwenye moja ya petrol station. Nikajaribu kuuliza kuna shida gani hapa? Wenyeji wanasema mafuta ya petrol hamna kabisa wilayani hapo.
Baadhi ya vituo vya mafuta vimesitisha huduma. Pia majuzi nilisikia kuna sehemu hapa tz pia kuna shida ya mafuta.
Baadhi ya vituo vya mafuta vimesitisha huduma. Pia majuzi nilisikia kuna sehemu hapa tz pia kuna shida ya mafuta.
- Tunachokijua
- Julai 13, 2023, Mtumiaji mmoja wa JamiiForums alitoa taarifa inayodokeza uwepo wa uhaba mkubwa wa mafuta ya Petroli Wilayani Ngara.
Kwa mujibu wa maelezo yake, hiyo ilikuwa ni siku ya 4 mfululizo tangu uhaba huo wa mafuta uanze kuonekana.
Madai haya hayakuishia hapo. Julai 14, 2023, mtumiaji mwingine wa JamiiForums alizungumzia tatizo hilo kuwepo huko Liwale. Hali kadhalika, Julai 17, 2023, tatizo hili liliripotiwa kwa mara ya 3 kuwepo nchini.
Hali halisi ilivyo
JamiiForums imezungumza na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo aliyethibitisha uwepo wa changamoto hii. Amesema:
"Ni kweli kuna changamoto hususani maeneo mikoa iliyopo pembezoni kidogo, kulitokea hitilafu katika mfumo wa upakuaji, hivyo ukasababisa mafuta kuchelewa kufika katika maeneo ya mbali. Lakini mafuta yapo, yasingekuwepo ungeshuhudia Dar es Salaam kukiwa na changamoto."
"Kutokana na changamoto hiyo baadhi ya watu wamechukulia hali hiyo kununua mafuta kwenye madumu au Mapipa na kuuza kwa gharama ya juu, hali ambayo tunaichukulia kama ulanguzi.
"Mfumo wa usafirishaji nao unaleta changamoto ambapo lori linachukua siku nne hadi kufika Kigoma au Katavi au Kagera, hivyo kufanya huduma hiyo kusuasua.
"Changamoto ya ulanguzi hakuna anayejionesha na hakuna risiti anayopewa, bali tunasikia watu wakilalamika na kwa kuwa wanauziwa nje ya vituo hiyo ni Police Case, lakini cha muhimu tunafuatilia kumaliza tatizo hilo"
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ni taasisi ya udhibiti wa huduma za nishati na maji inayojitegemea, iliyoundwa kwa Sheria ya EWURA Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 2019.
EWURA, ilianza kazi rasmi Septemba, 2006 ikiwa na wajibu wa kusimamia shughuli zote za kiuchumi na kiufundi katika sekta za Nishati (umeme, petroli na gesi asilia); na Maji (majisafi na usafi wa mazingira).
Hii ni taarifa ya Julai 17, 2023.